Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Very sad indeed. Hii inaweza kuwa stori ya kutunga lakini ina ujumbe mzito sana.

Mhitimu wa chuo kikuu anauza maji barabarani, jambo la ajabu sana.

Na wengine wanakudhihaki humu na kushangilia kwamba wacha likome na madigrii yake!

Tumekuwa na jamii ya ajabu sana ambayo inaona ni jambo la kawaida muhitimu wa chuo kikuu kuwa muuza makopo!?
 
hivi elimu ya sasa hivi kweli inawajenga vijana wetu au inawapoteza kabisa,kwa akila yako ya chuo unaona uwezi kuuza maji,sasa wewe endelea kujiona una degree na utabaki kula iyo degree uliyonayo,sasa hivi usomi ili upate kazi unasoma ili upanue ubongo ebu weka degree pembeni na ikiwezekana hata hivyo vyeti kusanya fungia kabatini,chukua hayo maji na hizo energy anza kuuza bila aibu,hao unaowaonea aibu ni watu kama wewe ukiwa masikini watakusema pia ukiwa tajiri watakusema tu ni bora usemwe ukiwa una pesa,maana wengine wataona ni jealous tu kwa kuwa umepata.komaa kama miezi sita weka kila siku angalau 2000 na zaidi baada ya miezi6 utakuwa na kama 300000 hivi,baada ya miezi sita anza kuuza mishikaki huko huko ulipokuwa unauza hayo maji maana unajulikana nakuhakikishia baada ya mwaka utakuja hapo kutushukuru
Kazi ya juani sijawahi fanya afu macho yangu kwenye jua yanauma sana
 
Political science and public administration
Daaah mzee ulifanya field?
Rudi hapo uombe internship

Mm nakuelewa,mm mwenyewe mwaka juzi nilikua nauza nguo k/koo elimu yangu ilinifanya niskie aibu ila baadae nikazoea nilipiga kaz kama miezi 6 hadi nikapata internship mahali
Kaza buti mkuu,you have to walk smart walk fast
Miaka 26 sio kijana mdogo,angalie wenzetu wa ulaya mwenye miaka iyo amesha vuka challenge za namna iyo

Huu ni wakati wa miradi mingi kufunguliwa kwenye NGOs so chakalika mkuu

Tengeneza CV zako weka kwenye bag ukimuuzia mtu maji kwenye private car mpe na cv yako,Mungu ni mwema sana.

#hatammbadojobless ila nimevuka hatua hiyo.
 
Pole Kwa uliyopitia ndugu Yangu lakini ifike mahali usimame sasa Kama mwanaume Anza kuishi Maisha yako futa kitu kinaitwa aibu ,piga goti muombe Mungu wako endelea kupiga hio mishe huenda ukakutana na mishe nyingine huko barabarani kuliko kushinda home , endelea kupiga hio mishe hata Kama hujazoea jichanganye na wenzio wanaofanya hio kazi utazoea Tu lakini pia elimu Yao usiiache ipite bila kukulipa wakati ukifanya kazi yako endelea kuomba kazi sehemu zingine bila kuchoka , kingine kuwa na nidhamu ya hela ndg Yangu Naamini Mungu atakusaidia Tu Kaka
Asante sana mkuu mungu akubariki
 
aibu gani !
kwani unamuangalia nani kwenye maisha yako?
kama aibu kwa kuona watu watakuchukuliaje basi hata kazi yoyote uwezi fanya.

tafuta historia za watu wametokea wapi !
ndio utajiona kuwa kilaza UDSM kwenye maisha ambapo elimu uliyonayo akufungui akili yako.
Kama huko Kuna kazi nzuri nishtue mkuu
 
Very sad indeed. Hii inaweza kuwa stori ya kutunga lakini ina ujumbe mzito sana.

Mhitimu wa chuo kikuu anauza maji barabarani, jambo la ajabu sana.

Na wengine wanakudhihaki humu na kushangilia kwamba wacha likome na madigrii yake!

Tumekuwa na jamii ya ajabu sana ambayo inaona ni jambo la kawaida muhitimu wa chuo kikuu kuwa muuza makopo!?
elimu yake inamsaidia nini,nyie ndo wale wazee mtaani tunaopewaga story huyu mzee kasoma sana ila anakunywa gongoo tu sasa hivi
 
Back
Top Bottom