Naombeni ushauri nataka kuuza mali zangu polepole nifurahie maisha urithi kwa watoto ni elimu niliyowasomesha mnasemaje?

Naombeni ushauri nataka kuuza mali zangu polepole nifurahie maisha urithi kwa watoto ni elimu niliyowasomesha mnasemaje?

Nani kakuambia elimu ni urithi?
Elimu ni kama hitaji la kawaida kwa mtoto kama ugali.
Mpe mtoto urithi unaoshikika yaani shamba, chombo cha usafiri, biashara, mgodi nk.
HEBU TOFAUTISHA HII MIATARI MIWILI YA BIBLE HAPA CHINI.

Methali 13:22 BHND
[22] Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake, lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu.

Methali 22:6 BHND
[6] Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni.

HAA!! 🙄🙄

Wakati wengine tunafikiria kuongeza assets za kutosha kumbe kuna wengine wanafikiria kuzila.
 
Sina mali nyingi ila nashukuru Nina nyumba kadha wa kadha, viwanja , mashamba na mifugo kijijini kwetu.
Watoto wangu wanasoma na watamaliza bila shaka. Nimetafakari haya maisha hayana garantii naweza kufa saa yeyote je kwanini nisianze kula mali zangu taratibu kabla sijafa? Naombeni ushauri.
Fanya haraka tena chap kwa upesi usichelewe zaidi
 
Sina mali nyingi ila nashukuru Nina nyumba kadha wa kadha, viwanja , mashamba na mifugo kijijini kwetu.
Watoto wangu wanasoma na watamaliza bila shaka. Nimetafakari haya maisha hayana garantii naweza kufa saa yeyote je kwanini nisianze kula mali zangu taratibu kabla sijafa? Naombeni ushauri.
Urithi wa watoto ni elimu ni kauli ya wazazi wavivu, moja ya kauli za kimaskini. Watu wa jamii wa asia wangekuw ana mindset hizo wasingefika hapa
 
Na hii ndio sababu kubwa kwanini ngozi nyeupe inatuzidi mbali, sisi ni wabinafsi sana tunataka tunapopotea kwenye uso wa dunia basi tupotee na kila kitu chetu tulichofanikiwa kuwa nacho.

Hii ni roho ya kuendeleza umasikini kizazi hadi kizazi, kuna hasara gani wanao, wajukuu, wakinufaika na matunda aliyopanda baba/babu yao?
Hapo sasa yani ni upumbavu wa kiwango cha sgr....
 
Hakuna heshima yenye kumbukumbu na ya kudumu kama heshima ya muda mfupi. Fanya jambo mkuu, familia itakukumbuka mpaka vitukuu vyako
 
Sina mali nyingi ila nashukuru Nina nyumba kadha wa kadha, viwanja , mashamba na mifugo kijijini kwetu.
Watoto wangu wanasoma na watamaliza bila shaka. Nimetafakari haya maisha hayana garantii naweza kufa saa yeyote je kwanini nisianze kula mali zangu taratibu kabla sijafa? Naombeni ushauri.
Kwani ulikuja na nini hapa duniani mkuu? Kwa uhakika 100% utaondoka bila kitu. Sana-sana watakupa kiwanja cha ft. sita kwa sita au pungufu ya hapo kiwe ni mali yako.
 
Kasome hiki kitabu hata kama we si mkristo utajifunza tu kitu

TAJIRI MPUMBAVU Luka 12:13-21
 
Ni vizuri ukaishi kwa kuamini kuwa ni "bora ufe uache mali kuliko mali kuisha ukiwa hai", maana ikitokea mali iishe ukiwa hai ni mateso.
 
Back
Top Bottom