Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Daaaah wewe jamaa una roho ngumu sana, are you Hitler?

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Mama Kuolewa hilo huwezi kuzuia kama wengi wanavyo sema, ila kuolewa halafu aendelee kuishi na huyo mwanaume hapo nyumbani hilo linaleta ukakasi kwa kweli. Mwanaume aoe aende naye kwake na sio yeye ahamie hapo nyumbani hilo hapana.
Ni kweli hilo la mama kuolewa hawezi kuzuia.....Shida ninayoiona hata Mimi kuleta mwanaume kwenye nyumba ya familia ni kuwanyima watoto Uhuru...halafu mzee ni choka mbaya hapo anaona amepata opportunity atawatesa hao watoto maana itabidi wamhudumie indirect...umeshawahi kujiuliza mzee akiugua nani atamtibu akiwa anaishi humo.? Ama kweli dunia INA mambo.
USHAIRI:-
Watoto watafute wazee wa ukoo kumdhibiti mama asilete mwanaume nyumbani!
 
Halafu ana 68! Ana haki yake lakini mambo mengine yanafikirisha sana. Ningekuwa nampa ushauri, ningemshauri akae na wanae na wajukuu basi. Mzee wangu alifariki akatuacha na mama. Mama akiwa na miaka 47 tu. Mama hakuolewa tena. Alikaa nasi wanae mpaka mwisho wake. Wala sikuwahi kumsikia hata na mtu wa pembeni. Mama ubarikiwe sana.
Miezi 8 mother anavuta jiko duuh
 
Mimi ujinga huo mama aliukata mwenyewe kaza homeboy uwezi kushindwa unajua vizeee hivi vinapenda sana mtelemko
 
Ndugu yangu usimwimgilie mama kwenye.maamuzi yake jua mama ana radhi kubwa sana hayo ni matokeo mzazi mmoja akifariki hata baba angefanya hivyo kwa hyo kubali yaishe kunjua moyo kijana wa kiume mpokee baba mpya kwa upendo kabisa hisia zinakufa unapokufa jua hivyo...
 
Maamuzi ya mama yaheshimiwe, haki ya watoto itunzwe. Anae muoa amchukue nanyi mtaenda kumsalimia huko kwake. Kumleta mume ndani watoto msikubali. Ni kuwavunjia heshima. Ni uthibitisho mama alikuwa na mchepuko wakati wa uhai wa ndoa yao. Akiwakatalia mwache atekeleze, kateni misaada.
 
Miaka 68... Bi mkubwa anataka vita tu na wanae
 
Sawa ila amchukue amchukue mkewe akaishi naye kwake, na si kubanana hovyo hovyo kwa watoto.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
huyo babu atakua very very sinior marioo[emoji1][emoji1]

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Yes

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
68 halafu anataka kuolewa,ngoja nitafakari kwanza nitarudi na coment yangu
 
Ni kweli, ugumu ni kwamba mzee anataka kuishi kwenye makazi ya mzee.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Hata Mimi nongempa ushauti Kama wako,hongera.
 
Bi mkubwa anatafuta nini kuolewa sahizi na jua lishazama huu ni wakati wa kusali tu na kucheza na wajukuu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…