Naombeni ushauri wenu kwenye hili tafadhali.....

Naombeni ushauri wenu kwenye hili tafadhali.....

Kijana shikilia msimamo wako utakuja kujishukuru mbeleni ktk maisha. Epuka kujiingiza ktk pombe bangi shisha na madawa... Wapo watakao kucheka kukuona mshamba ila usijari omba Mungu akusaidie. Pombe sio nzuri imepoteza afya uhai na muelekeo wa maisha ya watu wengi sana... Hakuna mtihani mgumu kama kuishinda pombe kiukweli sio kazi rahisi...
By the way mimi nakunywa pombe ila haijawahi kuni control nakunywa kwa siku maalumu tu, sifati mkumbo, sinywi pombe za kuitwa sehem na marafik, nakunywa pombe maalum sio yoyote ile, sinywi pombe kwasabab zipoza bure ni heri ninywe maji kuliko kufakamia pombe za bure, naenda kunywa pombe sehem za starehe ambapo kuna watu wastaarabu, na nikiamua kulewa nalewa haswaa ila kamwe sigombani sileti vurugu situkani na siokoti malaya... Na hapa ndipo nilipoishinda nguvu mbaya ya pombe, kitu ambacho 80% ya watu hawawez wanajikuta wanakua watumwa wa pombe na marafik mwisho wake ni matumiz mabaya ya pesa na kushindwa kufanya kazi na kuhudumia familia...
Pombe sio mbaya ila ni hatari ukishindwa kuimudu, halafu pombe inaweza kutumika ktk nguvu za giza kuangamiza future ya maisha yako...
 
simple tu, kaa mbali na marafiki wenye tabia ambayo unaona kwako haifai,

 hawa wazee wa Jf wasikufanye ujione mdogo kwakua wao age imekata maana wengi wao hata pesa hawana ila umri wao ni mkubwa,ila kwa umri wako huo ni mzuri kutumia jukwaa la Jf kama kujijenga kimawazo na kimtazamo
 
simple tu, kaa mbali na marafiki wenye tabia ambayounaona kwako haifai,

 hawa wazee wa Jf wasikufanye ujione mdogo kwakua wao age imekata maana wengi wao hata pesa hawana ila umri wao ni mkubwa,ila kwa umri wako huo ni mzuri kutumia jukwaa la Jf kama kijijenga kimawazo na kimtazamo
asante sana bro.....
 
Mimi ni kijana mdogo wa miaka 19. Hivi karibuni nimekua nikipatwa na msukumo mkubwa wa kunywa pombe na kuvuta bangi. Kusema kweli najaribu sana kujizuia, lakini naona kama hizi jitihada zangu hazitozaa matunda.....

Kwa muda mrefu sasa, marafiki zangu nawaona wanachukulia hii ishu kawaida sana..... Tukiwa kwenye mitoko, hawawezi acha kulewa ovyo, kuvuta bangi na shisha, na ku-vape. Kwa mtazamo wao, ni kitu cha kawaida sana, na wanaona kama hakuna madhara yoyote yanaweza kutokea. Wanasema 'wanakula ujana', 'wanamwagilia moyo'.....
Miaka mingi sasa tumekua tukiishi haya maisha.... kwenda maclub weekend na 'kula bata'. Mimi nimekua nikijizuia mno...... nazugazuga chupa moja nainya hata masaa 2-3.....

Unaweza sema niko kwenye makundi mabaya, lakini mimi sioni hivyo.... hawa ni marafiki zangu wa muda mrefu, tumekua tukisaidiana sana, sema hapo kwenye mambo ya starehe ndo tunatofautiana.....

Pia ndugu, ukizingatia kwamba mimi ni mchaga(kote upande wa baba na mama), wanatumia sana haya mazaga na wamekua wakinishawishi sana, na hata wengine kuonyesha dharau.... Nakumbuka kuna siku nilitoka na bamkubwa nikakataa kunywa pombe.... alicheka sana na kunishangaa.....

Najua wengine mnaweza sema hakuna shida yeyote kwenye kutumia kidogo, lakini kama nilivosema..... mimi ni kijana mdogo, bado maisha yangu ni marahisi, nategemea wazazi, hivyo bado nina ndoto za kufanya vitu vikubwa na maisha yangu, hivyo naogopa sana pombe na bangi vitanirudisha nyuma. Nimeona watu wengi wakiharibikiwa kwasababu ya pombe na bangi....

Najua humu JF watu wazima mko wengi, naomba mnishauri..... Kuna namna ya kubalance maisha ya kawaida na hizi starehe?? Au niendelee kukaa navyo mbali.... na ikiwa hivyo, nitumie mbinu gani??
Washa kitu wewe shetani ahepe acha ubwege
 
Una miaka 19 alafu unatuambia ni miaka mingi Sana umeanza kuishi hayo maisha ya kulewa na kuvuta bangi, ko we umeanza kuvuta bangi na kulewa ukiwa na miaka mitano ama????
 
Una miaka 19 alafu unatuambia ni miaka mingi Sana umeanza kuishi hayo maisha ya kulewa na kuvuta bangi, ko we umeanza kuvuta bangi na kulewa ukiwa na miaka mitano ama????
Sijasema natumia hivo vitu, ila mazingira hayo nimeanza kukutana nayo nikiwa 14....
 
Back
Top Bottom