Napata faida ghafi kwa siku 400,000=lakini mtaji hauongezeki

Napata faida ghafi kwa siku 400,000=lakini mtaji hauongezeki

Gharama ya bidhaa mpaka kuwa tayari kuuzwa
Gharama za uendeshaji wa biashara

Ukitoa hizo zote ndo unapata faida ya 400k per day?
 
Matumiz yepi hapo nimekuambia matumiz ni hayafiki 50000
Screenshot_20231118_093033_Chrome.jpg

Mtoa mada imebidi nigoogle kwanza faida ghafi kumbe ni gross profit,

Sasa kama laki 4 ni faida ghafi maana yake ni mauzo - gharama za bidhaa, swali kwako faida ni shilingi ngapi (net profit)

Maana unaweza kua na matumizi hayo uliyoyasema kwa siku ni elfu 50, kumbe unakula mtaji(jokes)

Lazima ujue faida halisi ni ngapi, na matumizi ni ngapi ndo uone hapo
 
View attachment 2817338

Mtoa mada imebidi nigoogle kwanza faida ghafi kumbe ni gross profit,

Sasa kama laki 4 ni faida ghafi maana yake ni mauzo, swali kwako faida ni shilingi ngapi (net profit)

Maana unaweza kua na matumizi hayo uliyoyasema lwa siku ni elfu 50, kumbe unakula mtaji(jokes)

Lazima ujue faida halisi ni ngapi, na matumizi ni ngapi ndo uone hapo
Faida ghafi siyo mauzo, ni Kiasi cha mauzo kinachobaki baada ya kutoa gharama za manunuzi ya stock husika.
 
Mbali na chuma ulete naskia wame advance zaid siku hizi mtu anaingia dukani mpaka katika droo haonekani namtu yoyote Kisha anachukua pesa anayoitaka
Mkuu ila twende mbele turudi nyuma.

Kama matumizi yako ni 50,000/= kwa siku ina maana katika net profit unabakiwa na 350,000/=. Tuseme una dharura au kuna hela huwa zinatoka kwa namna moja au nyingine kutokana na ukwasi wako tukadirie 100,000/= inatoka kwenda kwenye dharura na shughuli za maendeleo.
Unabaki na 250,000/= kwa wiki ni 1m (huwezi pata same faida kila siku).

Kwa mwezi ni 7m kwa mwaka ni 80m. Ina maana mtaji hauongezeki hata kwa 10m mwaka mzima? Je hali hii imedumu kwa muda gani?
 
View attachment 2817338

Mtoa mada imebidi nigoogle kwanza faida ghafi kumbe ni gross profit,

Sasa kama laki 4 ni faida ghafi maana yake ni mauzo - gharama za bidhaa, swali kwako faida ni shilingi ngapi (net profit)

Maana unaweza kua na matumizi hayo uliyoyasema kwa siku ni elfu 50, kumbe unakula mtaji(jokes)

Lazima ujue faida halisi ni ngapi, na matumizi ni ngapi ndo uone hapo
Sahih kbsa. Umemjibu kiuhasibu Sana. Mnk anacho fanya faida. Kabla hajatoa ghrama za uendeshaji na kila cost alizo ingia kwa siku ,week ,mwez Sasa yey anauza juis kweli upate laki nne kwa siku

Mm nauza mabati na nondo na faida yangu hata haifiki laki mbili kwa siku ila mauzo Ni makubwaa
 
Ngoja nikujibu kitaalamu kidogo.

Gross profit less expenses equals to net profit or net loss.

Based on that aforementioned equation you are spending more than what you earn hence when you come to add net profit/loss to capital unapata ongezeko dogo la capital.

Vipi ukiachana na hizo expenses zako kuna liabilities mahala una clear , madeni ya benki etc
 
Siku kumi tayar laki Tano iyo na mwezi mil1 na nusu
Mara mwaka million 18, hayo ni matumizi ya ndani
Hujapeleka mtoto shule,hujaumwa, hujajaza mafuta kama unausafiri, hujahonga
, hapo lazima mtaji usiongezeke matumizi makubwa mno mnooo
Umesahau kwa siku anapata faida ya 400k kwa mwezi ni 12M kwa mwaka ni 144M, toa hio 18M ya matumizi anabaki na 126M 🤔

Soma habari yote usikurupuke kujibu
 
mkuu kama unapata faida hiyo fungua account. pesa yote ya faida ukitoa ile ya matumizi ya kibinadam iweke benk kwenye akAunti maalum ambayo hutoweza kutoa.

baada ya mwaka uje kutoa ushuhuda. mimi siamini kwenye uchawi. mchawi wa kwanza ni wewe mwenyewe. ambae unashindwa kujibana na kusave mapato yako.​
 
kaka,me naelewa biashara za rejareja kwa uchache ina changamoto za uswaihli ila kama unapata laki 4 kama faida ina maanisha hapo hakuna uswahli ila labda useme unauza laki 4 kwa siku na ikatokea unatoa pesa ya kula n.k na haizid laki 4 ya matumiz tatzo lako lipo kweny kuchanganya pesa za mauzo na faida na hapo hapo unatumia kwenye kula na kununua bidhaa za dukani matokeo yake faida huion na kwa namna hyo uchaw ndyo unaingia lakin kama umetenga lak 4 ya faida pemben hapo n akil zako.
 
mkuu kama unapata faida hiyo fungua account. pesa yote ya faida ukitoa ile ya matumizi ya kibinadam iweke benk kwenye akAunti maalum ambayo hutoweza kutoa.

baada ya mwaka uje kutoa ushuhuda. mimi siamini kwenye uchawi. mchawi wa kwanza ni wewe mwenyewe. ambae unashindwa kujibana na kusave mapato yako.​
Huyu anataka kuambiwa kuwa ni ''chuma ule'' kitu ambacho hakuna. Sana sana naona kuna ufanyaji mahesabu mbovu ambao unaonyesha faida kumbe kiuhasilia siyo faida. Kama ulivyomshauri inatakiwa hiyo faida kama anadhani ipo basi aitenge kila siku jioni baada ya mahesabu na apeleke benki kila wiki au mara kwa mara.
 
Dawa ya mambo ya kiswahili a.k.a chuma ulete si simple tu mkuu uhitaji hata mganga.
1. Tia mkaa unapoweka hela.
2. Weka ndimu iliyochomwa na sindano.
3. Usipokee hela za jioni unapokaribia kufunga biashara au unapopokea zitenge na nyingine.
Fanya kimojawapo kati ya hayo.

Bila kusahau kuogea maji ya chumvi ya mawe.
Mambo ya ujima haya, unampoteza zaidi.
 
Back
Top Bottom