Naona si sahihi mtu kuweka plate namba ya Jina lake

Basi kama ni hivyo matajiri wengi ni washamba halafu kajamba nani ndio wenye akili.
Akina MO, VUNJABEI, SANDALAND wote hao wameweka majina.
Kuamini mtu mwenyepesa hawezi kuwa mshamba nao ni ulimbukeni. Nyie ndio mnaamini mtu akishakuwa na pesa basi yuko perfect...
 
Kuweka majina kwenye plate number ni ushamba
 
Ijumaa ya tarehe 16 Mei mwaka 2016 tuliangazia matumizi ya neno limbukeni. Mtaalamu wetu alikuwa Onni Sigalla, mhariri mwandamizi, Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, huko nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anaangazia neno limbukeni ambapo anafafanua limbukeni kama mtu ambaye anapata kitu kwa mara ya kwanza aghalabu kitu chenye thamani na kuonyesha kukiajabia sana. Aidha ni mtu ambaye anafanya kitu kwa mara ya kwanza na kupata shida kwa sababu hana mazoe nacho.
 
Kama unaumia na watu walioamua kutumia fedha zao kujipa furaha basi utakuwa una matatizo mno. Hilo halina tofauti na wewe kuamua kuvaa saa ya gharama, miwani, pete au cheni. Ni nakshi tu na kuikonga nafsi ya anaeamua kufanya hivyo.
 
Kuweka majina kwenye plate number ni ushamba
Sawa!
Kuelewe maana ya ushamba au ulimbukeni...inategema kiwango cha uelewa wako. Kwa sababu tunatofautiana fikra na mitazamo, haiwezekani wote tukawa na definition moja ya ushamba/ulimbukeni.

Kwa mfano: Mimi naweza kusema, ile tabia ya kuning'iniza funguo za gari kiunoni ni ushamba, just bcoz mi sipendi kufanya hivyo, haimaaninshi kwamba ni ushamba.....

Kama wewe hupendi, basi waache wanaopenda na wenye uwezo wao wafanye wapendavyo. NA UWASHESHIM KWA SABABU WEWE HUNA HELA ZA KUFANYA HIVYO
 
Siwezi kumheshimu mshamba.
 
Ni ushambaaaaa
 
Ukiwa huna pesa unakuwa na mawazo ya ajabu ajabu, Tafuta pesa mkuu.
 
Braza umeandika kwa hasira sana. Hebu kwanza piga glass ya maji ya uhai ujipongeze.
Unaanzaje kupangia wanaume wenzio matumizi ya pesa zao?
Unajua ukiwa huna hela….kila mwenye nazo unamuona anazitumia vibaya.
Halafu naona wewe ni mzee mwenzangu umeingia JF kitambo sana.
Kuwa makini uko kwenye umri hatarishi.
 
Pesa nnazo mzee mwenzangu.....ilinibidi nitafute pesa kwanza kabla sijaanza kuongea vitu kama hivi kwenye jamii...

Sijaandika kwa hasira na simpangii mtu matumizi ya pesa. Ila kuandika jina kwenye plate ni ulimbikeni. Ushamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…