Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Maandalizi ya kifo ni kwa kila rika, hakuna rika la kifo. Wapo watu wanaishi miaka 95 na wengine 30. Kila mtu anapaswa kujiandaa, na kujiandaa huko ni pamoja na kutafuta sitara ya ndoa baadala ya kugawa uroda vichochoroni.
Jamani jamano! Unataka kusema bibi wa 68 years atawashwa mpaka akagawe uroda vichakani🙆‍♀️
 
Mhhh inaonekana huyo alikuwa mzee mwenzake toka enzi za mdingi,mapenzi gani ya fasta hivyo,huyo babu alikuwa anasubiri tu mzee atangulie ajimilikishe bi mkubwa,anyway mshaurini bimkubwa kwa umri wake ni heri angepumzika alee wajukuu zake,lkn mkiona aelewi basi mruhusuni lakini mwambieni ahame aende huko huko kwa mzee mwenzake yakimshinda atarudi tu mwenyewe
 
UTAKUA Unakosea Sana kijana,
Mwache amalizie uhai wake, maisha Ni hapa hapa duniani[emoji4]
 
Jamani jamano! Unataka kusema bibi wa 68 years atawashwa mpaka akagawe uroda vichakani[emoji2296]
Unazijua nyege au unazisikia? Subiri ufikishe miaka 70 kama utakuwa huna nyege labda uwe na kisukari au bp lkn kama mzima wa afya utarudi jf kutoa mrejesho
 
Mhhh inaonekana huyo alikuwa mzee mwenzake toka enzi za mdingi,mapenzi gani ya fasta hivyo,huyo babu alikuwa anasubiri tu mzee atangulie ajimilikishe bi mkubwa,anyway mshaurini bimkubwa kwa umri wake ni heri angepumzika alee wajukuu zake,lkn mkiona aelewi basi mruhusuni lakini mwambieni ahame aende huko huko kwa mzee mwenzake yakimshinda atarudi tu mwenyewe
Hao wajukuu zake ndio watakuwa wanampa huduma anayopaswa kutoa mume?? Chunga ulimi wako bro
 
Kaa na huyo bi mkubwa wako muongee friendly,atakueleza mawazo yake nawe utampa maoni yako.Kama anakupenda atakusikiliza maana wazazi wanakawaida ya kuwasikiliza watoto wao wanaowapenda.
 
Ukristo upi unakataza kuoelewa tena? Baada ya kifo cha mwenza?
Haikatazwi Nakubaliana na wewe. Lakini kwa Heshima ya mume wako na watoto wako, achana na kuolewa! Especially if you are at an advanced age! Ukia kijana ukafiwa na mume, ruksa na Heshima kuolewa
 
Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.

Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi chote tangu sisi watoto wake tuanze kujitegemea tumekuwa tukijitahidi kuwawekea mazingira mazuri ya wazee wetu.

Pamoja na kuwajengea nyumba yenye hadhi na ya kisasa lakini tumehakikisha wazee wetu wanaishi maisha standard kuanzia chakula na mahitaji yote kiasi kwamba familia ya mzee wetu imetazamwa kama familia yenye nafuu pale kijijini.

Juzi ndugu zangu waliopo kijijni wamenitaarifu kwamba kajitokeza mzee anasema anataka kumuoa bi mkubwa. Nikauliza akishamuoa ataondokanae kwa maana bi mkubwa atahama mji tuliomjengea na mzee? Wakaniambia hapana inavyoonyesha huyu mzee kafuata maisha mseleleko.

Binafsi nimejiuliza je ni sahihi mama alete mwanaume kwenye kitanda alicholala na mzee wetu? Je ni kweli nyumba tuliowajengea wazee wetu mama atumie kuishi na mzee mwingine? Alifanyalo mama sio kutufedhehesha sisi watoto tunaohakikisha anapatiwa chochote akitakacho?

Uamuzi wangu nimepanga kuvuruga mpango wa bi mkubwa. Nataka nimwite nimuombe nije niishi nae mjini kwa maisha yake yote ili nizuie mipango yake na akikataa nimepanga sitomuhudumia chochote maana Mimi ndie mwanawe mpendwa.

Je, ndugu uamuzi wangu huu nitakuwa namkosea mama yangu? Au nimwachie tu ahangaike na maisha yake? Kinachoumiza mzee muoaji mwenyewe kachoka mno hata ndala anazovaa ukute zina matundu nusu anagusa ardhi nusu malapa.

Naona kama bi mkubwa atatuongezea mzigo wa kuangalia watu wawili kwa maana akibaki mwenyewe inakuwa rahisi hata kumchukua wakati wowote. Ushauri wenu
Hebu muheshimu mama yako kuwa na adabu
 
Muache mama afanye roho yake itulie. Cha muhimu wewe nenda mapema huko tafuta wakili na mwenyekiti wa mtaa na mashaidi. Mama akabidhi urithi kwa watoto kwa mali zilizopo, kiwepo kipengele cha kutotambua ndoa nyingine kwenye urithi wa mali zilizopo. Hiyo itakuwa njia sahihi kuliko kumkataza mama.
 
Back
Top Bottom