Napambana sana niwatoe hatua moja ndugu zangu

Napambana sana niwatoe hatua moja ndugu zangu

Ni jambo jema na zuri kusaidia ndugu.
Ila ni vyema pia kujua kama huyo unayepanga kumsaidia anasaidika.
Mfano
1)mtu ambaye tayari ameanza kupambana katika shughuli kazi fulani,au ana ujuzi fulani au ana penda kipaji kufanya shughuli fulani iwe ujasiriamali/biashara,ujuzi ufundi,kilimo,ufugji ,kazi yoyote halali
akaomba umshike mkono kumuongezea labada mtaji kidogo,vifaa vitendea kazi,mashine za kazi yake ambayo anaifanya,kumuongezea labda ujuzi,mbolea,mbegu,dawa za wadudu kama ni mkulima n.k MARA nyingi watu hawa wenye spirit ya upambanaji kwanza huwa wanaomba msaada mdogo sio mkubwa sana,pia wana shukrani,pia wanathamini kile ulichomuwezesha,pia ni wenye bidii wapambanaji,wanathamini kile ulichomuwezesha mana wanatambua umuhimu wake,pia hawachagui sana kazi ukisaidia mtu wa aina hii kuna uwezekano mkubwa wa msaada uliomsaidia ukaleta matokea chanya kwa sababu WANAJITAMBUA. na wana nidhamu ya kazi na nidhamu ya pesa na nidhamu ya maisha .
2)Kinyume chake ni kumsaidia mtu ambaye HAJITAMBUI kwanza ni mlalamishi,mtu wa kuchagua kazi,hana anachokifanya currently kama ni graduate unakuta toka a graduate amekaa anasuburi ajira ,hajui anataka nini,hana uzoefu wa shughuli yoyote ujuzi wowote,hana interest ya kufanya chochote ana lalamika na kuomba omba ,pia hana nidhamu ya pesa ,kupenda anasa starehe,
PIA NI VIZURI
Ukampa msaada wa kitu mtu anachokiweza kipaji,interest yake anachokipenda ..wewe unaweza ukawaza umfungulie biashara kumbe sio wote wanaweza kufanya biashara ,sio wote wanawezs kufanya kazi ya usafirishaji ,japo mtu anayejiekewa anaweza asichague kazi akafanya hata ile asiyoipenda akiwa anajitafuta ili akijipata afanye kazi ambayo ana kipaji nacho.
Kabla ya kumpa HIACE angalia pia kama ana interest na hiace au anza kumpa boda boda kwanza.
AANZIE CHINI ukiwa unamsoma displine yake na kipaji au uwezo wake
Akimudu boda boda au bajaji productivily ni rahisi kumudu hiace hata bus.
Akifeli kwenye bajaji sio rahisi akafaulu kwenye hiace.
 
masai dada angalia mahubiri ya ijumapili hii iliyopita ya mchungaji eliona kimaro ,ndugu sio wakusaidiwa saudia wazazi wako
 
Hongera sana kwa kuwa na moto huo!! Japo sisi wengine tulijaribu kuwainua ndugu zetu lakini mpaka leobado wanahisi wanahitaji kusaidiwa. Ila hatuwatupi tu nakomaa nao kadri uwezo unaruhusu
 
Kuna mtumishi alichukua mkopo wa watumishi ili amsaidie ndugu yake mchimbaji mdogo kununua mashine ya kupima ardhini kuangalia miamba yenye madini
Maana changamoto yake ilikuwa ni hiyo mashine ambapo ilinkufanya kazi ya uchimbaji alilazimika kukodi kwa garama kubwa na kwa muda wa saa moja.
Mtumishi huyu akamwambia ndugu yake nachukua mkopo benki nakununulia mashine mpya,ila mimi ninachotaka tukubaliane hili deni la mkopo utakuwa unalilipa wewe kila mwisho wa mwezi nitumie marejesho maana nakatwa kwwnye mshahara .
Baada ya kumpatia mashine ,ndugu akawa anaikodisha anapata hela anazitumia kwa anasa uzinzi,pombe starehe ,mashine vifaa vikaanza kupote kimoja kimoja seti ikabaki nusu.Akituma marejesho mwezi mmoja tu.Mtumishi kamsamehe mpaka sasa anapambana kulipa deni kwa kukatwa mshahar wake kila mwezi.Yule ndugu hela anapata ila hana displine.
Kama angekuwa na displine wangefika mbali mana ile mashine inawasaidia watu wengine wanaoikodi na walioiba vifaa.Wanapima wanapata madini wanachimba yeye anapata pesa kidogo ya kuikodisha na baadae alikuja kuiuza kwa hasara.Mtu ambaye hana nidhamu ya kazi,nidhamu ya pesa ,uaminifu,bidii katika kazi,hasaidiki tena msaada wako unaweza ukawa sababu ya kumuumiza mana pesa ni kama kisu ukitumia vibaya kinakukata mwenyewe.
 
KI IMANI KUSAIDIA NDUGU NI JAMBO JEMA KUWAJALI WA NYUMBANI KWAKO/KWENU.
 

Attachments

  • Screenshot_20241106-155152.jpg
    Screenshot_20241106-155152.jpg
    89.5 KB · Views: 5
Wala hukosei, pambana usaidie, lakini kamwe usiiweke moyoni, inaweza kukutesa baadae kama uliowasaidia wakakukosea adabu, kukujali ama kukupa msaada baadae.
 
Wala hukosei, pambana usaidie, lakini kamwe usiiweke moyoni, inaweza kukutesa baadae kama uliowasaidia wakakukosea adabu, kukujali ama kukupa msaada baadae.
TENDA WEMA UONDOKE ZAKO USINGOJE SHUKRANI.
Shukrani ya punda wakati mwingine ni mateke.
JAPO WEMA HAUOZI.
 
Ndio kaka
Ana ela kama nini
Ila dah naskia uzuni sana
Walah nakwambia
Ila sitaki sana kumuongelea
Naona kama Mungu kanipa hilo jukumu baada ya lango kuzingua

Aisee nina uchungu
Hapa namtafutia brother yangu mmoja hiace ya kufanya kama daladala mkoani
Kwa uchungu sana

Nampigia bro kumsalimia na madogo m(wanae) anakwambia ninapanga holday twende nchi gani
Yaani roho inaniuma hivi aoni ndugu zake???
Achana na mambo haice Kuna uwezekano wakupoteza pesa tafuta eneo wajengee nyumba utabarikiwa sana huo mradi unayotaka kuwaanzishia zitafaidi zaidi sketi hutoamini tafuta kiwanja uwajengee nyumba
Biashara ni habari nyingine inahitaji watu wenye skills za kutosha
 
Achana na mambo haice Kuna uwezekano wakupoteza pesa tafuta eneo wajengee nyumba utabarikiwa sana huo mradi unayotaka kuwaanzishia zitafaidi zaidi sketi hutoamini tafuta kiwanja uwajengee nyumba
Biashara ni habari nyingine inahitaji watu wenye skills za kutosha
tena hata nyumba ukiwajengea hati isome jina lako na ukae nayo wewe,hawakawii kuuza,ili siku wakitaka kuuza wasiweze.
Na mifugo wafuge na kulima.
 
Mwenyezimungu akusimamie katika mambo yako! Mi nasemaga hakuna investment nzuri kama kuinvest kwa ndugu zako hapa ndo wanatushindaga wenetu wahindi na waarabu. Utajiri unazunguka tu kwenu nyinyi wenyewe hata siku uki-fail unajuwa unaanza wali sio ukianguka wewe basi kila kitu kimeiaha wote mnaanza moja
Bahati nzuri umetaja wahindi na waarabu, nakuhakikishia, ndugu wengi wa kiafrika ni hopeless kbs...utasaidia na watakupiga matukio, mimi nimeyaona.
 
TENDA WEMA UONDOKE ZAKO USINGOJE SHUKRANI.
Shukrani ya punda wakati mwingine ni mateke.
JAPO WEMA HAUOZI.
Mie naishi katika imani kuwa nikitenda wema, malipo yangu yapo kwa mungu, haijalishi niliyemtendea wema na atanitendea wema au lah, lakini kwa mungu malipo yangu yako pale, akinitendea wema nae atalipwa wema wake na akinitendea ubaya nae atalipwa ubaya wake..
Na malipo ya mungu ndio makubwa kuliko akupacho mwanadamu.
 
Mie naishi katika imani kuwa nikitenda wema, malipo yangu yapo kwa mungu, haijalishi niliyemtendea wema na atanitendea wema au lah, lakini kwa mungu malipo yangu yako pale, akinitendea wema nae atalipwa wema wake na akinitendea ubaya nae atalipwa ubaya wake..
Na malipo ya mungu ndio makubwa kuliko akupacho mwanadamu.
ameen.
 
Back
Top Bottom