Nimepoteza Marafiki wengi na hata Kushindwana na Mademu wengi kutokana tu na Suala zima la Muda ( Ahadi ) na Kujali Ratiba. Hakuna Kitu ambacho GENTAMYCINE nakipenda na nakiheshimu kama kwenda na muda, kuwa Mtu wa Ahadi na Kujali / Kuheshimu Ratiba. Ukitaka ' nikuchukie ' na ' tugombane ' Wewe niambie Uwongo au nipoteze muda na hapo ndiyo utanijua vizuri na huenda hata ' ukanichukia ' Maisha yako yote.
Kuna Demu Mmoja nakumbuka niliwahi Kupendana nae mno tu na alijua kuwa Mimi ndiyo nitakuja kuwa Mumewe lakini kuna Siku tulikubaliana kukutana muda fulani ( siyo kwenda Kufanya Mapenzi ) na nilifika eneo husika dakika 15 kabla ya muda wetu na Yeye alifika dakika 45 baadae tofauti na muda tuliokubaliana na kilichofuatia pale pale nilimpa ' Makavu ' yangu na kuwambia Mimi na Yeye Safari yetu ndiyo imeishia pale rasmi. Hadi hivi leo haamini Mkuu japo nakiri kuwa alikuwa ni Mwanadada Mmoja Mrembo sana lakini sikuliangalia hilo kwani GENTAMYCINE Kiasili ni Mtu wa ' PRINCIPLES ' na nitakuwa hivyo hadi nazama zangu Shimoni Kaburini pale Mwenyezi Mungu akiniita Siku aliyonipangia.
Na kilichonikasirisha zaidi kwa huyo Demu ni kwamba nakumbuka kabla kabisa ya Kukubaliana nae kuhusu muda wetu wa Kukutana nilimuuliza zaidi ya mara tano kuwa je, ana uhakika huo muda atauweza na atawahi nae kwa Kujiamini kabisa na ' Mikogo ' kibao ( kama mnavyowajua Wanawake wetu / Dada zetu ) akanihakikishia kuwa atawahi lakini hatimaye hakutimiza Ahadi yake na Urafiki wetu ukafiki Kikomo hapo hapo.
Desturi yangu mara zote nikiwa napanga ' appointment ' na Mtu yoyote yule huwa napenda kumpa Yeye nafasi ya Kupanga au Kuchagua muda husika ili ' ajinyonge ' mwenyewe na kama asipoenda na huo muda basi Kazi yangu ya Kumpa ' Makavu 'iwe rahisi na Kumalizana hapo hapo. Kama unajua huna uhakika basi usiniahidi muda wa Kukutana / Kuonana na huwa napenda mno wale Watu ambao hufika mahala dakika 15 au hata 30 kabla ya ule muda wetu tuliokubaliana. au hata kama unaona utachelewa basi nijulishe mapema hapo nitakuheshimu kuliko unanichelewesha halafu hunipi taarifa zozote za sababu ya Kuchelewa Kwako.
Sasa kwa mfano kama Maulid Kitenge na Kituo chake cha Wasafi fm kumbe walijua kuwa kwa leo Jumatatu hii hawatakuwa na Kipindi muda ule aliotuambia tokea Siku ya Alhamisi katika Kurasa zake mbalimbali za Mitandao kwakuwa watakuwa katika Sherehe za Uzinduzi kama ambazo zinaendelea sasa basi hata Jana tu kupitia Kurasa zake zile zile angetuambia au hata Kutuomba Radhi Wasikilizaji wake tofauti na ambavyo amefanya na ndiyo maana hata Mimi nimekuwa ' Mkali ' hivi Kwake / Kwao. Mawasiliano ni jambo zuri na jema sana na kwa hili kidogo ' PR ' ya Wasafi fm ' imenajisiwa ' hasa kama Wewe ukiwa ni Mwana Taaluma ' tukuka ' wa Mawasiliano ya Umma na Uhusiano. Hili Kosa lisijirudie tena tafadhali.