Naona Bunge linapiga chafya

Naona Bunge linapiga chafya

H
Kwa kweli pasipo kupoteza muda, ninayo furaha ya dhati toka moyoni kwa hiki ambacho nimekiona kwa bunge la leo!

Yaani ni kama mgonjwa mahututi ambaye ghafla ameanza kupiga chafya!

Chafya ni dalili ya uhai.

Hongereni sana wabunge wote mliohusika kukemea vibaka walioko kwenye wizara mbalimbali ambao kazi yao ni kuiba na kuiba na kuiba tena!

Rais Samia Suluhu Hassan aliwaambia wajitathmini, lakini hadi sasa hatujaona mtendaji yeyote serikalini akijihudhuru au hata kuomba radhi tu kwa kile kilichotokea!

Wabunge naomba msiishie tu kutufurahisha wananchi wenu kwa maneno mazito mazito mnayoyasema huko, bali hakikisheni wahalifu wote wanachukuliwa hatua ili kuinusuru nchi yetu na hawa mchwa wanaokula kila kitu hadi vyuma wao wanakula tu!
HILI NALO MKALIANGALIE
 
Wabunge nao akili hamna na nitawashangaa sana kama hawatakuja na maazimio miongoni mwayo ni kubadili Baadhi ya sheria za adhabu na Kuzuia.

-Serikali kuanzia mwaka Jana wamempa Mkaguzi wa ndani fungu lake ,Sasa isiishie hapo ripoti yake isiishie kwenye management ambako Huwa wanamuhonga na kuomba aondoe Baadhi ya hoja kuhalalisha wizi ambapo mwisho wa siku CAG anakuja kubainisha.

Ripoti ya Internal Auditor iende kwenye Sekretarieti za Mkoa Ili Ofisi ya RC ndio ishughulike na wahusika.

Pili Serikali iwaongezee salary na posho Watumishi wa ngazi ya Halmashauri na Wilayani.Tunajua pesa Huwa haitoshi lakini Wana vimishahara vidogo na hivyo kuingia kwenye ushawishi wa upigaji.

-Sheria ya Rushwa nk iwe na kipengele Cha kufilisi Ili kufidia hasara zilizotokea,kumfunga mtu harafu anakula Bure jela sio sawa.

-Wakurugenzi na maofisa wa Juu wa Halmashauri(Wakuu wote wa Idara) waombe kazi na ziwe za Mikataba.Maofisa wa chini ndio wawe na permanent terms.

-Mwisho ni Aisha tufute ofisi ya DC au ipewe Nguvu na iwezeshwe kusimamia Halmashauri kuliko saiizi hawana hata Mafungi Wala Wataalamu ila ni kama omba omba Sasa huyu atasimamiaje Halmashauri zinazotekeleza miradi na kukusanya mapato?

-Takukuru kazi Yao ni ipi ikiwa yote haya yanatokea? Ofisi ya DSO inafanya kazi zipi ikiwa haya yanatokea?
 
Walishaambiwa wajipatie maokoto kulingana na urefu wa kamba zao
View attachment 2803075
Nyie ndio mnapotosha Kauli ya Rais,sijaelewa Huwa mnatafsiri mnavyotaka au mnatafsiri Kwa mantiki yenyewe ya Kauli?

Kwamba wewe Ile methali ya mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake unailewaje? Kimsingi Rais Yuko sahihi Kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake ukikata kamba au kuvuka mipaka ndio unakuwa mwizi Kwa kuingia sehemu isiyokuhusu.

Nasisitiza Kila mtu akila.kulingana na urefu wa kamba yake wizi utatoka wapi?
 
Kila mtu anajua CCM yote ni mijizi. Hapo yameambizana kukemeana.huo ni ukoo wa panya book
 
Nyie ndio mnapotosha Kauli ya Rais,sijaelewa Huwa mnatafsiri mnavyotaka au mnatafsiri Kwa mantiki yenyewe ya Kauli?

Kwamba wewe Ile methali ya mbuzi ale kulingana na urefu wa kamba yake unailewaje? Kimsingi Rais Yuko sahihi Kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba yake ukikata kamba au kuvuka mipaka ndio unakuwa mwizi Kwa kuingia sehemu isiyokuhusu.

Nasisitiza Kila mtu akila.kulingana na urefu wa kamba yake wizi utatoka wapi?
Hili nalo inabidi TUKALITIZAME.
 
Kama kweli wako serious basi tuone hatua zikichukuliwa dhidi ya hao majizi. Otherwise ni maigizo yale yale tuliyozoea.
 
Kwa leo angalau wabunge wa sisiyemu wameonesha uhai wao kwa kuikemea mijizi iliyo serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa ambayo imetafuna mabilioni ya fedha za wavuja jasho pasipo aibu.Hebu nendeni mbele zaidi kwa kuishauri serikali liwe jua au mvua hao wezi waende wakanyoe
Watatulia baada ya muda...
 
Ukifuatilia siyo wana wa system walioamsha hiyo kitu..Wazee wa mifumo wao huwa ni kimya na kupiga meza kimya kimya
 
Kwa kweli pasipo kupoteza muda, ninayo furaha ya dhati toka moyoni kwa hiki ambacho nimekiona kwa bunge la leo!

Yaani ni kama mgonjwa mahututi ambaye ghafla ameanza kupiga chafya!

Chafya ni dalili ya uhai.

Hongereni sana wabunge wote mliohusika kukemea vibaka walioko kwenye wizara mbalimbali ambao kazi yao ni kuiba na kuiba na kuiba tena!

Rais Samia Suluhu Hassan aliwaambia wajitathmini, lakini hadi sasa hatujaona mtendaji yeyote serikalini akijihudhuru au hata kuomba radhi tu kwa kile kilichotokea!

Wabunge naomba msiishie tu kutufurahisha wananchi wenu kwa maneno mazito mazito mnayoyasema huko, bali hakikisheni wahalifu wote wanachukuliwa hatua ili kuinusuru nchi yetu na hawa mchwa wanaokula kila kitu hadi vyuma wao wanakula tu!
CCM Lao moja tu, mwizi huwa hakemewi, mwizi, anauliwa, anafungwa, anafukuzwa kazi, tatizo la nchi hii, hili tabaka tawala, kuanzia ikulu(raisi), wizarani, halmashauri, local government, kote huko ni wezi watupu!
Hakuna wa kumkamata mwingine,
 
Mimi binafsi hao wabunge hawajanifurahisha Kwa sababu Wanalalamika badala ya kuchukua hatua na namna ya kuchukua hatua ni kuja na maazimia makali na wamueleze Waziri Mkuu kwamba kama Serikali haitatekeleza maazimio wasipitishe Bajeti ijayo Kwa sababu huu ni ujinga.

Angalia hapo Tabasamu anasema taarifa 3 za CAG hakuna walichofanya.

Ndio maana Kuna haja ya Wapinzani mana awangesha table Azimio la Kuta target wahusika kabisa ila Hawa wanapiga makelele yasiyo na msingi.

Mbaya zaidi mda wa kujadili hiyo taarifa ni mdogo na umewekwa mwezi wa 11 makusudi Ili Serikali ikatafute majibu ya kufunika Kombe ikiwemo kuhonga Baadhi ya Wabunge.

Mwisho mnufaika mkubwa wa wizi ni ccm na hivyo sitarajii chochote Cha maana sana sana wataitana kwenye Kamatia za Vyama vyao huko.
Leo umeongea kma mwanadamu
 
Back
Top Bottom