Naombeni ushauri wa kisheria kuhusu bomba kubwa la maji kupita kwenye uwanja wangu!

Naombeni ushauri wa kisheria kuhusu bomba kubwa la maji kupita kwenye uwanja wangu!

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Mdogo wangu amejikusanya na kununua kauwanja anakotaka kujenga nyumba ya kuishi ajabu wakati mafundi wanachimba msingi wamekutana na bomba kubwa la maji hali ambayo hatukuitarajia!

Wadau tunaomba ushauri wa kisheria wa nini kifanyike
 
Mdogo wangu amejikusanya na kununua kauwanja anakotaka kujenga nyumba ya kuishi ajabu wakati mafundi wanachimba msingi wamekutana na bomba kubwa la maji hali ambayo hatukuitarajia!Wadau tunaomba ushauri wa kisheria wa nini kifanyike
Fafanua boss bomba la mradi wa serikali au binafsi
 
Asijaribu kabisa kujenga kabisa hapo,

Kama uwanja umekuwa mdogo akatafute sehemu nyingine (alipigwa kuuziwa kwenye bomba maana kalikuta) ni mali ya jamii hiyo.

kwahiyo hawezi kushinda hiyo kesi.!
 
Najifunza hapa. Nina rafiki yangu aliuziwa kiwanja baadae akaambiwa chini kuna bomba la maji limepita. Wakamshauri akashughulikie hati kwanza ndiyo aweze kulitoa kwa gharama ya serikali juzi tu aliniambia kapata hati. Nasubiri anipe mrejesho.
 
Fafanua boss bomba la mradi wa serikali au binafsi
Mahali ambapo hilo shamba lilinunuliwa na ambapo kwa sasa watu tayari wamegeuza kama viwanja na kuanza kujenga nyumba za heshima kwa mbele kuna kijiji!Hilo bomba linapeleka maji kijijini!Lina ukubwa wa mpapai!
 
Najifunza hapa. Nina rafiki yangu aliuziwa kiwanja baadae akaambiwa chini kuna bomba la maji limepita. Wakamshauri akashughulikie hati kwanza ndiyo aweze kulitoa kwa gharama ya serikali juzi tu aliniambia kapata hati. Nasubiri anipe mrejesho.
Huyu wangu kaenda kupigiwa gharama za hati kaambiwa milioni 7!Kauliza sababu akajibiwa kuwa yuko mbali sana na eneo lililopimwa!Hadi katolewa mfano eti ni sawa na abiria mmoja anaenda kukodi basi la abiria 100,limpeleke yeye peke yake toka DAR hadi Bukoba
 
Mdogo wangu amejikusanya na kununua kauwanja anakotaka kujenga nyumba ya kuishi ajabu wakati mafundi wanachimba msingi wamekutana na bomba kubwa la maji hali ambayo hatukuitarajia!Wadau tunaomba ushauri wa kisheria wa nini kifanyike
Hapo wewe ndiye umelifwata bomba na sio bomba limekufwata. Ingekua bomba limekufwata ungelipwa fidia au wangepitisha bomba route ingine.

Kwa maelezo yako hilo ni bomba la inch 3 au 4, sasa ukijenga juu yake alafu likapata hitilafu huoni nyumba yako itaweza pata shida pia?

Je siku wakitaka kulifanyia matengenezo watafanyaje wakati wewe umejenga juu yake?

Mkuu kujenga juu ya bomba maana yake una hatarisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi..
 
"...kwa nguvu za wanakijiji..."

Siku ikitokea shida utaisoma namba.
Eti kaka mnashauri nini kifanyike?Jamaa anafikiria ajenge hivyo hivyo maana jirani yake amefumba macho na kujenga juu yake
 
Hapo wewe ndiye umelifwata bomba na sio bomba limekufwata. Ingekua bomba limekufwata ungelipwa fidia au wangepitisha bomba route ingine.

Kwa maelezo yako hilo ni bomba la inch 3 au 4, sasa ukijenga juu yake alafu likapata hitilafu huoni nyumba yako itaweza pata shida pia?...
Duuhh!Sasa bosi nini kifanyike maana jamaa aliyemuuzia kisha kunja mkwanja sh.10,000000!Hataki kusikia chochote anadai yeye hilo shamba aliachiwa na baba yake na hana taarifa ya uwepo wa hilo bomba.
 
Eti kaka mnashauri nini kifanyike?Jamaa anafikiria ajenge hivyo hivyo maana jirani yake amefumba macho na kujenga juu yake
Hoja ya msingi ni nani kamfwata mwenzake? Je ni bomba au mnunuaji kiwanja, jibu ni mnunuaji kiwanja.

Unaweza jitoa ufahamu ukajenga ila siku ikitokea shida jua kabisa sio tu utabomoa nyumba ila utalipa fidia kwa kuharibu mali ya serikali.

Nimekupa mfano mrahisi hapo juu, je ukijenga juu ya bomba alafu bomba likavuja unadhani nyumba itakua kwenye hali gani? Haitapata ufa?

Sishauri ujenge juu ya bomba maana utaleta madhara kwenye bomba. Na kwa sababu umesema ni bomba kubwa jua ukijenga juu yake unahatarisha maisha yako na wote watakao ishi ndani ya hiyo nyumba.

Pia kwa sababu wewe ndiye umefwata bomba jua kisheria umekalia kuti kavu siku likivunjika jua utakua kwenye wakati mgumu..
 
Inategemea na kiwanja kimekaajae kama kimepimwa ni rahisi kwako maana ni rahisi kufanya divation
 
Back
Top Bottom