Naona Maulid Kitenge na Wasafi FM ulikohamia rasmi mmeshaanza ‘ kuchemsha ‘ mapema tu

Hiki ninachosikia hapa kama ni kweli, basi watangazaji wa Tanzania wanapanda bei kama wacheza mpira wa ulaya.
Yaani unaambiwa watangazaji wanaletwa kwa helicopter, hizi mbwembe sidhani hata BBC wamewahi kufanya.
 
Nimeshangaa tu Makonda hajaalikwa

Amesajiliwa rasmi na Majizo kuwa Msoma Vichwa vya Habari vya Magazeti katika Kipindi cha Joto la Asubuhi huku Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam akituachia Sisi wana Dar es Salaam wenyewe.
 
saa mbili asubuhi unapata muda wa kusikiliza radio..shughuli zako za kukuingizia kipato unazifanya saa ngapi au huna kazi za kufanya?
Shughul zinatofautiana mzeee. Kuna mwingine ni dalali, mwingine ni mjasiliamal mambo yake anayaamua mwenyewe na kutoa malekezo kwa watu wake.

Mwingine yupo likizo. Kuna sababu nyingin hapa mzee
 
Maelezo meeeengi
 
Hiki ninachosikia hapa kama ni kweli, basi watangazaji wa Tanzania wanapanda bei kama wacheza mpira wa ulaya.
Yaani unaambiwa watangazaji wanaletwa kwa helicopter, hizi mbwembe sidhani hata BBC wamewahi kufanya.

Hiyo ni mbinu nzuri tu ya Kujitambulisha na Kujitangaza zaidi hivyo wala sioni tatizo juu ya hilo. Lakini pia mambo kama haya pia yanaibua mwamko, kuongeza chachu na kuibua Ubunifu zaidi hasa kwa Wanafunzi wa Fani husika ya Habari na Utangazaji na hata kwa Watangazaji wa Vipindi vingine katika Redio zingine.
 
kuna clip moja hivi Kitenge alinifurahisha sana.... alikuwa EFM studio akisoma magazeti mara paap kanyanyua kiti anataka kumtwanga nacho Musiba mtandaoni.
sijui kiti angekiingizaje mtandaoni!!
 
HIVI WACHANGIAJI WA UZI HUU KWELI WANASIKILIZA WASAFI FM??!! LEO SIO SIKU YA KUANZA KIPINDI BALI NI UZINDUZI WA KIPINDI NA WAGENI WAMEANZA KUWASILI PALE MIDA YA SAA MBILI NA KUMEKUWA NA MAHOJIANO YANAYOENDELEA KATI YA WAGENI WANAOWASILI NA WATANGAZAJI WA WASAFI
NI SHEREHE ZA UZINDUZI WA KIPINDI NA SIO KIPINDI KAMILI
 
Mod mpigeni ban huyu .kwani yeye nani anatulisha maneno
 
notisi zote hizi mwamba!!!..jua kufanya muhtasari
 
saa mbili asubuhi unapata muda wa kusikiliza radio..shughuli zako za kukuingizia kipato unazifanya saa ngapi au huna kazi za kufanya?
Mkuu ratiba za watu tofauti what if kama yuko likizo au anaingia shift ya mchana au yuko kwenye gari akisikiliza au anauza duka lake huku akisikiliza.....
 
saa 2 asubuhi badala ya kumpikia chai mumeo awahi kazini unasikiliza redio, utapewa talaka, shauri yako
 

Kwahiyo Kosa ni letu tulioaminishwa tena hadi Kuhakikishiwa kuwa leo Saa 2 asubuhi hadi Saa 5 asubuhi Kipindi kitakuwa hewani na Maulid Kitenge au ni Wahusika wao wenyewe? Na kama walijua kuwa leo hawatakuwa na Kipindi na badala yake watakuwa na ' Uzinduzi ' kwanini pia hawakutuambia mapema kupitia ' njia ' zao zile zile kama walivyokuwa wakituambiwa hapo awali? Hata muwatetee vipi ila kwa hili la leo wametukosea mno Sisi Watu makini wakiongozwa na Mimi GENTAMYCINE.
 
Mod mpigeni ban huyu .kwani yeye nani anatulisha maneno

Bahati nzuri Moderators wa JamiiForums hawana ' Upumbavu ' ulionao na wanajitambua vile vile na huenda ' wamekudharau ' kuliko unavyodhani.

This is GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE a.k.a Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…