Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Ushauri wangu ni was kikatili sana kama upo tayali njoo PM nikutonye!

Mimi sipendagi kuumiza kichwa mambo madogo kama hayo!

Narudia tena njoo PM nikupe ushauri wa kikatili kama ataponyoka wallah nakuapia hata tamani kuishi hapo kijijin wala puan atasogeza kwenu
Daaaah wewe jamaa una roho ngumu sana, are you Hitler?

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Mama Kuolewa hilo huwezi kuzuia kama wengi wanavyo sema, ila kuolewa halafu aendelee kuishi na huyo mwanaume hapo nyumbani hilo linaleta ukakasi kwa kweli. Mwanaume aoe aende naye kwake na sio yeye ahamie hapo nyumbani hilo hapana.
Ni kweli hilo la mama kuolewa hawezi kuzuia.....Shida ninayoiona hata Mimi kuleta mwanaume kwenye nyumba ya familia ni kuwanyima watoto Uhuru...halafu mzee ni choka mbaya hapo anaona amepata opportunity atawatesa hao watoto maana itabidi wamhudumie indirect...umeshawahi kujiuliza mzee akiugua nani atamtibu akiwa anaishi humo.? Ama kweli dunia INA mambo.
USHAIRI:-
Watoto watafute wazee wa ukoo kumdhibiti mama asilete mwanaume nyumbani!
 
Halafu ana 68! Ana haki yake lakini mambo mengine yanafikirisha sana. Ningekuwa nampa ushauri, ningemshauri akae na wanae na wajukuu basi. Mzee wangu alifariki akatuacha na mama. Mama akiwa na miaka 47 tu. Mama hakuolewa tena. Alikaa nasi wanae mpaka mwisho wake. Wala sikuwahi kumsikia hata na mtu wa pembeni. Mama ubarikiwe sana.
Miezi 8 mother anavuta jiko duuh
 
Mimi ujinga huo mama aliukata mwenyewe kaza homeboy uwezi kushindwa unajua vizeee hivi vinapenda sana mtelemko
 
Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.

Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi chote tangu sisi watoto wake tuanze kujitegemea tumekuwa tukijitahidi kuwawekea mazingira mazuri ya wazee wetu. Pamoja na kuwajengea nyumba yenye hadhi na ya kisasa lakini tumehakikisha wazee wetu wanaishi maisha standard kuanzia chakula na mahitaji yote kiasi kwamba familia ya mzee wetu imetazamwa kama familia yenye nafuu pale kijijini.

Juzi ndugu zangu waliopo kijijni wamenitaarifu kwamba kajitokeza mzee anasema anataka kumuoa bi mkubwa. Nikauliza akishamuoa ataondokanae kwa maana bi mkubwa atahama mji tuliomjengea na mzee? Wakaniambia hapana inavyoonyesha huyu mzee kafuata maisha mseleleko.

Binafsi nimejiuliza je ni sahihi mama alete mwanaume kwenye kitanda alicholala na mzee wetu? Je ni kweli nyumba tuliowajengea wazee wetu mama atumie kuishi na mzee mwingine? Alifanyalo mama sio kutufedhehesha sisi watoto tunaohakikisha anapatiwa chochote akitakacho?

Uamuzi wangu nimepanga kuvuruga mpango wa bi mkubwa. Nataka nimwite nimuombe nije niishi nae mjini kwa maisha yake yote ili nizuie mipango yake na akikataa nimepanga sitomuhudumia chochote maana Mimi ndie mwanawe mpendwa.
Je ndugu uamuzi wangu huu nitakuwa namkosea mama yangu? Au nimwachie tu ahangaike na maisha yake? Kinachoumiza mzee muoaji mwenyewe kachoka mno hata ndala anazovaa ukute zina matundu nusu anagusa ardhi nusu malapa. Naona kama bi mkubwa atatuongezea mzigo wa kuangalia watu wawili kwa maana akibaki mwenyewe inakuwa rahisi hata kumchukua wakati wowote. Ushauri wenu

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Ndugu yangu usimwimgilie mama kwenye.maamuzi yake jua mama ana radhi kubwa sana hayo ni matokeo mzazi mmoja akifariki hata baba angefanya hivyo kwa hyo kubali yaishe kunjua moyo kijana wa kiume mpokee baba mpya kwa upendo kabisa hisia zinakufa unapokufa jua hivyo...
 
Maamuzi ya mama yaheshimiwe, haki ya watoto itunzwe. Anae muoa amchukue nanyi mtaenda kumsalimia huko kwake. Kumleta mume ndani watoto msikubali. Ni kuwavunjia heshima. Ni uthibitisho mama alikuwa na mchepuko wakati wa uhai wa ndoa yao. Akiwakatalia mwache atekeleze, kateni misaada.
 
Miaka 68... Bi mkubwa anataka vita tu na wanae
 
Ndugu yangu usimwimgilie mama kwenye.maamuzi yake jua mama ana radhi kubwa sana hayo ni matokeo mzazi mmoja akifariki hata baba angefanya hivyo kwa hyo kubali yaishe kunjua moyo kijana wa kiume mpokee baba mpya kwa upendo kabisa hisia zinakufa unapokufa jua hivyo...
Sawa ila amchukue amchukue mkewe akaishi naye kwake, na si kubanana hovyo hovyo kwa watoto.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Pole kwa changamoto ila kiuhalisia mama anahitaji mtu wa kumpa kampani
Tatizo ni kwamba huyo mzee anataka ahamie kwenu hili ndio linakupa ukakasi
Mama yako ndio anae olewa so ni vema akaenda kwa mumewe na sio yeye kumleta senior marioo hapo kwenye mji wa family yenu
huyo babu atakua very very sinior marioo[emoji1][emoji1]

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Maamuzi ya mama yaheshimiwe, haki ya watoto itunzwe. Anae muoa amchukue nanyi mtaenda kumsalimia huko kwake. Kumleta mume ndani watoto msikubali. Ni kuwavunjia heshima. Ni uthibitisho mama alikuwa na mchepuko wakati wa uhai wa ndoa yao. Akiwakatalia mwache atekeleze, kateni misaada.
Yes

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
68 halafu anataka kuolewa,ngoja nitafakari kwanza nitarudi na coment yangu
 
Ndugu yangu usimwimgilie mama kwenye.maamuzi yake jua mama ana radhi kubwa sana hayo ni matokeo mzazi mmoja akifariki hata baba angefanya hivyo kwa hyo kubali yaishe kunjua moyo kijana wa kiume mpokee baba mpya kwa upendo kabisa hisia zinakufa unapokufa jua hivyo...
Ni kweli, ugumu ni kwamba mzee anataka kuishi kwenye makazi ya mzee.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Pole kwa changamoto ila kiuhalisia mama anahitaji mtu wa kumpa kampani
Tatizo ni kwamba huyo mzee anataka ahamie kwenu hili ndio linakupa ukakasi
Mama yako ndio anae olewa so ni vema akaenda kwa mumewe na sio yeye kumleta senior marioo hapo kwenye mji wa family yenu
Hata Mimi nongempa ushauti Kama wako,hongera.
 
Bi mkubwa anatafuta nini kuolewa sahizi na jua lishazama huu ni wakati wa kusali tu na kucheza na wajukuu..
 
Back
Top Bottom