Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Acha tu hapa naishi na wazazi wangu tena wakunizaa ila naona manyanyaso yamekuwa mengi hapa nyumbani ngoja nichomoke mwisho wa mwezi huu
Wazazi wako wana watoto wangapi na we ni wangapi kwenu?
 
Mkuu hayomaisha kwangu mimi naona kawaida mkuu maana nilishawahi kushindia mkate na maji tena nilishawahi kutembea kwa mguu kutoka home mpaka chuo wiki nzima kipindi hicho boom lilichelewa kutoka nikawa nashida maji na mkate chuoni so kwangu maisha kama mimi nimeshayazoe hivo usinitishie maisha
[emoji16][emoji16][emoji16] hii sentence imenifanya nifurahi sana. Yani ulikuwa unashindia mkate halafu unarudi nyumbani usiku unakuta ugali wa mama unakula unapunguza njaa. Sasa huko unakokwenda ukishindia hivyo mkate, ukirudi usiku room uliyopanga nani atakufadhili hiyo usiku?. Hasira siku zote huwa ni hasara na siku zote wahenga huwa wanasema " kamwe usitoe maamuzi au usifanye jambo ukiwa na furaha sanaaa au ukiwa na hasira sanaaaa". Utapotea.

Hilo boom Hilo boom unalolitegemea peke yake bila kipato kengine litakupoteza. Usiwasikilize wengine wanakupush hapa ooh we nenda hata Mimi nilianza hivyo hivyo Kuna wengine walilipiwa Kodi na wazazi wao, Kuna wengine walisapotiwa na videmu vyao, Kuna wengine walisapotiwa na vijanaume vyao. Sasa wewe shupaza shingo ukiwa na chanzo cha boom alone uje upotee hivi hivi.

Kabla hujatoka hapo home, tumia hekima na kaa tafakari kwa unachofanya je ni sahihi au lah. Vijana mnajulikana mkishafika chuoni basi mnakengeuka na wewe unamuwekea kifua mama Ako kwa kutaka kuwa juu, siku zote mama ni mama tu,haijalishi ana mapungufu ya aina gani. Toka nyumbani kwa mipangilio, sio kwa hasira wala kwa kukurupuka. Sasa wewe shikilia muhemko uende ukateseke huko mtaani kwa kula punje za mihogo.

All in all, nakutakia Kila la kheri katika safari yako uliyoianzisha ya kimaisa.
 
Mkuu em nitag hio story ya aliendoka home kisa boom😂😂😂
Story ni ya kitambo kidogo. Ubaya wa humu, usipokumbuka jina la msimuliaji au title ya huo Uzi, ni ngumu kuupata. Ila Kuna siku utakutana nao tu.

Jamaa anakwambia alikuwa anavizia watu wameingia ndani, pakiwa na Giza giza anapanda zake juu ya mti 😅😅
 
Hamna maza sikuhizi kabadika mpaka mimi namshangaa sijui anataka nini kwangu kama anataka nijitegemee kwanini asinifukuze nijue moja sio kunifokea tena kwa sauti kubwa.
Mzee wako yupo? Ushajaribu kumshirikisha kuhusu hizo kero za bi mkubwa?
 
Dah mimi ndio mkubwa na nina mdogo wangu moja nae ni wakiume ila dogo yupo la pili so me ndio nakuwa house girl na house boy home maana maza washaniifanya niwe hivi ukiwaambia ndugu unaoneka una jeuri kwa wazazi mara umeanza zarau. Basi naamua kukaa nayo moyoni
Yaani we upo chuo mdogo wako la pili?ndio maana unaona hutaki kugombezwa,yaani kifupi hujazoea maisha Hayo gap Kati yako na Dogo ni kubwa sana so inaonyesha uliishi Maisha ya kuendekezwa sana ulipokuwa mwenyewe Kabla Dogo hajazaliwa
 
Sikiliza mdogo wangu,
Mzazi hawezi badilika bila Sababu za msingi,lazima Kuna sehemu utakuwa unamkwaza,kaa tafakari njia zako hapo nyuma na za sasa utajua tatizo Nini!
Kama mzazi anajaribu kukuweka kwenye njia iliyo sahihi,humu utashauriwa mengi,tafadhali yachuje Kabla hujafanya maamuzi.

Haya unakwenda kupanga chumba source of income ya kulipia Kodi na kula,kulipia bili za umeme na maji,vitanda na godoro ,vyombo unazitoa wapi?unafanya kazi?
Sometime unakuta mzazi anapitia menopause au ana matatizo ta kisaikolojia anafanya vitu ambavyo anaona ni sahihi kumbe anafanya sivyo anakuwa hajielewi
 
[emoji38][emoji38] acha tu ndugu Imagine unaambiwa unaacha mavi chooni tena kwa sauti kubwa utajifeel vipi hapo majirani washasikia yaani ni aibu tu maza ananitia mtaanj
Mkuu wewe ni Mwanaume hakuna kurudi nyuma wewe Sepa hapo. Vielelezo vyote hapo vinaonesha Maza ako anataka USePE na ukijifanya kichwa ngumu atakutamkia live kabisaaaa

Unatakiwa uanze kujitegemea sasa usihofie changamoto ndio zinatukuza na kutufanya tuwe Wakubwa. Ila maza yako naye inaonekana education empty set kabisa huwezi kutumia njia ya kukudhalilisha hivyo eti unaacha "mzigo" chooni duh! 🤣🤣
 
Sometime unakuta mzazi anapitia menopause au ana matatizo ta kisaikolojia anafanya vitu ambavyo anaona ni sahihi kumbe anafanya sivyo anakuwa hajielewi
Sasa huyo bwana ni mdogo sana,Kama kashindwa tu kuvumilia kugombezwa na Maza ataweza magombezo ya dunia??Dunia unagombeza nyie sio poa😅😅😅😅
 
Story ni ya kitambo kidogo. Ubaya wa humu, usipokumbuka jina la msimuliaji au title ya huo Uzi, ni ngumu kuupata. Ila Kuna siku utakutana nao tu.

Jamaa anakwambia alikuwa anavizia watu wameingia ndani, pakiwa na Giza giza anapanda zake juu ya mti [emoji28][emoji28]
Nakumbuka ile story HV Ni umughaka ndio kasimuliaa
 
Sasa huyo bwana ni mdogo sana,Kama kashindwa tu kuvumilia kugombezwa na Maza ataweza magombezo ya dunia??Dunia unagombeza nyie sio poa[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Yote kwa yote ila kuishi na mwanamke anaepitia menopause ni mtihani mkubwa sana
 
Njoo geto kwangu tuishi, ila sitakuoa ukimaliza chuo unarudi home kwenu.
 
Pole sana ndugu!!

Kuna brother Ake mshkaji wangu hivi, alitimuliwa kwao kipindi ako na 15 yrs.

Mshkaji kimalezi hapo kwao aseee wameteseka vibaya mnoo na MTU aliyewatesa ni dingi yao kabisa.

Na huyo brother Ake kwa sasa Mungu amemjaalia kajipata ako vyema na biashara zake, jamaa anasema hana hamu na huyo dingi yao.

Jamaa anasema dingi yao hapo NYUMA alikuwa na hela sana sasa akajafilisiwa na ndugu zake kwahiyo madhila ameyarudisha Kwa watoto wake.

Kuna watu wanateseka mnoo Kwa wazazi wao, kama hujawahi pitia hizi mambo asee mshukuru sana Mungu wako Kwa kukupa wazazi wema.

Mo jitahidi asee uondoke Kwa wema hapo home, pia upambane upate ramani za kujishkiza kipindi unasoma Ili life lisikupige chenga za Lionel Messi.

Chukua hiyo changamoto kama chachu ya kufanikiwa kwako kama Christiano Ronaldo, wengi walioteseka makwao Mungu amewabariki sana katika maisha wako vyema sana kama Napaku wa Arusha.
 
Yes yes,haya makwazo yatakujenga na kukufanya imara, kuna njia ya mafanikio unatakiwa upite na hiyo ndio njia sahihi..

Kajitegemee sasa na utafanikiwa,na ukifanikiwa utamshukuru bi mkubwa kwa roporopo zake zimekufanya ufanikiwe..
Kama si hivyo ungebaki tegemezi mpaka kesho.

Kila linalotokea usilaumu hio ni njia ya mafanikio yako.
 
Yes yes,haya makwazo yatakujenga na kukufanya imara, kuna njia ya mafanikio unatakiwa upite na hiyo ndio njia sahihi..

Kajitegemee sasa na utafanikiwa,na ukifanikiwa utamshukuru bi mkubwa kwa roporopo zake zimekufanya ufanikiwe..
Kama si hivyo ungebaki tegemezi mpaka kesho.

Kila linalotokea usilaumu hio ni njia ya mafanikio yako.
Fact
 
Pole sana
Sio rahisi kujitegemea ongea na mama vizuri mwambie shida nin?
Nazania ni wakati sahihi wa yeye kujitegemea sasa,
Ila anatakiwa aondoke nyumbani vizuri,na asikate tamaa kabisa,siku akikwama aweze rudi na wakampokea(asiweke akilini mentality ya kurudi ama kushindwa,ikifika hatua amerudi imebidi na hamna namna tena,ila kwa changamoto ndogo ndogo apambane nazo,anatakiwa awathibitishie wazazi wazo lake la kujitegemea ni sahihi,mana ukirudi tena home na huna kitu hali itakuwa mbaya zaidi ya mwanzo)

Sijui lakin kama ananielewa.
 
Back
Top Bottom