Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Mimi nimeshajitahidi sana kujali mishemishe zangu nakuishi na wazazi wangu ila tabia ya bimkubwa kunifokea kwa sauti kubwa kwakweli nimeshamvumilia vyakutosha sasa ni muda wangu wa kuwa huru na kelele za bimkubwa. Kuhusu umri wangu 21, najua utashangaa kwanini naondoka home ila ndio hivo mkuu kelele za bimkubwa ndio zinanifanya niondoke nyumbani
Mwambie aache kukufokea bhana mfate akiwa amerelax umwambie kwanini unanifokea sana mwambie yoote yaliyopo moyoni
 
Hasira hasara.....Kuna wenzio na hizo boom wanalala na njaa..chumba Cha 50 ni expensive kutegemea boom labda Kama una support ya mzazi

Anyways,kupanga ni kuchagua
Acha tuone itavyokuwa ila kwangu kuondoka nyumba ni muhimu mwisho wa mwezi huu
 
Nimecheka sana unaposema eti umemvumilia sana. 😅😅😅

Mpaka umri huo, nani kamvumilia mwenzie sana?. Narudia kukwambia mdogo wangu, nyumbani hutakiwi kuondoka kwa hasira. Na siku utakayoamua kuondoka, make sure umejipanga, wahenga waliposema "Ukitaka kuruka, Agana na nyonga" walikuwa na maana yao kubwa sana.

At 21, bado sana mdogo wangu. Tena kibongo bongo ndio kabisaaa. Tumia hizo hasira ulizo nazo kujipanga namna ya kuondoka hapo home. Kama Unaona huwezi kuendelea kukaa hapo mpaka utakapo graduate, basi atleast jiwekee deadline, then anza mipango ili kumeet hiyo deadline.

Unga kilo 2200, nyumba za kupanga hata huwe na taa moja tu ndani malipo ni 10000/=. Usije ukasoma story za watu waliosurvive kitaa zikakupa mori, mwaka mmoja una siku 365, na siku moja ina masaa 24. Haya masaa 24 ni mengi sana, hasa ukiyapitisha bila kupata proper meals.

Humu JF Ushawahi kusoma story ya yule jamaa aliyeondoka kwao kwa jeuri ya boom? Matokeo yake mambo yalikuwa tight ikafikia hatua giza likiingia anapanda juu ya mparachichi anakula Yale majani, then anaenda kushushia na maji bombani?

Fikiria upya mkuu. Then jipange
Mkuu em nitag hio story ya aliendoka home kisa boom😂😂😂
 
Pole sana kuna wazazi na walezi wengine huchangia kuharibu watoto manyanyaso yanakuwa mengi mm nishawahi ishi maisha kama hayo nilivumilia mpaka muda ulipofika nikaondoka.
Yeah ila mie naona inakuwa bora wanakufundisha maisha siyo lelema siyo unalialia tu baadae unataka unataka urithi!!!!
 
Umejaribu kuongea na mzaziwako wa kiume umsikie anasemaje huenda Kuna changamoto wazazi wanapitia hivo wanadhindwwa kuzuia hasira zao Kwa watu wengine kujitegemea na kusoma naona haviend pamoja waulize hata ambao walifnya hivo wengi waliishi Kwa shida sana
Ni kweli sametimes wazazi wangu huwa wanafokeana wenye kwa wenye hila huwa sifualiagi sana itakuwa hasira zao wananihamishia kwangu na mimi nataka niwe huru nisiwe mtumwa kama ni hasira zao basi wamaliziane wenye
 
Ni kweli sametimes wazazi wangu huwa wanafokeana wenye kwa wenye hila huwa sifualiagi sana itakuwa hasira zao wananihamishia kwangu na mimi nataka niwe huru nisiwe mtumwa kama ni hasira zao basi wamaliziane wenye
Mkuu usihame home, tumia kufokewa ka morali ya kupambana, tumia kama morali ya kusoma umakize chuo vizuri

Itumie kama morali tu usisahau mama naye ni binadamu

Sema mimi mama angu akinifokea heeh waga namwambia ndo unanifokea sasa, ndo unanifokea 😂😂😂 hata ka nimekosea by then
 
Huko kufoka kaanza lini au wewe humjui maza ako??
Maana huyo sio mke kusema eti mmekutana ukubwani, umekua unamuona, au hujaishi nae muda mrefu??
Me namjua maza A to Z huwa akitoka kugombana na marafiki zake huko au kwenye shughuli zake akirudi nyumbani hasira zote ananiamishia kwangu sasa mimi najiuliza nimemkosea nini maana kosa dogo ataongea hapo mpaka majirani wanasikia nami nimemchoka
 
Mkuu usihame home, tumia kufokewa ka morali ya kupambana, tumia kama morali ya kusoma umakize chuo vizuri

Itumie kama morali tu usisahau mama naye ni binadamu

Sema mimi mama angu akinifokea heeh waga namwambia ndo unanifokea sasa, ndo unanifokea 😂😂😂 hata ka nimekosea by then
anasema eti 'mungu atanipambania' anachukulia pesa ni rahisi sana 😂
 
Back
Top Bottom