Napata faida ghafi kwa siku 400,000=lakini mtaji hauongezeki

Napata faida ghafi kwa siku 400,000=lakini mtaji hauongezeki

Habari wakuu ushauri kwenu nahitaji.

Katika biashara zangu tatu wastani wajumla napata faida ghafi laki nne kwa siku wakat mwingne huzid hapo.

Ila mtaji wangu kwa mwaka nikama hauongezeki uko pale pale.

Ukizingatia matumizi yangu kiujumla kwa siku ni 40000-50000 sababu ya familia kubwa.
Ukiona hivyo kuna mtu anafaidika kwenye biashara yako ambaye siyo wewe.

Fuatilia transactions zako zote kwa mwezi na angalia bank deposits kama zinaoana na bank statements na kisha anza kushiriki usimamizi wako wa moja kwa moja kwenye biashara zako.

Hakikisha kama umeajiri ndugu anza kuwaondoa mmoja mmoja na labda ufungue small scale business somewhere uwape waendeshe kisha wawe wanakuletea hesabu
 
Mkuu nafanya stock taking na hivo vyote unavyovisema
I dont trust you at all. Kama unasema kweli basi kuna kitu unafanya kimakosa kwenye mahesabu na hujui kuwa unakosea. Possibly pia kuna wizi ambao huwa unatokea kwenye mali au mauzo lakini hujagundua. Nina experience ya muda na hizi biashara za aina hii na pia maduka ya nguo au bidhaa na nimeshakutaka na visa vingi vya fedha kupotea bila kujua lakini mwishowe inakuja kugundulika ni wizi na biashara bila mahesabu.
 
Mpaka nahis ntakua nafanyiwa mambo yakiswahili

Hakuna cha uswahili unaibiwa na mfanyakazi wako ama mtu mwingine ambaye alishakusoma!!!
Hivi majuzi tu nimemkamata mwizi wangu baada ya kumwekea mtego!
In short nipo na goli mahali, so pale kuna vijana watano, miezi mitano ya mwanzo hesabu zilienda vizuri, baada ya hapo jioni nikienda fedha hazionekani, wakasema chuma ulete nikawabishia kabisa, wakasema jumapili njoo ushinde uone!
Daah kweli bhana zipo fedha nilizitenga kama laki 6 hivi, kufika kuja kuzitazama zimeenda!!
Ndipo nikaja na wazo la kufunga cctv maeneo yote nyeti kwa siri!
Hatime nikalufanya, na mwizi akanaswa live na wala hakuwa miongoni mwa vijana wangu!
Niishie tu hapa maaa kesi inanguruma!!!
 
Habari wakuu ushauri kwenu nahitaji.

Katika biashara zangu tatu wastani wajumla napata faida ghafi laki nne kwa siku wakat mwingne huzid hapo.

Ila mtaji wangu kwa mwaka nikama hauongezeki uko pale pale.

Ukizingatia matumizi yangu kiujumla kwa siku ni 40000-50000 sababu ya familia kubwa.
Faida ghafi kwa lugha nyingine huitwa Gross profit (mauzo kabla ya kutoa gharama)
Sasa mauzo ya laki nne yaweza kuwa mengi sana au kidogo kulingana na Biashara unayofanya.
Mfano: kama unauza sukari kwa jumla, mifuko 4 ya kilo 50 inaweza kukupa Mauzo ghafi ya zaidi ya shs laki nne ila faida yake ni kwenye 25,000 ina maana ukitumia zaidi ya 25,000 unakula mtaji
Ila ukiuza chakula (mgahawa) Mauzo ghafi ya Shilingi laki nne; unaweza kuta faida ni shs 200,000 =
nk nk nk
Kukusaidia; unatakiwa ujue kwenye hayo mauzo ghafi, wastani wa faida (net profit) ni kiasi gani ili ujue ukichukua hiyo 50,000 ya chakula/familia; faida inabaki kiasi gani
 
Habari wakuu ushauri kwenu nahitaji.

Katika biashara zangu tatu wastani wajumla napata faida ghafi laki nne kwa siku wakat mwingne huzid hapo.

Ila mtaji wangu kwa mwaka nikama hauongezeki uko pale pale.

Ukizingatia matumizi yangu kiujumla kwa siku ni 40000-50000 sababu ya familia kubwa.
Gross Faida laki 4,
Net Faida kiasi gani?
Matumizi tushajua ni 50k,
 
Mpaka nahis ntakua nafanyiwa mambo yakiswahili
Ahahaa....mswahili apo ni wewe mwenyewe niamini ndugu...

Biashara ni namba mkuu....mfano 12 na 21 apa zpo namba mbili tu zinazofanana lakini thamani za hzo namba ni tofauti...

Zingatia wewe na biashara yako....ni vitu viwili tofauti kabisa...biashara ni biashara na wewe ni wewe kitendo cha kufanya biashara ni rafiki yko (mazoea) unachukua maokoto unavyojisikia,unakopa haulipi....mwisho wa siku lazima update hasara.

Nakushauri ukiwa na biashara....
1. Jitahidi kuandika manunuzi,matumizi na mapato.
2. Tunza kumbukumbu za miamala unayofanya pamoja na risiti zake..
3..Funga hesabu kila mwisho wa biashara [inategemea na aina ya biashara lakini]
4. Hakikisha unajilipa sehemu ya faida ya biashara yako kwanza......kinachobaki kipeleke kwenye biashara (mtaji)...

ICHUKULIE BIASHARA YAKO KAMA MTU BANDIA....UKICHUKUA PESA KWENYE BIASHARA HUO NI MKOPO UMEIKOPA BIASHARA NA UNAPOWEKA PESA KWENYE BIASHARA HUO NI MKOPO UMEIKOPESHA BIASHARA....

.....naweza kukusaidia kwenye kuandaa hesabu zako,na tukampata mchawi wako....kwa makubaliano maalumu.
 
Kuna mahali ubakosea na bila shaka ni kwenye matumizi.

Kama hupati hasara ni kwa vipi mtaji usiongezeke.
Ada za watoto unalipa kutokea wapi? Hizo juice kina junia wakija dukani hawachukui bila kulipa?

Vipi hao wafanyakazi wako, hawajakusoma jinsi unavyofanya hesabu zako na wao wakazifix ili uone ni shwari, au unawaamini kwa kiasi gani??

Fanya tathmini yako vizuri na kwa umakini utajua tu..

Siamini kama ni chuma ulete.
 
I dont trust you at all. Kama unasema kweli basi kuna kitu unafanya kimakosa kwenye mahesabu na hujui kuwa unakosea. Possibly pia kuna wizi ambao huwa unatokea kwenye mali au mauzo lakini hujagundua. Nina experience ya muda na hizi biashara za aina hii na pia maduka ya nguo au bidhaa na nimeshakutaka na visa vingi vya fedha kupotea bila kujua lakini mwishowe inakuja kugundulika ni wizi na biashara bila mahesabu.
Nin solution yake
 
Habari wakuu ushauri kwenu nahitaji.

Katika biashara zangu tatu wastani wajumla napata faida ghafi laki nne kwa siku wakat mwingne huzid hapo.

Ila mtaji wangu kwa mwaka nikama hauongezeki uko pale pale.

Ukizingatia matumizi yangu kiujumla kwa siku ni 40000-50000 sababu ya familia kubwa.
Faida ghafi unaipataje, ni sawa na maizo au maizo toa Nini?
 
Mengineyooo ni Mengi kuliko ya msingiii...!!
 
Fanya mahesabu vizuri, napia biashara zako zitenganishe kusiwe namuingiliano wakifedha kati ya moja nanyingine, unawezakuta hardware imetoa faida ya laki4 halafu vinyanywaji vikakukata laki4 ningumu kujua bila kuzitenganisha
 
Habari wakuu ushauri kwenu nahitaji.

Katika biashara zangu tatu wastani wajumla napata faida ghafi laki nne kwa siku wakat mwingne huzid hapo.

Ila mtaji wangu kwa mwaka nikama hauongezeki uko pale pale.

Ukizingatia matumizi yangu kiujumla kwa siku ni 40000-50000 sababu ya familia kubwa.
Angalia stock zako zimeongezeka au zimepungua? Kama zimeongezeka mean mtaji umepanda.Kama zimepungua unatakiwa uwe na Cash nyingi mkononi.
 
Back
Top Bottom