Naombeni ushauri wenu juu ya mtu mwenye matatizo ya masikio anaweza kufanya shughuli ipi ikiwa ana mtaji wa fedha ?

Kama yuko dsm kwa mtaji wa 20 anaweza fungua duka la vifaa vya ujenzi maeneo ya kigamboni(ujenzi unaendea sana), Goba au Kinyerezi.
Kama ni Dodoma anaweza kufungua sehemu ya kuuza tofali maeneo ambayo ndio yanajengeka sasa hivi.
 
Habari zenu, awali leo niliweka maana >> hii << juu ya ndugu yangu ambae ana chang moto za kusikia.

Kwa ufupi ni kwamba alizaliwa fresh ila akapata homa akiwa na miaka 9, alipigwa sindano ya kwinini kwa dozi iliyozidi matokeo yake taratibu akaanza kupoteza usikivu mpaka imekuwa ni tatizo kabisa kusikia.

Kwao naweza tu kusema pesa si haba zipo, kila siku hupewa 30 hadi 40, hivyo kwa mwezi ni kama milioni, si jambo la kushangaza kwa hali waliyonayo lakini kwa sasa naona nae kapata shauku ya kutaka kutafuta chake, anataka pesa ya kuipambania yeye .

Nipo nae karibu na hata kwenye simu huwa tunachat sana, kaniomba nimpe ushauri wa biashara ya kufungua, Yeye kanipa wazo kwamba biashara isiwe ya kuhitaji kulazimu mazungumzo sana kwa watu wengi, mimi nimepata wazo la biashara ya gym inayoendana na anachotaka ila nimeona tuunganishe mawazo tumsaidie kwa mawazo ya biashara za ziada,

Kwake mtaji wa fedha anaoweza kupewa ni milioni 20.

Mimi binafsi nimekuja kwenu wadau mnisaidie maana nae dogo naona kashafika umri flani anatamani maisha yake, mwanaume anaweza kuwa na changamoto lakini bado ana malengo yake

Miaka: 22

Jinsia: Mwanaume

Elimu: Form 4 alifaulu kwa division 2 alichaguliwa kombi ya science ila aliishia hapo kwa sababu yeye na wazazi waliona kwamba mfumo wa elimu nchi hii kwake utamshinda katika upande wa ufundihaji, jamii (walimu + wanafunzi), na pia waliona hata wenye shida hio waliofika vyuoni wanapata changamoto kupata ajira baada ya kuhitimu.
Aisee pole yake Allah ampe nguvu ya kushinda mitihani hiyo,
Ni kweli mfumo wa elimu kwa Sasa ni kama haukidhi matarajio ya wengi yes Kuna muda unahisi unapoteza Muda ila Kuna vipengele vichache unaviona kabisa Kuna utafauti wa aliyesoma na ambae hakusoma

Biashara : kama ni mzaliwa wa mjini anaweza kufungua barber shop kwa kuwa uwezo upo anaweza akaweka watu gym pia si mbaya muda mwingine Huwa tunashauri mtu kufanya biashara flani kutokana na ;-

1) Hobbies - mtu kama hobby yake ni mazoezi akifungua gym ni rahisi kwake, kama hobby yake movies anafungua library kwake ni rahisi
2) uzoefu: kama ana uzoefu wa kitu kinachoendana na Hali yake basi afanye hivyo mf ana uzoefu wa ufundi wa welding itakuwa rahisi kwasababu anazijua changamoto zake.
3) Elimu - hapa kwa elimu ya form4 naona atakuwa hayuko kokote
 
...Bucha la Kuuza Samaki, Mzigo anafata anauona ubora wake... ukiweka kwenye mzani bei inajiandika hatokuwa na haja sana na sauti madam anajua kusoma na kuandika, Meseji zitatumika katika mawasiliano hasa ya bei pia kupitia groups mbali mbali atajua vingi zaidi. Muambie apitie Forum za biashara kwenye mitandao ya kijamii duniani kuna kitu atapata kitamsaidia katika kujua nini afanye kulingana na hali yake, Anaweza kujifunza kunyoa akafungua Salon Berbershop nzuri sababu Management yake haitakuwa ngumu sana(Atatumia myindo unaitwa MBWA-Management By Walking Arround) akiwa na wafanyakazi zaidi pia anafunga Camera ana-link na simu kwa kipindi asichokuwepo ana-pata taarifa ya kinachoendelea bila kuambiwa.
 
Habari zenu, awali leo niliweka maana >> hii << juu ya ndugu yangu ambae ana chang moto za kusikia.

Kwa ufupi ni kwamba alizaliwa fresh ila akapata homa akiwa na miaka 9, alipigwa sindano ya kwinini kwa dozi iliyozidi matokeo yake taratibu akaanza kupoteza usikivu mpaka imekuwa ni tatizo kabisa kusikia.

Kwao naweza tu kusema pesa si haba zipo, kila siku hupewa 30 hadi 40, hivyo kwa mwezi ni kama milioni, si jambo la kushangaza kwa hali waliyonayo lakini kwa sasa naona nae kapata shauku ya kutaka kutafuta chake, anataka pesa ya kuipambania yeye .

Nipo nae karibu na hata kwenye simu huwa tunachat sana, kaniomba nimpe ushauri wa biashara ya kufungua, Yeye kanipa wazo kwamba biashara isiwe ya kuhitaji kulazimu mazungumzo sana kwa watu wengi, mimi nimepata wazo la biashara ya gym inayoendana na anachotaka ila nimeona tuunganishe mawazo tumsaidie kwa mawazo ya biashara za ziada,

Kwake mtaji wa fedha anaoweza kupewa ni milioni 20.

Mimi binafsi nimekuja kwenu wadau mnisaidie maana nae dogo naona kashafika umri flani anatamani maisha yake, mwanaume anaweza kuwa na changamoto lakini bado ana malengo yake

Miaka: 22

Jinsia: Mwanaume

Elimu: Form 4 alifaulu kwa division 2 alichaguliwa kombi ya science ila aliishia hapo kwa sababu yeye na wazazi waliona kwamba mfumo wa elimu nchi hii kwake utamshinda katika upande wa ufundihaji, jamii (walimu + wanafunzi), na pia waliona hata wenye shida hio waliofika vyuoni wanapata changamoto kupata ajira baada ya kuhitimu.
Bro kama wana uwezo huo si wangemnunulia vile tumashine tudogo twa masikioni twakumwezesha kusikia. Mi nilimnunulia Mzee wangu na mpaka leo mwaka wa kumi yuko poa. Au sikio limekufaje. Ufafanuz plz.
 
havimsaidii,
 
Kwa hy pesa anunue bajaj au boda atoe mikatab au awe anachukua Chak kila siku .. pia anaweza akafungua duka la kuuza gesi hz oryx ,mihan ,lakin pia anaweza akawa mfanya forex hainaga maneno hy
 
unaweza pitia hii post yangu
 
Back
Top Bottom