Naombeni ushauri: Kwa hali hii maamuzi ya kuuza nyumba yatakuwa sahihi?

Kuna madalali wengi tu hapo kinondoni na kwingine hawana ofisi wanachofanya ni kuyapost magari mitandaoni wanashinda bar kusubiri wateja.

Unaweza fanya hivyo.
 
Kinachomfaa mtu chake! Nimetafsiri msemo huu kutoka kabila flani!

Kama nyumbani Ina thamani kubwa unaweza kuuza ukanunua nyumba yenye thamani ya kati ukapata mtaji!

HUWEZI KULA NYUMBA!
 
Chakula, Malazi na Mavazi... Katika Udalali wako unapata pesa ya kula ? Sasa unataka kuuza basic need moja ili ufanye biashara ambayo hauna uhakika nayo ?

The only way itakuwa ni sawa kuuza hio nyumba ni iwapo utakachopata kitakupa nyumba nyingine sehemu ya kuishi na itabaki pesa ya kuzungusha kupata kipato...

Kuhama sio mbaya ila kama nyumba unaweza kuipangisha ofisi au kitu kingine fanya hivyo...

Wealthy sio kuwa na pesa kiasi kingi benki bali income ya kutosha na consistently......
 
Huna uzoefu wa udalali wa kuuza magari halafu unataka kuuza nyumba utumie tobo ikiwa huna uzoefu?pata kwanza uzoefu halafu utajua kama hela yako itarudi.
 
Usije ukauza nyumba kisa kuja kifanya kazi ambayo huna uhakika nayo Dar
Nyumba ni asset , ardhi ni asset hvii vitu vinatabia ya kupanda bei muda unavyokwenda nadra sana kukutaa vinashuka thamani
Okay umezungumzia udalali hi kazi unaweza kufanya bila kuuza nyumba ni wewe kuwa online (matumizi mazuri ya mitandao) na kutafta wateja
Dalali kwenye baishara yyte hana hasara maana yeye sio mwenye mali yeye ni kiunganishi kati ya mwenye mali na mteja
 
Kutoka South mpaka kuja kuwa dalali bongo..bonge la msamba.
Hii akili na yeye pia anayo, ndio mana anashindwa kuishi bongo,kabeba usouthusouth kichwani kiasi kuokota makopo apate pesa ya kuishi anaona jau, Wana watamcheka,, anataka biashara zenye hadhi ya kisouth south, ningemshauri kitu jamaa, atune, apunguze mahitaji na vipaumbele, aanzie chini, this time ajitahidi kutafuta Hela ya kula tu, watoto awapeleke shule za kawaida, atangaze Hali ngumu ya kiuchumi kwa wife ili wife nae ajiandae kisaikolojia , kama mke ana hofu ya Mungu atavuka kipindi hiki, mana mwanamke kama siyo mwelewa ni kazi kufuata ushauri wangu, wanapenda sifa sana wanawake
 
Shukran mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…