Naona Bunge linapiga chafya

Naona Bunge linapiga chafya

Kwa hiyo wamekubaliana ili kumtoa kafara mtu fulani wapate uhalali wa kumweka mtu wao wanayemtaka?! Anyway, kwa ile report ya CAG, hakuna namna serikali nzima ilipaswa kujiudhuru ila kwa sababu tuko kwenye shithole countries, business will be as usual!
Inasemekana namungo fc ni kigingi kinachozuia mtiririko wa asali kuwafikia wazuri hawafi!

Nasikia eti hukatas kusaini Baadhi ya Bajeti za ofisi yake zikiletwa kwa kigezo eti "mnawaibia wananchi"

Konda boy eti ana baraka zote za kulivuruga Baraza Ili asiekua na madhara ashike kwa namungo fc!

Ngoja tuone hatma!
 
Maigizo yale,we ripoti imetoka miezi 6 ishapita leo ndo wanajifanya wana kuumia
 
Inasemekana namungo fc ni kigingi kinachozuia mtiririko wa asali kuwafikia wazuri hawafi!

Nasikia eti hukatas kusaini Baadhi ya Bajeti za ofisi yake zikiletwa kwa kigezo eti "mnawaibia wananchi"

Konda boy eti ana baraka zote za kulivuruga Baraza Ili asiekua na madhara ashike kwa namungo fc!

Ngoja tuone hatma!
Ngoja tuone
 
Kwa kweli pasipo kupoteza muda, ninayo furaha ya dhati toka moyoni kwa hiki ambacho nimekiona kwa bunge la leo!

Yaani ni kama mgonjwa mahututi ambaye ghafla ameanza kupiga chafya!

Chafya ni dalili ya uhai.

Hongereni sana wabunge wote mliohusika kukemea vibaka walioko kwenye wizara mbalimbali ambao kazi yao ni kuiba na kuiba na kuiba tena!

Rais Samia Suluhu Hassan aliwaambia wajitathmini, lakini hadi sasa hatujaona mtendaji yeyote serikalini akijihudhuru au hata kuomba radhi tu kwa kile kilichotokea!

Wabunge naomba msiishie tu kutufurahisha wananchi wenu kwa maneno mazito mazito mnayoyasema huko, bali hakikisheni wahalifu wote wanachukuliwa hatua ili kuinusuru nchi yetu na hawa mchwa wanaokula kila kitu hadi vyuma wao wanakula tu!
Kama unataka maigizo tune Azam 3. Hiyo channel ya Bunge ina waigizaji wa kiwango cha chini Sana.
 
Hilo bunge ni furahisha genge, kama kweli wanajiamini wafanye azimio la bunge kuwatoa baadhi ya mawaziri. Kinyume na hapo ni maigizo kama kawaida.
Naunga mkono hoja
 
Kwa kweli pasipo kupoteza muda, ninayo furaha ya dhati toka moyoni kwa hiki ambacho nimekiona kwa bunge la leo!

Yaani ni kama mgonjwa mahututi ambaye ghafla ameanza kupiga chafya!

Chafya ni dalili ya uhai.

Hongereni sana wabunge wote mliohusika kukemea vibaka walioko kwenye wizara mbalimbali ambao kazi yao ni kuiba na kuiba na kuiba tena!

Rais Samia Suluhu Hassan aliwaambia wajitathmini, lakini hadi sasa hatujaona mtendaji yeyote serikalini akijihudhuru au hata kuomba radhi tu kwa kile kilichotokea!

Wabunge naomba msiishie tu kutufurahisha wananchi wenu kwa maneno mazito mazito mnayoyasema huko, bali hakikisheni wahalifu wote wanachukuliwa hatua ili kuinusuru nchi yetu na hawa mchwa wanaokula kila kitu hadi vyuma wao wanakula tu!
usanii tu hamna kitu hapo. wale wabunge ni wa CCM na serikali ni ya CCM
 
Bunge limetoroka Mortuary
fcc54b51502383.58ef97b7bf467.gif
 
Pia wakati fulani ukiona mgonjwa aliyemahuti, ambaye siku zote mnamlisha chakula na anakula kwa tabu, siku hiyo akidai chakula akala cha kutosha kiasi kwamba hata unayeuguza ukashangaa na kujisikia furaha, angalia sana. Mara nyingi ndio kinakuwa chakula cha mwisho wa uhai wake.
Kwa Bunge hili hizi ni mbwembwe tu, hakuna Bunge hapo.
Bunge linatakiwa litoe azimo. Sio kelele zisizo na tija.
 
Kwa leo angalau wabunge wa sisiyemu wameonesha uhai wao kwa kuikemea mijizi iliyo serikali kuu na mamlaka za serikali za mitaa ambayo imetafuna mabilioni ya fedha za wavuja jasho pasipo aibu.Hebu nendeni mbele zaidi kwa kuishauri serikali liwe jua au mvua hao wezi waende wakanyoe
Waziri Simbachawene anasema tunalaumiwa wizi lakini ndio tuliojenga miundombinu kuliko awamu zilizopita!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi binafsi hao wabunge hawajanifurahisha Kwa sababu Wanalalamika badala ya kuchukua hatua na namna ya kuchukua hatua ni kuja na maazimia makali na wamueleze Waziri Mkuu kwamba kama Serikali haitatekeleza maazimio wasipitishe Bajeti ijayo Kwa sababu huu ni ujinga.

Angalia hapo Tabasamu anasema taarifa 3 za CAG hakuna walichofanya.

Ndio maana Kuna haja ya Wapinzani mana awangesha table Azimio la Kuta target wahusika kabisa ila Hawa wanapiga makelele yasiyo na msingi.

Mbaya zaidi mda wa kujadili hiyo taarifa ni mdogo na umewekwa mwezi wa 11 makusudi Ili Serikali ikatafute majibu ya kufunika Kombe ikiwemo kuhonga Baadhi ya Wabunge.

Mwisho mnufaika mkubwa wa wizi ni ccm na hivyo sitarajii chochote Cha maana sana sana wataitana kwenye Kamatia za Vyama vyao huko.
Wapo waliosema wezi wanyongwe, wengine wakasema wakinyongwa hatujui huko mbinguni watasemehewa, wapewe mashamba walime wajutie wizi! Ni geresha geresha tu huku wakijua wazi wizi wameanza wao kwa kuiba kura, wao wenyewe wezi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hatua nani achukue?
Hivi kweli mbunge anasimama anaongelea wizi wa mabilioni huku akitania tania na wengine kupiga meza na kucheka hapo usitegemee lolote
Hao hao wanaocheka ndio majizi
Kweli majitu yanapata mda wa kucheka
Hivi hayana damu haya
Hata Covid 19 nao wana ujasiri wa kukemea ubadhirifu wa mali kweli,ama ni maigizo tu maana walipo wamekuls pesa kiubadhirifu. mkaguzi yuko wapi. mengine tunayo uvunguni mwetu.
 
Hata Covid 19 nao wana ujasiri wa kukemea ubadhirifu wa mali kweli,ama ni maigizo tu maana walipo wamekuls pesa kiubadhirifu. mkaguzi yuko wapi. mengine tunayo uvunguni mwetu.
Hao wapo hapo kiwizi tu hawana uhalali
 
Back
Top Bottom