Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Habari zenu jamani mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 26 nimemaliza chuo cha Dar es salaam mwaka jana. See saizi nipo apa Dar es salaam Tandika nakaa na kaka angu ndoananipiga jeki nakaa kwake akienda kazini na mke wake wananiachia buku tu la msosi usiku wakirudi shemeji anapika msosi tunaufinya.
Umesoma course gani mkuu?
Tuanze na hapa
 
Aibu gani!
kwani unamuangalia nani kwenye maisha yako?

Kama aibu kwa kuona watu watakuchukuliaje basi hata kazi yoyote huwezi fanya.

Tafuta historia za watu wametokea wapi!

Ndio utajiona kuwa kilaza UDSM kwenye maisha ambapo elimu uliyonayo akufungui akili yako.
 
Pole Kwa uliyopitia ndugu Yangu lakini ifike mahali usimame sasa Kama mwanaume. Anza kuishi Maisha yako futa kitu kinaitwa aibu, piga goti muombe Mungu wako endelea kupiga hio mishe huenda ukakutana na mishe nyingine huko barabarani kuliko kushinda home, endelea kupiga hio mishe hata Kama hujazoea jichanganye na wenzio wanaofanya hio kazi utazoea Tu lakini pia elimu Yao usiiache ipite bila kukulipa wakati ukifanya kazi yako endelea kuomba kazi sehemu zingine bila kuchoka, kingine kuwa na nidhamu ya hela ndg Yangu Naamini Mungu atakusaidia Tu Kaka
 
Habari zenu jamani mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 26 nimemaliza chuo cha Dar es salaam mwaka jana. See saizi nipo apa Dar es salaam Tandika nakaa na kaka angu ndoananipiga jeki nakaa kwake akienda kazini na mke wake wananiachia buku tu la msosi usiku wakirudi shemeji anapika msosi tunaufinya.
Hivi elimu ya sasa hivi kweli inawajenga vijana wetu au inawapoteza kabisa,kwa akila yako ya chuo unaona uwezi kuuza maji,sasa wewe endelea kujiona una degree na utabaki kula iyo degree uliyonayo,sasa hivi usomi ili upate kazi unasoma ili upanue ubongo ebu weka degree pembeni na ikiwezekana hata hivyo vyeti kusanya fungia kabatini, chukua hayo maji na hizo energy anza kuuza bila aibu,hao unaowaonea aibu ni watu kama wewe ukiwa masikini watakusema pia ukiwa tajiri watakusema tu ni bora usemwe ukiwa una pesa,maana wengine wataona ni jealous tu kwa kuwa umepata.komaa kama miezi sita weka kila siku angalau 2000 na zaidi baada ya miezi6 utakuwa na kama 300000 hivi,baada ya miezi sita anza kuuza mishikaki huko huko ulipokuwa unauza hayo maji maana unajulikana nakuhakikishia baada ya mwaka utakuja hapo kutushukuru
 
Back
Top Bottom