Naombeni ushauri: Kwa hali hii maamuzi ya kuuza nyumba yatakuwa sahihi?

Fanya unachopenda na kila kitu ni sawa na kinaweza kuleta matunda makubwa ila usisahau majuto ni mjukuu

Na ndio maana wahenga walisema heri kenda shika kuliko kumi nenda uje

Sasa wewe uza kila ulichonacho halafu anza upya ndio utajua ya kuwa kwanini mabeberu walisema Roma haikujengwa siku moja
 
nsha nunua gari tatu sijawahi uziwa na dalali,,,,kwa hio sio kazi rahisi kwa upande wangu....rudi chini acha upredeshee fungulia mkeo hata genge msonge ukipata kibunda jaribu kubet huko kwenye udalali...mi nauonaga ni wizi na utapeli
 
Oya nyumba si yako uzaa...afuu chomoa kama milioni mbili njoo bar tuyajenge
 
Kaka, maamuzi ya kuuza nyumba ni makubwa na yanahitaji uangalizi wa kina. Kitu cha kwanza ni kujiuliza je, hii nyumba ni mali isiyohamishika ambayo inaweza kuwa faida kwako baadaye? Kama ukiuza sasa na mpango wa biashara mpya usifanikiwe, utakuwa na kitu gani cha kuangalia nyuma? Pia, soko la magari lina changamoto zake, hasa ukiwa mpya kwenye hiyo sekta.

Ikiwa unaamini kweli kwamba kuuza nyumba kutaweza kusaidia katika kuwekeza kwenye biashara yenye faida, basi unaweza kufikiria kuendelea. Lakini hakikisha unafanya utafiti wa kina juu ya biashara ya magari, haswa kuhusu uagizaji kutoka Japan, ili ujue changamoto na faida zake. Pia, ongea na mtu mwenye uzoefu ili akupe mwongozo wa kina kwenye biashara hii mpya.

Jipe muda wa kutafakari na kuhakikisha kuwa una back-up plan iwapo mambo hayataenda kama ulivyopanga.
 
Hii nyumba inathamani gani? Ukiuza unaweza kuagiza magari mangapi Toka japani? Nakushauri tulia utafute biashara TU ndogo na uendeshe maisha. Kubali kuishi maisha ya kawaida maana kama ulivyosema mambo yameyumba. Usipoikubali hiyo Hali inaweza kukugharimu zaid
 
Kama biashara umeifanyia utafiti wa kutosha , don't afraid to take risk .

Kikubwa usikurupuke.

Kuna MTU mmoja hapo amesema uendelee na udalali angalau mwaka mmoja then ukiona biashara imekubali itakuwa rahisi kuuza nyumba na kuwekeza katilka biashara unayoijua vzr.
 
Inaonekana unafanya mkumbo bila kutafakari. Hakuna mtu wanauza nyumbani kwenda kufanya biashara hata najijua haifahamu na hata kama anao fahamu nayo.
"life is an exam. People fail because they try to copy others but what they forget is that everyone has a different question paper"
 
Usiuze nyumba kama unapata hela ya kuendesha maisha yako, pangisha hiyo nyumba ukipata hela ya kodi anzisha biashara kwa mtaji mdogo ikue taratibu, kidogokidogo ndiyo mwendo
 
Kuuza nyumba yatakuwa ni maamuzi ya haraka,hauna tofauti na mtu anayechukua mkopo akaanze biashara,ikiwa bado hajasoma upepo.
 
Usiuze. Niliuza nyumba yangu kimasiala kama wewe, nikaongeza mtaji kwenye biashara yangu. Toka utawala wa Kikwete mpaka hivi leo sijawahi pata pesa kubwa ya kujenga nyumba kama ile na maeneo yale.
 
Acha Mara moja,umeshakiri huna uzoefu na hiyo biashara,kuuza aset na kuwekeza kwenye biashara usiyoielewa vyema sii poa.
Nafikiri ujifunze hiyo biashara mdogomdogo then ufanye maamuzi baadae sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…