Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Wewe utakuwa una kijana kamaliza chuo, Sasa unaona anashangaa shangaa na maisha hapo kwako ukaona uje uanzishe uzi huku, lakini kusema kweli vijana wahitimu wa vyuo mbalimbali hususani ktk karne hii ya 21, tupo na changamoto nyingi sana kwa sababu mbalimbali ikiwemo mfumo wa elimu, mabadiliko ya sayansi na teknolojia, mifumo ya maisha ya kileo nk.

Moja,Unajikuta upo na material mengi kichwani uliyoyasoma, lakini hayana uhusiano wa moja kwa moja na mahitaji ya mtaani huku.

Pili, unaweza kuwa na idea nzuri tu inayohitaji reasonable capital, lakini kukosa mtaji huu kunakufanya uanzie chini kabisa huko ambapo Kama huna moyo wa uvumilivu waweza feli.

Tatu, tunapokuwa vyuoni huwa tunasahau kudumisha mtaji mahusiano na wale ambao hawakupata fursa ya kuendelea na masomo ambao pindi tunapomaliza ndo wana ABCs nzuri za mtaani, hii nayo ni changamoto.

Mwisho, kwa wale ambao bado mpo vyuoni hakikisheni mnakuwa na mpango mkakati wa Nini utafanya baada ya kumaliza masomo yako, usiishie kuwa na mpango tu bali utafutie uzoefu huo mpango unapopata muda Kama weekend, likizo na siyo unapopata muda kuishia kuangalia movie na mambo mengine yasiyo ya msingi muda wote.
 
Asante nimeipata umeupiga mwingi
 
Ndo ushapigika na hiyo ni sign kua hao wenyeji wako wamekuchoka so ni kujiongeza kama unaona huwezi kuuza maji kua unatoka ukatafute chchte hata kazi viwandani huku buku 10 kwa siku hakuna anaekuona huko utatengeneza connection ya watu utapata kitu kingine hvyo hvyo unajibana unapanga kachumba kako cha msingi fanya uwezalo utoke hapo hata kama ni mimi ningeshakutimua
 
Sikiliza kijana. Nenda kafanye kazi. Hujaandikwa chapa usoni. Tena yakiisha ingia hapo afiya chukua mengine. Pia kama hapo home iko friji funga kandoro peleka shule ya msingi au stendi hapo tandika unaweza ingiza zaidi ya 10,000 kwa siku. Ukitoa elfu mbili ya umeme kwa siku na elfu moja ya vifuko. Na buko ya chakula Elfu saba faida kwa siku.
 
Habari zenu jamani mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 26 nimemaliza chuo cha Dar es salaam mwaka jana. See saizi nipo apa Dar es salaam Tandika nakaa na kaka angu ndoananipiga jeki nakaa kwake akienda kazini na mke wake wananiachia buku tu la msosi usiku wakirudi shemeji anapika msosi tunaufinya.

Changamoto ilianza majuzi huyu shemeji Ana roho mbaya kweli kumbe kipindi chote kaka angu huwa anampa 2000 ili anipe pesa ya msosi afu yeye anakata ananipa buku, nilikuja kugundua juzi broo aliposema kwa sauti nanukuu.,(hiyo buku mbili utampa dogo ya msosi) nikasema afadhari nitanunua namm Leo chips [emoji489] na Pepsi nijimwayemwaye, Sasa chaajabu shemeji akaja kunipa buku tu hapo tukaanza kugombana sasa akaanza kunifyezuri na kunifedheshesha mbele ya majirani wa kizaramo wavaa vijora, akisema tena kwa sauti ati amenichoka najaza kitambi tu kazi Sina nabweteka Kati pesa nizakaka angu.

Jana ilibidi yote nimwambie broo huku nikiwa na hasira sana kuliko mwanaume aliyemfumania mkewe . Broo akaniambia yote yaishe atanipa mtaji wa kazi.

SASA chaajabu Leo asubuhi naona ameniletea maji ya uhai kama Dazani tano hivi na MO energy kama dazani saba eti anasema nisimame kwenye mataa ya Sudani Temeke nianze kuuza huku nimebeba mimaji kichwani amesahau kuwa mimi nina degee kutoka UDSM chaajabu hajaniachia hata sent mpaka mdaa huu sielewi nakula nini wenyewe wameenda kazini, naombeni ushauri nifanyeje.

Pambana usione aibu angalia wewe utanufaika nini sio hao unao waogopa
 
Mkuu kauze maji acha ubishoo tena kuna watu wana phd zao na wanafanya hiyo shughuli

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hii chai sasa jamani huyo wa PhD anaeuza maji yupo mtaa gani
 
"Some times we need to put academic qualifications aside and husle like a school drop out because your degree doesn't pay bills"

Mkuu hata Mimi ni graduate lakini sichagui kazi nishapiga saidia fundi,kuuza duka kwa kujitolea mshahara hamna ni msosi tu.Sasa mkuu kwenye utafutaji wa pesa hakuna aibu utaendelea kuomba mpaka lini mzee.

Labda nikushauri nenda mkoa ambao hufahamiki then piga kazi... kumbuka "Mwanaume akiwa na pesa ni sawa sawa na demu kuwa mzuri".

Pia last but not least ukipata mtaji usisahau kubeti kwa akili nyingi ndo njia ngumu na rahisi kutoboa kwa graduates...
 
Back
Top Bottom