Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Huyo mama ni komesha, yaani miezi 8 tangu mumewe afariki keshapata mtu wa kumuoa! Isijekuwa alikuwa anachepuka naye wakati mumewe akiwa bado yu hai.

Vv
 
Inawezekana sababu kubwa ni upweke. Mtafutieni ndugu hata watatu wa kukaa nae na afuge kuku,bata, mbuzi na vitu vingine vidogo vidogo vya kumuweka bize. Mfungulieni hata kiduka akae hapo. Hata mi siafiki kuolewa kwa umri huo na hasa chini ya mwaka tangu mzee atangulie
 
Mkuu achana nae ,huyo bi mkubwa ako, huko mjini unakopanga kumfungia ,walah atakudhalilisha makusudi ,atatongoza vijana wadogo wamtoe nyege. na ukienda kichwa kichwa atakuja kukwambia neno gumu hutaamini!! bimkubwa ako anapenda kwichikwichi[emoji23]. muache mzee wa watu nae ajitoleage maumivu ,si bola amempata mzee mwenzie ,je angewngua mikononi mwa vijana!!
 
Hajakataa, the issue is, amchukue mkewe akaishi naye kwake, na sio kukaa kwenye mji wa mwanamke.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Hajakataa, the issue is, amchukue mkewe akaishi naye kwake, na sio kukaa kwenye mji wa mwanamke.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
ni ngumu mkuu,bi mkubwa Kama kamuelewa huyo mzee.mzee atakuwa anakuja kulala tu hapo kwa bi mkubwa,kwani watakuwa wanamlinda anaingiza Nani!? Ila ajaribu kumwambia ,Ila ikishindikana akubali matokeo kuhusu uamuz wa bi mkubwa.
 
Pole sana kwa changamoto
Kuwa makini kwenye harakati za kuzuia ndoa. Wazazi wetu hawa wakati Mwingine wana maneno makali yakuumiza
Anaweza kukuambia “ unataka nifanya mpnz na nani au ukakuambia hisia ninazo nazitoa na nini “

Utakosa majibu
 
Mkuu acha mama aolewe Kama uyo mzee atakuja kuishi hapo home saw, ishi nao tu Kama wazazi maana ukianza kumpangia bmkubwa maisha utakuwa unamkosea chakufanya toa msaada uliondani ya uwezo wako
Mkuu, hebu fikiria huyo ndiyo mama yako wewe, utatoa ushauri huo? Nami naona hata KUCHEPUKA tu, na mimi mwanaye nikijua, nitajisikia aibu sana, nikizingatia huo umri wa kuhangaika na wajukuu!
 
Si ndio sisi hao waswahili
Wapo sawa maana kuna wengine kila wanavyozeeka ndio muwasho unazidi kuwa mkubwa.
Kuna bibi hapa mtaani kwetu yaani ile mishipa ya aibu yote imekatika Mungu amsaidie tu kwa kweli.
 
Huyo mama ana matatizo sio bure!
Umri miaka 68 mwanaume wa Nini?
 
Hivi hizi ndoa za uzeeni wanakulanaga au ni kampani tu.
 
Hapo inaonesha mzee marioo na huyu mama walikua wanakulana kitambo sana sabab umefiwa na mume alaf baada ya miezi nane unavuta mwanaume mwingine ni jambo la kufikirisha
 
Komaa huo upumbavu usikubali hata kidogo, wataanza kukukejeli na kuanza kuwaita majina yasiofaa, kama mama anataka kuolewa atoke kwenye huo mji wa mzee wako.

Na hata huyo mzee mkanye kabisa na usimuone kwenye mji wenu hapo nyumbani , kaza mwanzo mwisho huku ni kuleta aibu kwenye familia
 
Kama mama anaolewa na kuhama boma la marehemu mumewe fresh ruhusu kiroho safi,ila kama huyo fala anataka kuhamia kwenye boma la marehemu baba yenu usije kuruhusu kabisa iko kitu itakuja kuwa gharimu sana mbeleni.
 
Punguza wivuuu... Nyaauuu weeee..!!!
Samahani mkuu ni akili za balimi hizi.

#YNWA
 
Hii hathi ya kutunga au uhalisia?
Mama 68 years, anapata mchecheto kwa mzee mwenziwe?
Mbona hesabu zinakataa!
 
Hii hathi ya kutunga au uhalisia?
Mama 68 years, anapata mchecheto kwa mzee mwenziwe?
Mbona hesabu zinakataa!
Jidu La Mabambasi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daaah Jidu la Mabambasi

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Hilo huliwezi kama wewe ni muislamu. Mtume anasemaje katika hilo?...jibu liko hapo.

Kama ni Mkristo, mwambie point blank kuwa kuolewa baada ya baba kufa ni umalaya! Haimpi heshima. Mwambie waziwazi!

Ukristo upi unakataza kuoelewa tena? Baada ya kifo cha mwenza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…