Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Unapokuwa kwenye shughuri yako Futa kichwani mwako hii " nina degree kutika UDSM" hautojihisi aibu.
 
Wewe unadanganya sio graduate. Kama ni graduate kweli then shule haijakusaidia kimawazo na kimtazamo. Sasa wewe huna kitu halafu unapewa msaada halafu unaanza kukosoa basi toka hapo kwa broo ukapambane kupata unachokipenda.
 
Kuna maneno yanadhihirisha kuwa hauko serious.
........na mimi ninunue ata chips na pepsi niji......

......pesa n za kaka ang....

......eti nikauze maji kwenye mataa ya.....

.......amesahau kuwa nina degree.....

Ushauri wangu kwako
Nina miaka 26 tu bado mdogo najivunia
 
Wewe degree ulioipata hajakusaidia utamwambiaje kaka yako issue kama hiyo. Unataka kugombanishe kati ya mke na kaka yako.
Hayo mambo anafanya mtu wa shule ya msingi
Shemeji anakera haendi Nile kwa kaka
 
Wewe unadanganya sio graduate. Kama ni graduate kweli then shule haijakusaidia kimawazo na kimtazamo. Sasa wewe huna kitu halafu unapewa msaada halafu unaanza kukosoa basi toka hapo kwa broo ukapambane kupata unachokipenda.
Kuuza maji siwezi nina degree
 
Habari zenu jamani mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 26 nimemaliza chuo cha Dar es salaam mwaka jana. See saizi nipo apa Dar es salaam Tandika nakaa na kaka angu ndoananipiga jeki nakaa kwake akienda kazini na mke wake wananiachia buku tu la msosi usiku wakirudi shemeji anapika msosi tunaufinya.

Changamoto ilianza majuzi huyu shemeji Ana roho mbaya kweli kumbe kipindi chote kaka angu huwa anampa 2000 ili anipe pesa ya msosi afu yeye anakata ananipa buku, nilikuja kugundua juzi broo aliposema kwa sauti nanukuu.,(hiyo buku mbili utampa dogo ya msosi) nikasema afadhari nitanunua namm Leo chips [emoji489] na Pepsi nijimwayemwaye, Sasa chaajabu shemeji akaja kunipa buku tu hapo tukaanza kugombana sasa akaanza kunifyezuri na kunifedheshesha mbele ya majirani wa kizaramo wavaa vijora, akisema tena kwa sauti ati amenichoka najaza kitambi tu kazi Sina nabweteka Kati pesa nizakaka angu.

Jana ilibidi yote nimwambie broo huku nikiwa na hasira sana kuliko mwanaume aliyemfumania mkewe . Broo akaniambia yote yaishe atanipa mtaji wa kazi.

SASA chaajabu Leo asubuhi naona ameniletea maji ya uhai kama Dazani tano hivi na MO energy kama dazani saba eti anasema nisimame kwenye mataa ya Sudani Temeke nianze kuuza huku nimebeba mimaji kichwani amesahau kuwa mimi nina degee kutoka UDSM chaajabu hajaniachia hata sent mpaka mdaa huu sielewi nakula nini wenyewe wameenda kazini, naombeni ushauri nifanyeje.

Huu utani sasa, kwamba na wewe una degree?????
Kuanzia leo mimi sina degree yoyote. Pathetic
 
Nunua sun google kuubwa vaa na bonge la pama then zama road dear graduate [emoji310]...tatizo chuo boom ulihonga so unaogopa mademu zako wa first Yr watakuona.
 
Ushauri tafadhari
Ushauri wangu nenda kajifunze kuandika, uanze kuandika kama mtu aliyemaliza chuo, baada ya hapo tafuta barakoa kubwa na kapelo Mungu usinione vaa ingia mtaani uza maji unaowaonea aibu hawatakutambua
 
Back
Top Bottom