#COVID19 Napambana na COVID-19 deadly Delta

Mkuu umeongea maneno yangu yote mpaka nikahisi ni Mimi! Tofauti yetu ni kwamba Ugonjwa huu umeniacha Yatima. Umewachukua Baba na Mama!
 
Pole
daahh rangi ya bluu ni kwamba oxgen level ilikuwa chini sana.
huu ugonjwa toka mwaka umeanza umeshaondoka na 4 family members akiwemo mamaangu!!
na hapa sshv naongea mwingine amelazwa na ventilator juu...
acheni maskhara kbs.
Mkuu
 
Asante

Chukua tahadhari makinika, vaa barakoa ukitoka nje, nawa kwa maji tirirka na sabuni, epuka mikutano na msongamano, fanya mazoezi na toa elimu kila unapopita. UVIKO-3 ni hatari.
Dah pole kaka..mimi nimempoteza ndugu yangu juzi tu hapa kwa UVIKO...
 
Pole sana mkuu!
Covid19 ya awamu hii ndio umeitwa "deadly delta" ?
 
Magufuli ameharibu akili za watu,,majinga mengi yanapinga uwepo wa Covid19,eti wanamuenzi magufuli, Covid19 ipo, sisi mtaani kwetu tushazika watu karibia wanne
 
mkuu dawa zipi izo za kikohozi watumia
Inategemea na stage uliyoifikia ila kwa kuanzia ni Strong corticosteroids inaweza kuwa ni inj. au tabs high dose, antibiotics, ascorbic acid na anti coagulants
 
Upone haraka mkuuu, nashukuru kwa kuorodhesha hizo dalili.

Hivi karibuni nimekuwa nahisi vichomi kwenye kifua,joto la mwili liko juu,usingizi sipati,kichwa kinauma,mwili wote na mifupa kuuma na sometimes ucku nilitetemeka na uchovu wa hapa na pale japo sikohoi , Hali ambayo sijawahi experience kwa miaka mingi.

Nimelazimika kuingia jukwaa hili nione kama ntapata dalili kama zangu Ili nijue cha kufanya,nimepima vipimo vya kawaida kama typhoid,UTI,malaria na tumbo hakuna kitu.Hapa nawaza niendelee na vipimo au nitafute mkondo mwingine wa matibabu.

Siku nimeenda hospital kuchek afya walipima joto hakukuwa na shida ila Jana mchana hadi naandika sms hii joto liko juu Sana.Hapa Niko stuck nifanye uamzi upi japo tunatakiwa kutokuwa na hofu but lolote linaweza kutokea.Daa hatari sana may God helps me..
 
Unfortunately tahadhari ya mtu mmja haina maana kabisa
 
Kama upo Dar Nenda SANITAS kwa Dr.Hussein Bhaloo... mwelezee kinagaubaga tatizo lako utapona... Amesaidia wengi sana... Wahi Number Nenda saa 12 na nusu yeye uanza saa 3 ana Wagonjwa wengi sana
 
Tuliruhusu uongo uenee, tuliulinda kwa manufaa yetu ya kisiasa. Tulipiga vita ukweli. Baadhi ya wasema ukweli waliswekwa ndani,, basi uongo ukazidi kutamba sana. Vichwa vimehabarishwa uongo hadi vimetota. Kuuondoa haiwezi kuwa kazi ndogo.
Tuombeane [emoji120]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Sasa we jamaa sijakuelewa,kwa kuumwa huko ndo umesha jipima kwamba una ka Covid-19?

Sioni maelezo ya kupimwa kwako na kutuaminisha kwamba uliugua huo ugonjwa, hivi wa Tanzania mna nini?
Kunamawe zenu mazwazwa nyie
yule kenge wenu mkuu alitafunwa na mdudu covid, na ameaacha legasi ya huruhusiwi kupimwa mtu mpaka uwe una uthibitisho wa kusafiri.
mzee wa familia rafiki juzi alikuwa Aga Khan, na waliwaambia familia hapimwi mtu mpaka ulete uthibitisho wa safari ya nje ya nchi, kwa mujibu wa serikali ya wala vumbi,
Iliwabidi wakachakachua pasi ya karatasi ya kubumba na kibali cha kenya, hapo ilikuwa too little too late na muda wote walikuwa hawaruhusiwi kumuona tofauti kama angekuwa zahanati ya (mwanamatabatakizuanirangitatu ) mngelundikwa chumba kimoja na uji wa mgonjwa muendeleze legasi ya maambukizi, wakati wanarudi na karatasi hospitalini mzee tayari amepunzika milele
Halafu unaleta hekaya za kupimwa covid maaamalamae zenu covidiots nyie,
 
Ukimuona daktari tena, mpe somo kuhusu hii dawa inayotumika kusaidia kuepusha kuwa mgonjwa mahututi na uhitaji wa oksijeni au ventilator
inaiitwa dexamethasone steroid, ni ipo pande zote duniani.

 
Sasa we jamaa sijakuelewa,kwa kuumwa huko ndo umesha jipima kwamba una ka Covid-19?

Sioni maelezo ya kupimwa kwako na kutuaminisha kwamba uliugua huo ugonjwa, hivi wa Tanzania mna nini?
Jamani, tusijidai wehu, ugonjwa huu upo na mm binafsi ni muhanga, wiki ya nne Sasa nipo kitandani Na bado cja recover vzr,
Dalili alizo ziongea huyo bwana ni za covid na pia mm hakuna dawa za mitishamba na hospital ambazo sijatumia, kila nilichoambiwa ni dawa nilinyookea bila hata kujali side effect,
Turudi kwenye point ya kupima, ni ujuha mtu mzima umevuta bangi zako kupinga hoja ya mtu eti kwasababu hajapima ku confirm ugonjwa, maabara inayo deal na covid ni moja tuu Tanzania na ipo Dar, kwa wa mikoani majibu hurudi baada ya 72 hours na kama ni Corona ya Sasa lazima utakuwa Usha kufa,
Sasa kinacho fanyika nikwamba, ukienda hospital na kumuekeza daktari akakukuta una dalili tatu t za covid yy anacho kifanya ni kuku suspect Kama mgonjwa wa covid na kukuchukua x-ray ya mapafu na akikuta yana shida hapohapo anaanza kuku treat Kama mgonjwa wa covid,
Binafsi mm nilifanyiwa hivyo ikiwemo kudungwa sindano 12 za Acef kwenye mshipa na kupewa antibiotics Kali sana ,pia kufanya mazoezi kila wakati, kula vizuri na kuhakikisha unatumia maji ya moto yenye limao Kama kinywaji Chako na matunda kwa wingi ilikupandisha Kinga ya mwili, usisahau kutumia vitamin C,
Sasa huyo anaesema et mpaka upimwe ni mwehu mpuuzeni kabisa,anaongea maana haijamkuta,kwa yeyote anaye taka ushauri asisite Kuni pm,mm ni muhanga wa covid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…