Naombeni ushauri wenu kwenye hili tafadhali.....

Kijana shikilia msimamo wako utakuja kujishukuru mbeleni ktk maisha. Epuka kujiingiza ktk pombe bangi shisha na madawa... Wapo watakao kucheka kukuona mshamba ila usijari omba Mungu akusaidie. Pombe sio nzuri imepoteza afya uhai na muelekeo wa maisha ya watu wengi sana... Hakuna mtihani mgumu kama kuishinda pombe kiukweli sio kazi rahisi...
By the way mimi nakunywa pombe ila haijawahi kuni control nakunywa kwa siku maalumu tu, sifati mkumbo, sinywi pombe za kuitwa sehem na marafik, nakunywa pombe maalum sio yoyote ile, sinywi pombe kwasabab zipoza bure ni heri ninywe maji kuliko kufakamia pombe za bure, naenda kunywa pombe sehem za starehe ambapo kuna watu wastaarabu, na nikiamua kulewa nalewa haswaa ila kamwe sigombani sileti vurugu situkani na siokoti malaya... Na hapa ndipo nilipoishinda nguvu mbaya ya pombe, kitu ambacho 80% ya watu hawawez wanajikuta wanakua watumwa wa pombe na marafik mwisho wake ni matumiz mabaya ya pesa na kushindwa kufanya kazi na kuhudumia familia...
Pombe sio mbaya ila ni hatari ukishindwa kuimudu, halafu pombe inaweza kutumika ktk nguvu za giza kuangamiza future ya maisha yako...
 
simple tu, kaa mbali na marafiki wenye tabia ambayo unaona kwako haifai,

β€Šhawa wazee wa Jf wasikufanye ujione mdogo kwakua wao age imekata maana wengi wao hata pesa hawana ila umri wao ni mkubwa,ila kwa umri wako huo ni mzuri kutumia jukwaa la Jf kama kujijenga kimawazo na kimtazamo
 
asante sana bro.....
 
Washa kitu wewe shetani ahepe acha ubwege
 
Una miaka 19 alafu unatuambia ni miaka mingi Sana umeanza kuishi hayo maisha ya kulewa na kuvuta bangi, ko we umeanza kuvuta bangi na kulewa ukiwa na miaka mitano ama????
 
Una miaka 19 alafu unatuambia ni miaka mingi Sana umeanza kuishi hayo maisha ya kulewa na kuvuta bangi, ko we umeanza kuvuta bangi na kulewa ukiwa na miaka mitano ama????
Sijasema natumia hivo vitu, ila mazingira hayo nimeanza kukutana nayo nikiwa 14....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…