Napata mashaka juu ya ahadi ya Mito ya pombe mbinguni. Kama Pombe ni chukizo kwa Allah, ni kwanini Pombe iwepo mahali patakatifu?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Sijaja kwa kebehi wala maudhi ila nahitaji upembuzi juu ya hili la mito ya pombe mbinguni,

Quran 47:15 - Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya pombe yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa.

Binasfi hapa nimetathmini sana na nimepandwa na hasira, Kilicho haramu kikiruhusiwa mbinguni kuna utofauti upi gani na kula kitimoto, au nacho kimefichwa ili iwe surprise ya kushushia hizo pombe mbinguni ?

Naumiza kichwa na nashindwa kupata jibu, nijuavyo mimi pombe ilikaazwa kwasababu ina madhara mengi

  • Huchochea uzinzi (huwa inashuka chini)
  • Ugomvi - hupunguza uwezo wa kucontroll hasira.
  • Kutukana matusi - Mdomo utasema unachotaka
  • addiction / uraibu
  • imefanya wengi kufukuzwa kazini hadi mawaziri
  • Kuzima
  • Kutembea kwa kupepesuka bila balance
  • kujisaidia hadharani
  • Maumivu ya kichwa
  • Magonjwa ya figo, presha, kansa, n.k.

Tuajadiliane Hali hii ni vipi na inakuwaje sawa kwa Allah kuweka majaribu mbinguni?

 
Umefafanua scripture straight. Maandiko yanahitaji upembuzi yakinifu kabla hujawasilisha kwa watu
 
Mathayo 26:29
Ninawahakikishia sitokunywa Tena mvinyo wa mzabibu mpaka siku nitakapokunywa pamoja nanyi katika ufalme wa baba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…