Napambana sana niwatoe hatua moja ndugu zangu

Unakosea badala ya kupush ulipoolewa unahangaika na kwenu ulipotoka
 
Upo sahihi sana Mungu anataka kukutumia kwa ajili ya ndugu zako na amini kwamba misaada unayotoa sasa Mungu atakubariki siku za mbeleni.Watoto wakiume wengi wanamajukumu sana kuanzia mke watoto ndugu zake ndugu wa mke nk tofauti na wanawake
pole!
Daima toa kwa ndugu.

mimi ndugu zangu hata sijali,nasaidia Tu,siachi ndugu yangu ateseke nikiwa hai.

Nashukuru Mungu hapa nilipo.
 
Una moyo mzuri na wazo lako ni zuri sana ila kuwa makini sana kujijali pia. Kwenye kusaidia ndio huwa tunatengeneza maadui wa kudumu. Nikupe wazo usinunue Hiece ukampa bro kama zawadi bali hakikisha kupitia wao na wewe kuna faida unapata ambayo baadae huta regret kutoa msaada.

Hakikisha kwenye msaada kuna manufaa yako pia. Kwa mfano ukinunua Hiece inakuwa yako ila unamkabidhi aisimamie na percent fulani akupatie. Na hapa hakikisha unafuatilia Ikirudisha kiasi fulani cha pesa unamwachia rasmi. Kuna watu wamepewa assets kama hizo walibadilika kabisa wakawa na matumizi ya hovyo ya pesa.

Kama umri unaruhusu wape ujuzi fulani. Peleka chuo cha ufundi wawe na skills zitakazowasaidia kupambana na mfumo wa maisha. Kama mtu ana hobe ya ukulima nenda kwenye maeneo potential ya kilimo mpatie mtaji wa kuendesha shughuli zake ila hakikisha na wewe unapata hekari za kutosha ambazo atazisimamia.

Anzisha miradi ambayo watasimamia na wewe ukinufaika vinginevyo utakuwa disappointed.

Si wote watakuangusha ila kuwa mwenye tahadhari sana ili uutunze undugu.
 
Hongera sana, ila kutoka kimaisha inataka mtu mwenyewe apambane kutoka point A to B, kama hawana hiyo kitu unaweza ukasaidia mpaka tone lako la mwisho na watu wapo pale pale unapojaribu kuwatoa.
 
Asee
 
Mke wa kaka yako nae anajitahidi kuwasaidia ndugu zake wakae sawa. Huenda hata mume wako hana tume sana na ndugu zake kwa sababu nguvu zote mmehakishia kwa ndugu zako.

Kuna namna dada zetu wameumbwa, kusaidia ndugu ila kumbuka majukumu makubwa ya familia zao(walipoolewa) yanabebwa na waume zao. So wao hawana mzigo mkubwa wa kubeba.
 
Wanawake wanazingua mnoo,unakuta kwenye familia kipato chote anapeleka kwa ndugu zake
 
Wasaidie mama na Mungu akubariki. Nimekuja kugundua sie watoto wa kike tuna huruma sana na ndugu zetu.

Lakini pia tusiwalaumu sana kaka zetu, huwa mara nyingi hawawi open kwa yale wanayopitia. Yawezekana unamuona ana hela, ila ameelemewa pia.
 
Umekosa kazi ya kufanya siku utakuja kujiona ulikua mjinga wa Karne
 
Hongera sana dada Ubarikiwe, mimi story yetu ipo tafauti baba yetu ana mwanamke mwingine hatujali kuanzia mimi mpaka wadogo zangu kwenda tu nyumbani alisikia nataka kwenda akanitukana na kunifukuza

GOD BLESS YOU
Huwa sipendi wanaume wanaolalamika kwamba baba yetu/yangu hatujali haliyakua amekusomesha mpaka chuo kikuu au diploma.

Hivi ushawahi kukaa ukawaza Mzee wako alitoboa vipi maisha?, au nae alisaidiwa?.

Chukua hatua kuwajibikwa kwa ajili ya maisha yako, kama msaada utakuja hio mshukuru Mungu lakini usikae walaumu kama kusaidiwa nihaki yako.

Labda kama hujasoma unahaki ya kulaumu.
 
Mumeo, wewe na watoto wenu mmeshatoka?

Ukiwa kwenye ndoa jukumu lako la kwanza ni ndoa na familia yenu

Mumeo hana mke hapa

Kipato chochote cha familia kabla hakijatoka lazima mume na mke mkubaliane hasa inapohusu kuwasaidia wengine
 
Kuliko kuleta maneno huku uonekana ww wa msaada. Nenda kawasaidie kimya kimya.Ukishajitangaza tu huo sio msaada wala sadaka hiyo ni kiki
 
Usiongee kitu hukijui, mzee wangu ndie amekua ananizui fursa nyingi zisiende akisikia sehemu nimeajiriwa anatia chokochoko mpaka mambo anaharibika na hili anafanya ili kuonyesha kwamba watoto wa nje ni bora zaidi kwake
 
Usiongee kitu hukijui, mzee wangu ndie amekua ananizui fursa nyingi zisiende akisikia sehemu nimeajiriwa anatia chokochoko mpaka mambo anaharibika na hili anafanya ili kuonyesha kwamba watoto wa nje ni bora zaidi kwake
Siamini kama kuna mzee Mwenye akili hizo. Nahata ukiajiriwa nilazima ndugu/jamaa wajue umeajiriwa wapi?.
 
Siamini kama kuna mzee Mwenye akili hizo. Nahata ukiajiriwa nilazima ndugu/jamaa wajue umeajiriwa wapi?.
Kama huamini endelea kuamini unachokiona Sawa, ndugu zangu wa tumbo moja lazima wajue kwakua kazi ninayoifanya ni nyeti sana lazima awepo ndugu kama mwakilishi alafu mzee alishaacha kuwasomesha na wadogo zangu sio mimi tu nietelekezwa, chezea mchepuko nini! Nyumbani kipindi kile tulikua na mali kiasi kwamba mkoa X tulikua top three ila kwa sasa imebaki historia baada ya familia kutawanyana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…