Kama Mungu yupo kwanini atake tuamini yupo , hizi hadithi zako katishie watu walio kata tamaa na wenye hofu ya kitu wasichokijua.
Kwa maelezo yako unathibitisha kuwa Mungu hayupo,
Tumia akili yako tu kutafakari juu ya mbingu zilivyokaa na zilivyo simama, tazama kwa makini muundo wa dunia ulivyo kaa jitafakar,
Angalia tu kwa makini umbo la mwanadam lilivyokaa, mfumo mzima wa mwanadam ulivyo,
Angalia sana suala la uzee na kifo , tafakari kuhusu hilo
Unapata picha kuwa kama yupo aliyeviumba hivi vitu basi atakuwa ni supper power, ukubwa wake haupimiki kwa akili zako, na anaweza kufanya atakavyo kwa muda autakao,
Nilitaka kukufafanua kimaandiko juu ya uwepo wake ila wewe huviamini hata vitabu hivyo,
Angalia tu kuwa mtu akifika miaka 60 nguvu zinamuishia maana yake anarudi kwa aliye muumba, sasa wewe umri wako hata uishi miaka 120 lakini utakufa,
Kabla hujafa jua yafuatayo YATAKUKUTA NA UTAYAONA LIVE
1.atakuja malaika mtoa roho, utamwona live, ukiwa na matendo mema atakuja na ura nzuri na atakutoa roho kwa upole, ukiwa na madhambi na wasio amini uwepo wa Mungu atakuja na umbo la kutisha sana na atakutoa roho kwa ukali mno hadi kinyesi na mkojo vinaweza kukutoka kwa pamoja kwa yale utakayoyaona. ( WAULIZE WATU WA MORTUARY au WANAOOSHA MAITI WANAJUA MAMBO MENGI SANA SEMA NI SIRI TU,
2. UKIFA MOTO UTAUONA LIVE kwa macho yako na utaanza kuchomwa hapo hapo kaburini kabla ya siku ya kufufuliwa , una siku ukifufuliwa utakutana nao tena na huo utakuwa ni moto wa milele, uki2a huna dhambi basi hata kaburini itakuwa ni bata tu
USHAURI KWAKO
Rudi kwenye njia ya Mwenyezi Mungu, soma vitabu vyote vya dini vya KIISLAMU NA kikristo, maswali usiyoyaelewa waulize wajuzi wa dini hiyo uelimishwe.
Ukifanya hayo kuna siku utarudi kuitazama post yako utamshkuru Mungu kwakukutoa ndani ya hilo giza ulilopo kwa sasa, yaani UPO NDANI YA GIZA NENE SANA. na usipofanya jitihada za haraka utashangaa mauti yamekukuta na hujamjua Mungu wa kweli, utakuwa ni mwenye kujuta
NENO NINGEJUA HUA NI MWISHO WA SAFARI