Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Ushauri wangu nenda kajifunze kuandika, uanze kuandika kama mtu aliyemaliza chuo, baada ya hapo tafuta barakoa kubwa na kapelo Mungu usinione vaa ingia mtaani uza maji unaowaonea aibu hawatakutambua
Sijawahi wala sijazoea kufanya kazi kwenye jua kali nina matatizo ya kichwa kuuma na macho pia
 
Habari zenu jamani mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 26 nimemaliza chuo cha Dar es salaam mwaka jana. See saizi nipo apa Dar es salaam Tandika nakaa na kaka angu ndoananipiga jeki nakaa kwake akienda kazini na mke wake wananiachia buku tu la msosi usiku wakirudi shemeji anapika msosi tunaufinya.

Changamoto ilianza majuzi huyu shemeji Ana roho mbaya kweli kumbe kipindi chote kaka angu huwa anampa 2000 ili anipe pesa ya msosi afu yeye anakata ananipa buku, nilikuja kugundua juzi broo aliposema kwa sauti nanukuu.,(hiyo buku mbili utampa dogo ya msosi) nikasema afadhari nitanunua namm Leo chips [emoji489] na Pepsi nijimwayemwaye, Sasa chaajabu shemeji akaja kunipa buku tu hapo tukaanza kugombana sasa akaanza kunifyezuri na kunifedheshesha mbele ya majirani wa kizaramo wavaa vijora, akisema tena kwa sauti ati amenichoka najaza kitambi tu kazi Sina nabweteka Kati pesa nizakaka angu.

Jana ilibidi yote nimwambie broo huku nikiwa na hasira sana kuliko mwanaume aliyemfumania mkewe . Broo akaniambia yote yaishe atanipa mtaji wa kazi.

SASA chaajabu Leo asubuhi naona ameniletea maji ya uhai kama Dazani tano hivi na MO energy kama dazani saba eti anasema nisimame kwenye mataa ya Sudani Temeke nianze kuuza huku nimebeba mimaji kichwani amesahau kuwa mimi nina degee kutoka UDSM chaajabu hajaniachia hata sent mpaka mdaa huu sielewi nakula nini wenyewe wameenda kazini, naombeni ushauri nifanyeje.

Ukilala njaa huta tuuliza mkuu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kuna mshkaji ana degree ya education,anauza korosho pale maeneo ya Africana ,barabara ya bagamoyo, na maisha yake yanaenda vizuri tu, sikuhamini siku niliyomuona
Yupo jamaa nilitambulishwa na mshikaji wake Wote ni degree holders wa education,mmja ni fundi mbao na mwingine anaosha magari kwa matambala ..

Sasa wewe mwenye aibu endelea kuwa na aibu.
 
Back
Top Bottom