Napambana sana niwatoe hatua moja ndugu zangu



Jihangaikie Wewe Mwenyewe na Watoto Wako ndugu Yangu.!

Hilo jukumu unalolihitaji Litakufanya uje Ujute huko baadae hasa unakapokua 'age go' umezeeka..!

Kila Mmoja hata kama ulimtoa kimtaji atakuwa na Yeye anahangaika na Familia yake na sio Wewe.!

Ukijichanganya tu..ujue itakuLamba..!
 
Hongera sana dada Ubarikiwe, mimi story yetu ipo tafauti baba yetu ana mwanamke mwingine hatujali kuanzia mimi mpaka wadogo zangu kwenda tu nyumbani alisikia nataka kwenda akanitukana na kunifukuza

GOD BLESS YOU
 
Charity begins at home
Wasaidie mama ila waambie wapambane sana maana mwanaume ni kupambana
Mimi nimeondoka home nikiwa 18 na nimepambana sana nimekutana na milima na mabonde
Nawapenda sana ndugu zangu niko tayari nitume senti yangu ya mwisho kwa anaepata shida ila Alhamdulillah wanajimudu ila tunapeana kama zawadi
 
Usimnunulie Hiace achana na hilo wazo mara moja. Kuna majirani zetu kijijini kwa bibi wana hela na mmoja maarufu ila Magufuli alivyoingia madaraka alimsumbua, yule jamaa na kaka yake wanajiweza walimnunulia kaka yao kijijini Hiace. Akashindwa maintenance na kulitunza, kila likifa anapiga simu kuomba hela ya vipuri na hela anazozalisha hazionekani.

Mara nyingi ndugu kama hao wameishashindikana hata mtazamo wa kimaisha (nisijue wa kwako). Wana mazingira duni kuanzia marafiki na washauri, hawajawahi fanya biashara ngumu kama Hiace hivyo ukiwapa ndio wataanza kujifunzia na kujifunza kuna kufeli.

Mimi ninachoweza kufanya ni kuwapa elimu watoto wao, uanzishe generation mpya inayojielewa. Alafu anzisha miradi midogomidogo ya gharama ndogo kati ya wote kuna watakaofeli achana nao endelea kujali wanaofanikisha hicho kidogo.

Usifuge uvivu na ubwetekaji ile kila kitu "dada atafanya". Usitambulike kama generous kwao, toa kwa masharti na uwe na haki ya kukagua mwendelezo na kuwa mkali.
 

Wahindi na waarabu hawako hivyo, walichofanya/wanachofanya ni kutengeneza utajiri mkubwa na kuufanya Mali ya familia.

Kila mwenye akili anashika angle na wale vichwa ngumu wanaishiwa kuwa waajiriwa wakilipwa mishahara waweze kuishi.

Huwezi kusaidia ndugu ilihali wewe mwenyewe unajitafuta, utaishia kuwasaidia na bado usifanikiwe na wewe pia utaangukia shimoni na watoto wako watakosa msaada.

Njia pekee yakuinua familia ni wewe kupambana kujenga uchumi mkubwa na investment za kutosha na hapo ndio unaweza kusomesha vizazi kadhaa vya ndugu zako vije kuwa sehemu ya biashara na kuleta consistency.
 
Kuna familia unakuta ndugu walikataa shule na kuendekeza ujinga kama pombe, umalaya na ujinga mwingine, wewe ukatuliza akili ukapiga either shule au mitikasi ukiwa na descipline kubwa halafu ukatoboa.

Unaanzaje kusaidia ndugu kama hawa?
Kuna wakati naamini waAfrica tunalea ujinga sana.
 
Ni kweli tunalea ujinga, ila kuna kitu inaitwa second chance, people are subjected to mistakes. Kama mtu ameonesha nia ya kubadilika msaidie.

Lengo sio kutengeneza kizazi kama cha waarabu uliowamention huko juu , Lengo ni kuhakikisha Wanaweza kuafford basics (chakula, malazi, mavazi) Na hapa nazungumzia your immediate family, sababu huwezi saidia “ukoo wote”

Sio kila familia itakuwa kama ya Baresa/balesa.
 

Ni kweli kuna second chance, lakini unakuta discipline haipo kabisa hata baada ya hiyo second chance, lakini unakuta mtu 1st chance amefail na kabla ya second chance haonyeshi kujutia au signs za changes bado anaendeleza tabia ileile hata baada ya vikao vingi sana.

Familia nyingi za kiAfrica zinapitia haya, naamini kila mtu anamoyo wakusaidia lakini shida inakuja either anayepaswa kusaidia naye ndio anajitafuta au msaidiwaji haonyeshi ushirikiano.
 
Mkuu kwani Mimi nimeandikaje hapo? Na mtoa mada kaandikaje?
 
Sahihi.
 
Haha pole.
Ndg huwa hawabebeki utakufa kwa stress.

We pambania kombe waje kukutumikia kama Yusufu.

Ukimbeba Lutu hutafika popote.
 

You took the words right out of my mouth.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…