Naombeni ushauri wa biashara ya juice ya miwa, mtaji ni milioni 1-2

Naombeni ushauri wa biashara ya juice ya miwa, mtaji ni milioni 1-2

kwa dar mkuu nauhakika ni sehemu sahihi...cha msingi usirudi nyuma kama akili ishakutuma kufanya iyo biashara kinachotakiwa ni kuanza tu utekelezaji...make sure iyo sehemu kama kuna muingiliano wa watu,kwa pembeni ya biashara yako kama kuna nafasi weka hata mabenchi mawili na drafti/bao watu wawe wanacheza na ka draft/bao pembeni...iyo itakuongezea wateja...but zingatia usafi usafi usafi mkuu....ukifanikiwa kufungua kama utakuwa interested usisite kuni alert maweza kukushauri na vitu vingine unavyoweza kuviongezea kwenye biashara yako sababu wakati mwingine biashara moja inaweza zalisha biashara nyingine...kila la kheri mkuu
Kuna kipindi nilikua namiliki duka la nguo..bas nikawa najaza mashost mle dukan wanalala tu chinu kwa tiles huyu ataagiza kiepe alie ndani..huyu juic huyusoda! Nk nk...mwingine atavya tite inambana yaan vuruge mechi tu.!

Basi mume akija saa12 anipitie twende home ananiwakia balaa .nikawa naona ananibania tu nisiwe na marafiki my friendukitaka kuharibu biashara weka hizo bench sijii viti ( maana walikopa had wengine had leo wana deni) mtu anakuja anakaa na sio mteja .na kuna watu akishaona nyomi la watu haji ng'o!.

Yaani uweke mchezo wa bao kwenye kilinge cha juice? Ustaarabu utaenda kwao! Sanasana utakopwa na hao washikaji na wasilipe kwa wakati...! Ni sumu sana kwa biashara!
 
Mie naogopa kukushauri watakuja manguli watasema hee na hii unaijua[emoji38]!..lakini kifupijuice ya miwa=popcorn ...! Sijui kama bado watu wanakimbilia miwa pale kariakoo gerezani dadek maisha haya!..imepoa!kidogo nitenguke kiuno kugombea miwa[emoji56]! Tena kama unamkabidhi mtu atauza atakuwa anakupa za glass kumi tu !
all the best
Asante, sema tu wala usiogope, mm mwelewa my dear,napembua siwezi beba kila kitu,nasoma nakupima mambo, karibu usishindwe kunipa wazo zuri kwasababu yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu. Wengi hawajui kuwa ''mtaji wa mawazo'' ni muhimu kuliko hata ''mtaji wa fedha''. Na mtaji wa mawazo kama ulivyo mtaji wa fedha chanzo chake ni wewe mwanzisha biashara mwenyewe. Kama ambavyo huwezi kutegemea watu kwenye kupata mtaji wa fedha basi hata kwenye mtaji wa mawazo huwezi kuwategea.

Sure mkuu...ukitaka kupata pesa toa pesa...! Toa hela mfukoni upate unachotaka ...! Mie kabla sijaianza nilitengeneza urafiki na mdada pale kariakoo..ikawa kila siku natoka goig naenda kariakoo..namuungisha nakaa naanza mhoji maswaki...nikaomba anifundishe kusaga....yaan unaondoka umejaza madini ni uamuz wako wewe .

Haiwezekan kwa siku akuambia analaza 80 unakubali...kaa kbs ona anachofanya...!peleleza kwa hali na mali...mie sasa hivi kusafiri naonakawaida tu ingawa mtu mwingine anaweza ona napoteza hela...usisubiri mafanikio yakukute..yafate! Mwe nnaandika sana!
 
Kuna kipindi nilikua namiliki duka la nguo..bas nikawa najaza mashost mle dukan wanalala tu chinu kwa tiles huyu ataagiza kiepe alie ndani..huyu juic huyusoda! Nk nk...mwingine atavya tite inambana yaan vuruge mechi tu.!
Basi mume akija saa12 anipitie twende home ananiwakia balaa .nikawa naona ananibania tu nisiwe na marafiki my friendukitaka kuharibu biashara weka hizo bench sijii viti ( maana walikopa had wengine had leo wana deni) mtu anakuja anakaa na sio mteja .na kuna watu akishaona nyomi la watu haji ng'o!.yaani uweke mchezo wa bao kwenye kilinge cha juice? Ustaarabu utaenda kwao! Sanasana utakopwa na hao washikaji na wasilipe kwa wakati...! Ni sumu sana kwa biashara!
Nikweli ulichosema na umenifungua kwa kiasi flani,cha msingi ni kusoma tu mazingira yanataka nini...mi mejaribu ku copy na ku paste,kuna jamaa niliona kigamboni anafanya hivyo na anawateja wengi so mejaribu kumpa tha same idea..but cha msingi ni kuangalia tu mazingira na aina ya wateja yanataka nini coz kuna wateja kweli huwa hawapendi kwenda kwenye biashara yenye mazingira kama hayo
 
Kaka/dada, habari yako!

Duniani hakuna biashara mbaya, biashara zote ni nzuri, zinahitaji tu heshima katika usimamizi

Asikudanganye mtu biashara mbaya usijaribu! la msingi tengeneza mazingira mazuri hakikisha unaiheshimu hiyo biashara na kama utaweka mtu basi jitahid sana kuwa kribu nae!

Ona wakina BOBPACK wameziheshimu biashara ya kuuza movie sh 1500 leo wako wapi, ona wakina MakJuice na biashara zao za juice ambazo kwa hali ya kawaida hatukutegemea leo wako wapi

asikwambie mtu, nenda kachukue fedha wekeza, na kuwa mbunifu, fuata mazingira ya usafi
 
Sijui kwanini comment yako imenifanya nikacheka sana! Mambo ni faya aisee
Labda na mm niseme kitu kwa hili

Mm nishaenda rufiji, mambo yapo hv
1: water pump 350000-400000
2: shamba 300000
4: kulima (70000*2 = 140000
5: kuandaaa
6: mipra wa maji (250000
7:......
Na zingine nyingi

Mwisho.kabisa kutoka pale ruvu daraja hadi mashambani lazima upande bodaaa


All the best
 
Kuna kipindi nilikua namiliki duka la nguo..bas nikawa najaza mashost mle dukan wanalala tu chinu kwa tiles huyu ataagiza kiepe alie ndani..huyu juic huyusoda! Nk nk...mwingine atavya tite inambana yaan vuruge mechi tu.!
Basi mume akija saa12 anipitie twende home ananiwakia balaa .nikawa naona ananibania tu nisiwe na marafiki my friendukitaka kuharibu biashara weka hizo bench sijii viti ( maana walikopa had wengine had leo wana deni) mtu anakuja anakaa na sio mteja .na kuna watu akishaona nyomi la watu haji ng'o!.yaani uweke mchezo wa bao kwenye kilinge cha juice? Ustaarabu utaenda kwao! Sanasana utakopwa na hao washikaji na wasilipe kwa wakati...! Ni sumu sana kwa biashara!
😀😀Hivi ushafanya biashara ngapi?
 
😀😀Hivi ushafanya biashara ngapi?
Well... success is a process !1, duka la mangi(2009-2012 niliacha waliniibia kila kitu)
..2: mitumba 2012-2015 alipoingia jpm ikaharibika..nihamia za dukani...wakanipigia mzigo wote kkoo ( kumbuka nna kaajira pia .so jion ndo nakaa dukani)..😆😆😙..2016 nikaingia kwa kilimo..tikiti... Mchicha , pilipili tango, tembele..strawberry till 2018 nilipopata ajali nikaachana na kilimo kabisa!
2019- ( hapa kuna juice ya miwa, mikopo midogo dogo, mama lishe)-till date nimeamua kuwa msafiri kafiri😊!( nafind solutions zaidi)

Nadhani nna idea zaidi kwa kilimo coz nimezaliwa kwa familia inayopractice sana kilimo cha kisasa na ufugaji🐂🐂!
kifupi hela naimanya vilivyo na inajua najua kuifata ...ugumu naumanya!

Pia kwa biashara nna idea nzur tu coz dingi had leo anapractice...so usishangae ukaniona nacomment hata kwenye mbishe za mbao...anaifanya sana hii so nna idea nayo coz sipendi kupitwa... Hutaniona nacomment kwenye alizet, dengu, rupia..et all! na mazao mengine!

Relax....!Iam not just a sweet talker!
Napenda maisha yasio na bugudha za hela kwahyo dawa ni kuzitafuta kwa hali na mali!
 
Labda na mm niseme kitu kwa hili

Mm nishaenda rufiji, mambo yapo hv
1: water pump 350000-400000
2: shamba 300000
4: kulima (70000*2 = 140000
5: kuandaaa
6: mipra wa maji (250000
7:......
Na zingine nyingi

Mwisho.kabisa kutoka pale ruvu daraja hadi mashambani lazima upande bodaaa


All the best


Msome tena sigara kali..uendeleze ulipoishia...ulichoandika na yeye tofauti!
 
Biashara ya car wash unaanza na pump moja ya dizel/umeme kulingana na sehemu uliopo au biashara ya chipsi inalipaaa,hata kipindi cha lockdown walikua wanauzaa na watu tulikua tunakula chipsi na mishikakii kwa kiwango cha lamii,tafuta Uzi huku kuhusu mchanganuo wa kufungua car wash/ banda la chips,eneo,wafanyakazi na usafi wa sehemu husika.kila la heri mkuuu
Screenshot_20200527-011045.jpeg
 
Nimesoma mengi hapa na kujifunza sana.
Ushauri wangu kwa mtu yoyote anayependa kufanya biashara ajitahidi kufahamu haya machache. Kwangu mimi yamenisaidia sana.

Kufanya biashara sio jambo rahisi, na kutengeneza faida ya uhakika kutoka kwenye biashara ni jambo gumu zaidi. Kama huamini jaribu kufanya biashara.!

Sio vizuri kuanza kufanya biashara kwa kutumia pesa za mkopo. Mkopo una maana kubwa kwenye kupanua mtaji wa biashara iliyokwisha anzishwa tayari na sio kuanzishia biashara.

Usitegemea kuvuna faida kirahisi kwa kuanzisha biashara na kuweka mtu wa kuifanya. Jaribu kuanza kuifanya wewe mwenyewe kabla ya kuajiri mtu.

Kama huna muda wa kuisimamia biashara yako wewe mwenyewe basi usifanye hiyo biashara kabisa! Biashara yako inakuhitaji wewe mwenyewe, uwepo wako, muda wako na Akili yako yote. Kadri ambavyo unakuwa mbali na biashara yako ndivyo ambavyo faida inapungua, hasara inakaribia na biashara ina lega lega. Ni biashara chache, kwa watu wachache tena baada ya kukua na kukomaa ndio ambavyo zinaweza kwenda bila uwepo wapo wa moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom