Utakufa itapita miaka b 10 hakuna hicho kitu kinachoitwa kiama kitatokea.
Siku hiyo Kutakuwa na makundi mawili, moja likuwa ni kundi la peponi( uzima) hili ndilo kundi litakalofuzu( tumuombe sana Mungu tuwe kwenye kundi hili. Amiin
Kundi la pili litakuwa ni kundi la motoni,
Sifa ya kundi ni
_HALIAMINI UWEPO WA MUNGU,
_HALIAMINI UWEPO WA KIAMA
_HALIAMINI UWEPO WA MOTO WALA PEPO
_HALIAMINI UWEPO WA MALAIKA
_HALIAMINI UWEPO WA VITABU VITAKATIFU VYA MUNGU
WAO HUTUMIA AKILI ZAO TU WANAAMINI AKILI ZAO, WANASAHAU HATA HIZO AKILI WAMEPEWA NA MUNGU
KUNDI HILI LITAPELEKWA MOTONI ,
kabla halijaingizwa kweye moto litasimamishwa na malaika wa motoni kisha wataulizwa kwanza kuwa
"HIVI NYIE HUKO DUNIANI HAMKUAMBIWA HABARI HII YA MOTO WA JAHANAM?"
watajibu tuliambiwa ila tulikaidi tu sisi wenyewe kwa ujinga wetu,
Wataambiwa ingieni sasa muonje huo moto kwa yale mlioyakanusha huko duniani, (Source: QURAAN)
SIFA ZA MOTO WA JEHANAM
Una rangi nyeusi, ueusi wake umepitia hatua tatu,
1. Ulianza kwenye rangi nyekundu
2. Ukaongezwa joto ukawa rangi ya bluu( huu ni kama ule wa gesi)
3.ukaongezwa tena ukawa mweusi,
Ambao huo moto unangoja watu wenye kupuuza maagizo ya Mungu,
Kuni za zake ni mawe, maana kwa joto lake hata jiwe litayeyuka kirahisi tu, na ngozi kila inapoisha inajirudia tena ili kuendelea kuteseka
Moto huu ni moto wa milele, (endless ) FIKIRIA SANA JUU YA HILI EWE MWANADAMU MKAIDI
Umri wa nwanadam ni miaka michache sana ni 60 tu, baada ya hapo nguvu zinakuwa zimeisha na happ kinachofata ni umauti na UTAENDA KUSHUHUDIA LIVE juu ya ujinga unaoukanusha sasa,
Muda sio mrefu utakufa na utaenda kushuhudia mwenyewe,
Usibishe maana haya utayakuta tu HAKUNA SHAKA JUU YA HILI. Ni Suala la Muda tu
NA adhabu itaanza mara tu roho yako itakapo anza kutolewa, pale pale unapokata roho anakuja malaika wa mauti kukutoa roho kwa uchungu hadi mkojo na kinyesi kinatoka kwa wakati mmoja, muda si mrefu utayaona live ukiwa na madhambi hasa kwa wanaokataa kufuata Sheria zake,
Ila kwa aliye amini atakatenda mema roho yake itatolewa taratibu na atakwepana na adhabu kama hizi,
TUMUOMBE MUNGU ATUJAALIE MWISHO MWEMA,
Tusife ila tuwe tume tubu dhambi zetu ili tupate salama kwa Mungu
Amiin