Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Hauwezi kumpangia mama yako kitu Cha kufanya.
Hakuna umri ambao mwanamke akifika inakuwa mwisho kuolewa.
Anayelala na Mama ndo baba.
Ila Kama Mama Mungu Akimpenda hapo Sasa ndo mnaamua kuchukua maamuzi magumu.
Kama nyumba,gari na Mali zingine zimeandikwa kwa jina la mama shida IPO wapi?
Jamani huyu mrembo 68 years anataka nini? Au mzee huna watoto wa kumkeep bize bibi? Nashauri mhamishie mjini aje kucheza na wajukuu. Huyo babu/ mchumba ni opportunist tuu anataka mtelemko. Ila pia bibi aambiwe ukweli akitaka kuolewa akukabidhi funguo. Tena mwambie mta-msend off kabisa ajue kwenu kaondoka
 
Pole kwa changamoto ila kiuhalisia mama anahitaji mtu wa kumpa kampani
Tatizo ni kwamba huyo mzee anataka ahamie kwenu hili ndio linakupa ukakasi
Mama yako ndio anae olewa so ni vema akaenda kwa mumewe na sio yeye kumleta senior marioo hapo kwenye mji wa family yenu
Sasa kwa mfano ikitokea na maza kavuta ina maana huyo mzee wake atabaki hapo nyumbani analelewa au ataondoka??
 
Bibi yangu kaolewa akiwa na miaka 50 na kitu na mzee mwenzie.
Bibi alipofariki mama zangu wadogo na wajomba wakamwambia ukweli Yule baba yao.
Mama kaondoka na wewe Safari yako imeishia hapa.
Kwa kuwa nyumba kaikuta imeshajengwa.
Ila kwa kuwa wewe kichwani ni MATOPE huyo baba anaweza kukudhulumu
Si kila mzee ni huyo aliyemuoa bibi yako.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Umenifanya niimagine kama dingi anavuta sasa hivi halafu baada ya miezi 8 bi mkubwa anatuambia anataka kuolewa, hahahahaha hakuna ndoa itapita hapo, siwezi mruhusu Bi Mkubwa aende kwa huyo Mwanaume na huyo Mwanaume hatoruhusiwa kupeleka lipua lake pale, dadekiiiii

Pole Mwamba huo mtihani ila ongea na Bi mkubwa vizuri aachane na mambo ya kuolewa, kwanza ni muda mfupi sana pili kumleta huyo mzee hapo ndani sio fair, lakini na yeye sio poa kwenda kwenye nyumba za watu huko akapate tabu wakati mjengo wake upo na watoto wanasababisha bila wasi.
 
Angekua Ni mtu wa imani
Asingepata huo muda wa kufikiria kuolewa

Kwa huo umri kwanini asianze kujitayarishia mazingira mazuri ya huko aendako?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maandalizi ya kifo ni kwa kila rika, hakuna rika la kifo. Wapo watu wanaishi miaka 95 na wengine 30. Kila mtu anapaswa kujiandaa, na kujiandaa huko ni pamoja na kutafuta sitara ya ndoa baadala ya kugawa uroda vichochoroni.
 
Binafsi naona sio sawa kwa mama kuolewa na kuleta mme hapo nyumbani.
Nyumba ilijengwa kwa ajili ya makazi ya wazazi waliowazaa yaan baba na mama yao (waliowazaa). Mmoja ameondoka hvyo nyumba ilitakiwa iendelee kubaki na heshima yake. Iheshimiwe kana kwamba baba mzazi bado tu hai.
Mama alitakiwa atulie amuombee dua mumewe huko alipo apumzike salama lakini bimkubwa anataka kuendelea kutesa na dunia ili Hali umri umeishaenda, anyway kuolewa sio dhambi lakini kumleta mwanaume hapo home n dhambi na mkiwa kama watoto mliojenga nyumba Hiyo mnahaki ya kukataa mume huyo kuishi hapo na hakuna lolote linaweza kuwapata.
 
It's challenge.

Wamama tunahitaji pia kampanyi upweke nao ni ugonjwa.

Usimchukue mama hataelewana na mkeo.

Mpe kiasi kile kile unachimpa maana hata hivyo ukute anampa pia huyo baba.

Waache,
 
Ushauri wangu ni was kikatili sana kama upo tayali njoo PM nikutonye!

Mimi sipendagi kuumiza kichwa mambo madogo kama hayo!

Narudia tena njoo PM nikupe ushauri wa kikatili kama ataponyoka wallah nakuapia hata tamani kuishi hapo kijijin wala puan atasogeza kwenu
 
Kwa mila za kwetu akitaka kuolewa haina shida, ila lazima atoke nyumbani aende kuishi kwa huyo mwanaume. Uliza wazee wa huko kwenu utaratibu ukoje.
 
Kama unaweza kumtimizia mahitaji ya kihisia mzuie mzee

ova
 
Pole kwa changamoto ila kiuhalisia mama anahitaji mtu wa kumpa kampani
Tatizo ni kwamba huyo mzee anataka ahamie kwenu hili ndio linakupa ukakasi
Mama yako ndio anae olewa so ni vema akaenda kwa mumewe na sio yeye kumleta senior marioo hapo kwenye mji wa family yenu
Very good. Simple solution!
Muombe baba (baba yako mtarajiwa) wakaishi naye kwake, ili mfahamiane vizuri na ndugu zenu wengine(watarajiwa), msije mkawaoa!
 
Pole kwa changamoto ila kiuhalisia mama anahitaji mtu wa kumpa kampani
Tatizo ni kwamba huyo mzee anataka ahamie kwenu hili ndio linakupa ukakasi
Mama yako ndio anae olewa so ni vema akaenda kwa mumewe na sio yeye kumleta senior marioo hapo kwenye mji wa family yenu
Senior marioo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom