Nimecheka sana unaposema eti umemvumilia sana. [emoji28][emoji28][emoji28]
Mpaka umri huo, nani kamvumilia mwenzie sana?. Narudia kukwambia mdogo wangu, nyumbani hutakiwi kuondoka kwa hasira. Na siku utakayoamua kuondoka, make sure umejipanga, wahenga waliposema "Ukitaka kuruka, Agana na nyonga" walikuwa na maana yao kubwa sana.
At 21, bado sana mdogo wangu. Tena kibongo bongo ndio kabisaaa. Tumia hizo hasira ulizo nazo kujipanga namna ya kuondoka hapo home. Kama Unaona huwezi kuendelea kukaa hapo mpaka utakapo graduate, basi atleast jiwekee deadline, then anza mipango ili kumeet hiyo deadline.
Unga kilo 2200, nyumba za kupanga hata huwe na taa moja tu ndani malipo ni 10000/=. Usije ukasoma story za watu waliosurvive kitaa zikakupa mori, mwaka mmoja una siku 365, na siku moja ina masaa 24. Haya masaa 24 ni mengi sana, hasa ukiyapitisha bila kupata proper meals.
Humu JF Ushawahi kusoma story ya yule jamaa aliyeondoka kwao kwa jeuri ya boom? Matokeo yake mambo yalikuwa tight ikafikia hatua giza likiingia anapanda juu ya mparachichi anakula Yale majani, then anaenda kushushia na maji bombani?
Fikiria upya mkuu. Then jipange