Napata harufu ya matumizi ya Nyuklia Ukraine baada ya Kursk kuanguka

Napata harufu ya matumizi ya Nyuklia Ukraine baada ya Kursk kuanguka

After few weeks Russia alipovamia Ukraine. NATO wakatenga bajeti ya miaka 5 kuisupport Ukraine. Sehemu kubwa ya watu tukasema wazungu wanazingua, Ukraine hawezi maliza miezi miwili akipambana na Russia.

Sasa hivi vita inatembea mwezi wa pili na nusu unatafutwa mwezi wa 3. Mzungu huwa anatumia akili nyingi sana kupiga hesabu zake.
Putin amepigiwa hesabu ya miaka 10 ijayo.

Kuna mwaka Putin atakuja kuondolewa na Warusi wenyewe sababu ya majnga yatakayo ikumba Rusia hasa uchumi
 
I think it's a game plan,

Vita inaelekea kwisha, wameona wawwachie kidogo ili wapate nafasi ya kukaa mezani.

If you remember, Russia alikuwa ameingia mpaka Kyiv mwanzoni mwa vita wakamwambia ili waanze mazungumzo atoke Kwanza then wakamgeuka.

Nadhan itakuwa vice versa ili wapate nguvu na justification kwa wananchi ya kukaa mezani
 
Putin anapukuchuliwa taratibu mpaka ataisha.

West wanampukuchua Putin kwa akili sana.

Angalia walianza kumpa Ukrain silaha ndogo ndogo ila kadiri siku zinavyozidi kwenda wanaongeza uzito wa silaha, ni kama vile mtoto unaanza kumpa Uji baadae ugali.

Mwanzo Marekani ilikuwa inawambia Ukrain marufuku kushambulia ndani ya Rusia, ila sasa hivi Ukrain ruksa kushambulia Rusia.

Mwishowe tutaanza kuona makombora yakitua Moscow hapo ndio Putin atashtuka kwamba kumbe kapukuchuliwa kweli.

Nmeshangaa sana Putin kaishiwa makombora hadi anaomba kutoka Iran.

Vita ni gharama, lakin wafuasi wa Putin ukiwambia hili kwamba Urusi baadae itakuwa hohehae wana bisha ila muda utaongea
Bakia kwenye siasa za bongo mzee, upande huu hauelewi chochote.
 
Putin amepigiwa hesabu ya miaka 10 ijayo.

Kuna mwaka Putin atakuja kuondolewa na Warusi wenyewe sababu ya majnga yatakayo ikumba Rusia hasa uchumi
20240814_192552.jpg
 
Attachments

  • 20240814_192546.jpg
    20240814_192546.jpg
    284.9 KB · Views: 8
  • 20240814_192528.jpg
    20240814_192528.jpg
    254.8 KB · Views: 7
Ukraine hana army ya kupiga russia kwa mda mrefu na kulinda maeneo anayo chukua na ku defend ndani kwenye maeneo yenye vita kwa wakati mmoja
Watu hawaelewi, sijui wanafuatilia habari kutokea wapi make hata mainstream media wanasema Ukraine amefanya gamble ya kijinga sana, why utumie resources zako chache za muhimu kuvamia eneo ambao kwa namna yoyote hautaweza kulikalia hata kwa mwezi mmoja halafu unaacha kulinda maeneo yako mengi ambayo yanaelekea kuanguka?
 
Putin alifanya kosa kubwa sana kuivamia Ukraine angebaki na mikwara yake ya kwenye TV kumbe uwezo ule tuliokua tunadanganywa hana leo hii anategemea siraha kutoka NK na Iran kweli?
Huyo ashakaguliwa ndio maana USA wamemruhusu apigwe hadi Moscow na Zelensky anasema apigwe hadi kwake ili asitishe vita kwa makubaliano..sasa hivi tunapewa mikwara ya Nyuklia tena..
 
I think it's a game plan,

Vita inaelekea kwisha, wameona wawwachie kidogo ili wapate nafasi ya kukaa mezani.

If you remember, Russia alikuwa ameingia mpaka Kyiv mwanzoni mwa vita wakamwambia ili waanze mazungumzo atoke Kwanza then wakamgeuka.

Nadhan itakuwa vice versa ili wapate nguvu na justification kwa wananchi ya kukaa mezani
Russia kuingia Kyiv ilikuwa ni ujinga wa karne wa kijeshi uliotokana na intelligence mbovu kwamba Wa-ukraine watawapokea kama wakombozi dhidi ya Zelenskyy na kwamba Zelenskyy atajisalimisha au kukimbia nchi, msafara wao wa vifaru ulivyoanza kumong'onyolewa na javelins ndipo wakaanza kukimbia kimbia kurudi kwao kwa miguu kama panya wakitekeleza vifaru.
 
Ikiwa Ukraine itaamua kusonga mbele, basi watasonga mbele hapo Kursk. Na hii ndio mbinu nzuri zaidi kwao ili kupunguza makali ya mashambulizi anayofanyiwa kwake.

Plan ya kuteka ardhi ya Russia ikifeli, yamkini watakuja na plan ya kupiga mabomu makali hapo Russia.

Kuna namna Ukraine anatafuta kumuadabisha Russia.
Namna ya kumuadabisha Russia ambayo Napoleon na Hitler walishindwa, sio?!
 
Russia kuingia Kyiv ilikuwa ni ujinga wa karne wa kijeshi uliotokana na intelligence mbovu kwamba Wa-ukraine watawapokea kama wakombozi dhidi ya Zelenskyy na kwamba Zelenskyy atajisalimisha au kukimbia nchi, msafara wao wa vifaru ulivyoanza kumong'onyolewa na javelins ndipo wakaanza kukimbia kimbia kurudi kwao kwa miguu kama panya wakitekeleza vifaru.

Hujui siasa wala siasa ya vita
 
Ukraine ana halalisha uvamizi wa Urusi katika mipaka yake.

Ukraine alipaswa kumfukuza Urusi katika mipaka yake na sio kuvamia mipaka ya Urusi kama Urusi alivyofanya kwake.

Sina hakika sana juu ya silaha hizo za maangamizi ila ninachoona ni Urusi kupata support zaidi ya kuingamiza Ukraine kupitia uvamizi huu.

Support ya ndani na ya nje kwa washirika wake na hata wasio washirika wake.

Urusi atasema najilinda dhidi ya uvamizi wa Ukraine atautumia udhaifu huu kuleta maafa sijajua ni kipi makamanda na majeshi ya Ukraine wanacho fikiri.
Kwa maneno rahisi Ukraine kaingia kwenye mtego wa kisheria maana kaingia ndani ya Urusi.
 
Putin haez fanya hivyo maana anajuwa sababu ya kuvamiwa hivyo ni kumchochea atumie silaha nzito ili Ukraine atumie midude yake pia ndani ya Urusi halaf wanancho waanze kuhoji umuhimu wa Putin kuendeleza vita inayowagharimu raia wake
Ukraine hana silaha ya kuisumbua Russia. Fikiria kama Ukraine ingekuwa na silaha inayoogopeka kama Iskander M.
 
Putin amepigiwa hesabu ya miaka 10 ijayo.

Kuna mwaka Putin atakuja kuondolewa na Warusi wenyewe sababu ya majnga yatakayo ikumba Rusia hasa uchumi
Mmeendelea kua wapiga ramli sasa au sio😀

Kwanini nato wasiende kumtoa mnabakia kua wapiga ramli poleni sana😀😀
 
Wakati wa Hitler Urusi ilipewa msaada na Marekani kupitia Lend-Lease act.
Nawakati huu wampe msaada ukraine ili russia atoke Ukraine au hawataki atoke

Pia wampe msaada german ili Russia aondoke ujerumani inayokaliwa na Russia
 
Watu hawaelewi, sijui wanafuatilia habari kutokea wapi make hata mainstream media wanasema Ukraine amefanya gamble ya kijinga sana, why utumie resources zako chache za muhimu kuvamia eneo ambao kwa namna yoyote hautaweza kulikalia hata kwa mwezi mmoja halafu unaacha kulinda maeneo yako mengi ambayo yanaelekea kuanguka?
Hizi akili kwanini tunashindwa kuzitumia vyema? Kama Ukraine hawezi shikilia hilo eneo kwa mwaka mzima, ulitegemea Russia angekaa zaidi ya miaka miwili bila kuidondosha serikali ya sasa ya Ukraine?

Hii vita imetupa matokeo mengi tofauti na matarajio yetu. Sidhani kama Ukraine hajakaa chini na washirika wake kabla ya kuchukua uamuzi wa kuingia Russia.
 
Ukraine ana halalisha uvamizi wa Urusi katika mipaka yake.

Ukraine alipaswa kumfukuza Urusi katika mipaka yake na sio kuvamia mipaka ya Urusi kama Urusi alivyofanya kwake.

Sina hakika sana juu ya silaha hizo za maangamizi ila ninachoona ni Urusi kupata support zaidi ya kuingamiza Ukraine kupitia uvamizi huu.

Support ya ndani na ya nje kwa washirika wake na hata wasio washirika wake.

Urusi atasema najilinda dhidi ya uvamizi wa Ukraine atautumia udhaifu huu kuleta maafa sijajua ni kipi makamanda na majeshi ya Ukraine wanacho fikiri.

wakati wa vita ni wakati wa kutafuta victory na kutafuta amani tumi kila nafas unayoipata dhidi ya adui
 
Back
Top Bottom