Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Habarini wakuu! Ni mimi kijana wenu humu jamiiforums nina miaka 21, kama mnavyojuwa umri huu bado nipo masomoni chuo flani hivi apa dar na bado nipo home.

Sasa tuludi kwenye mada, unajua nini hapa home sipaelewi sikuhizi nimekuwa nikichukiwa pasipo na sababu za msingi, hasa bi mkubwa amekuwa mtu wakunifokea fokea hadi majirani huwa wanasikia jinsi ninavyofokewa. Majuzi kati hapa niliambiwa sikuhizi hapo home sifanyi kazi na ninachelewa kurudi nyumbani, nikiwauliza wazazi wangu ni kazi gani wanataka mimi nizifanye hapa nyumbani naambiwa nioshe vyombo, mara nifyeke majani na mikazi mengine kibao.

Okay siku na kipingamizi kwasababu hawa ni wazazi wangu hivo ni wajibu kuwasikiliza na sio kwamba siku za nyuma nilikuwa sifanyikazi? Hapana ni kutokana na majukumu ya masomo huku chuoni yananibana sana hivo nakuwa mtu sio wakushinda nyumbani maana mda wote na huku chuoni huwa na baki mpaka saa 3 au nne usiku ndio narudi home. Nafanya hivi ili nikimbie majukumu ya nyumbani ila baadae nahisi wazazi wangu walinishukizia.

Anyway sasa kila nikifanya kazi za hapa nyumba bado maneno yanakuwa mengi mara uwambie urudie kuosha vyombo mara mbili wakati apo vyombo ushaosha na vinan'gaa bila shida , ukitoka hapo mara uwambiwe chooni unaachafua mara hausafishi mara unaingiza mchanga mara uwambiwe uliacha mavi leo asubuhi yaani maneno yanakuwa mengi halafu bimkubwa anaongea kwasauti kubwa hadi majirani wanasikia

Mimi hali hii sipendezwi nayo, naona wazazi wangu kama wameanza kunichoka, hapa nafanya mpango mwisho wa mwezi huu nichomoke hapa home najua mwanzo wa kujitegemea huwa mgumu ila potelea mbali siwezi kuendelea kukaa home huku nikidharirishwa na maneno ya bimkubwa.

Anyway natafuta chumba bei iwe 50k maeneo kuanzia ubungo kibo, kona mpaka kimara korogwe. Kama unaona au unasikia kuna chumba kinapangishwa maeneo hayo anipange sasa. Wakuu #natanguliza shukuran
Yani kweny hili swala mdogo angu la kwenda kukaa nje ya nyumbani kwa umri ulonao mim binafsi sikushauri.
Jitahid tu ufanye hivo vikazi hapo nyumbani na chuo pia ufike kwa wakati.
Wazazi wetu mara nyingi wanakua na uchizi huenda kwa sabb ya mambo walosikia kutuhusu.
Vumilia tu mzazi akimbiwi wala huwezi kumkwepa, Hyo pesa fanya kujitunzia tunzia ukimaliza chuo itakusaidia.
 
K

Kumbe una boom... Jiongeze kijana.. kukaa Kwa wazaz Kwa umri huo piah ni changamoto coz utaona Kama unaonewa... Yawezekana bi mkubwa anasema huyu mbna anaboom na anakula nyumbani na vitu vingne... Pia mzazi muda mwingne kwake unabaki mtoto bo matter umefikia wapi
Yaani mzazi achukie mwanae kukaa nyumbani kisa ana boom.

Acheni kumjaza kichwa dogo ionekane maza ake hataki akae hapo.
Mzazi anapenda mwanae apate tabu??
 
Story ni ya kitambo kidogo. Ubaya wa humu, usipokumbuka jina la msimuliaji au title ya huo Uzi, ni ngumu kuupata. Ila Kuna siku utakutana nao tu.

Jamaa anakwambia alikuwa anavizia watu wameingia ndani, pakiwa na Giza giza anapanda zake juu ya mti [emoji28][emoji28]

Tusimulie
 
Atanizingua bimkubwa ni mkorofi hata kaka sidhani kama atamuweza
Mtoto yeyote tena mtu mzima kama hivi wewe mleta mada ambaye anadiriki kabisa tena kwa nuia kuja kushitaki wazazi wake JF au kwenye public yoyote ni mpumbavu. Tena mpumbavu kabisa.
Wazazi waliokuzaa wamekulea toka utotoni bila kuchoka, wewe miaka 21 tayari ushawachoka na kuja kuwasimanga JF. Kweli?!
 
Mi wazazi wangu kitu kidogo tu eti ntakupa laana hasa Maza anapenda sana hii misemo[emoji848][emoji848
😂😂😂 mimi akiniambia hivo asee tena kitu kidogo tu lazima ni react yaani mi n abelieve katika kuongea akiniboa namwambia, akinifurahisha namwambia so at the end we are cool

Ila kunigombeza hajawai labda nikivokua mtoto kwa umri huu waga tunabishana 😃😃😃

Sio utovu wa nidham but mama nae ni binadamu haezi kua sahihi kila saa asa ukimuogopa unaeza kua victim kama mtoa mada, mie namuheshim ila kumuogopa ni hapana
 
Anaweza ongea nae mama atajua wapi anamkwaza mwanae atajirekebisha kama ni mama mzuri
shida ni kwamba sisi vijana wa umri wa kuanzia o-level kueleka hivi mpaka chuo, tunakua na ile kama shauku ya kujitegemea, lazima unakua unamuona mzazi mbaya, kazi za kuosha vyombo, kufagia n.k unachukia, kuna yale maisha una-imagine unatamani ukayaishi mwenyewe sema ndo hivo. kujitegemea sio rahisi....

Ugomvi mdogo ambao miaka ya nyuma ungetokea kati ya we na mzazi saivi hauwezi kuisha haraka unakua mkubwa, unakuta bado unabanwa muda wa kurudi, kunywa pombe na ratiba zingine.... wote tunapitia hili...
 
Ndio naanza sasa kujitafutia heshima hasa kwa wazazi wangu naona nikiendelea kukaa hapa nyumbani zarau zitakuwa nyingi na nataka niwaonyeshe kwamba naweza kuishi bila wao ili heshima iwepo
Pole ila kama Huna Bumu mzee jifanye LOFAAA fanya kazi za nyumbani na wazazi wakiongea usiwajibizeee.. Mtaani sio poaaa hasa kama ukiamua kuondoka kwa hasira bila baraka zao kesho kupiga simu wakusaidie ni Ngumu omba hata ulipiwe hostel tu waambie masomo yanakaba sanaaa ila Usiondoke bila taarifa ukaenda kupanga wakati bado unasomaa na huna chanzo cha kipato unaweza Kuishia pabaya.
 
Mbona atarudi home sio rahisi nimemuambia
Kurudi home apo sahau me nimeshapanga liwalo na liwe kama kupanga chumba ni ngumu basi kwetu hilo ni kawaida coz maisha ya mtaani nayajua A to Z
 
Back
Top Bottom