Naombeni ushauri wenu kwenye hili tafadhali.....

Usiache kabisa unaharibu mila kwetu wachaga ....jitahidi uicontrol pombe isikucontrol nashukuru hujataja uraibu wa uterezi hii ndio case study ya dunia
 
19 yrs old bado kijana mdogo??
 
Halafu mnanyegeshana na kuambiana upuuzi. Wazee tujitafakari.. Ngoja nihamie majukwaa ya maana labda nitakutana na Wazee wenzangu
Hahahaha!. Nimecheka sana.

Baadae unapanga kukutana naye, unamuona yule pale. Aibu na masikitiko kwa pamoja zinakuganda.

Hahahaha! Bora sisi wanaume, angalau!.
 
Kuna kila dalili hii ni chai lakini kama NI kweli basi tatizo kubwa ni hapa.
"Kwa muda mrefu sasa, marafiki zangu nawaona wanachukulia hii ishu kawaida sana..... Tukiwa kwenye mitoko, hawawezi acha kulewa ovyo, kuvuta bangi na shisha, na ku-vape. Kwa mtazamo wao, ni kitu cha kawaida sana, na wanaona kama hakuna madhara yoyote yanaweza kutokea. Wanasema 'wanakula ujana', 'wanamwagilia moyo'..."
Badilisha marafik ulionao kwano peer pressure Kwa makundi ya vijana ni Jambo ambalo ni vigumu kuliepuka.
Fata haki haijalishi Nani atakuonaje kwani kipindi unaangamia utakuwa mwenyw na wao watabaki wakikucheka .
Mwisho kabisa wewe ndiye utakae chagua destiny yako na wala si mzazi wako wala Nani yako kikubwa ni kutengeneza kesho yako iliyobora Kwa kupambana Leo.
Na hauwezi kuipambania kesho yako kama Leo yako ni
  • Kunywa pombe
  • Kuvuta bangi
  • Shisha
  • Kula mirungi
  • Uzinzi
  • Kuvuta shisha
  • Na starehe nyingine zinazofanania na hizo.
 
1. Simamia unacho amini.

2. Marafiki, ndugu wanaweza wakawa na msukumo mkubwa sana kwako (peer pressure) lakini tambua it is not worth it in the long run

3. Jivunie kutokunywa pombe sio kwa sababu inamadhara ila sababu ni misingi ya maisha yako unayojiwekea. Kumbuka you have freedom to choose

4. Ukiulizwa kwanini haunywi, jibu lako lisiwe kwa sababu ina madhara ila liwe kwa sababu sioni umuhimu wa kutumia.

5. Neno "nakula ujana" halina uhalisia kumbuka wewe ni kijana na una kesho nyingi. Na katika ujana wako 15-30 ndio umri wa kujiwekea misingi sahihi ya maisha.

Mdogo wangu: Kumbuka STAREHE haziwahi kuisha wa kupitwa na wakati ILA WATU NDIO WANAISHA.

CLUB ZILIKUWEPO TOKEA ENZI KABLA HATA YA TAIFA HILI KUPATA UHURU NA MPAKA LEO ZIPO ILA WATU (VIJANA WA MIAKA HIYO) SASA NI WAZEE WENGINE WAMEPOTEZA RAMANI YA MAISHA
 
miaka 14..... haikuwa club kipindi hicho.... tulikua tukifunga shule tunajichanga tunakodisha sehemu, tunafanya bash... ila pombe,bangi zilikuwepo
 
Usiache kabisa unaharibu mila kwetu wachaga ....jitahidi uicontrol pombe isikucontrol nashukuru hujataja uraibu wa uterezi hii ndio case study ya dunia
-Mnajivunia upumbavu sana.

-Mila kunywa na kulewa?? Nyie ndio pekee duniani mnakunywa?? Hahahaha

- Muone aibu kusambaza ujinga na mambo yasiyo na msingi
 
Achana na hayo makitu kwa sasa. Utafanya baadae sasa hivi utaharibikiwa mchana kweupe
Kweli kabisa maana hataaminika sehem yyte ile atayoenda sasa atakua binadam wa aina gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…