Napata mashaka mno na CHADEMA, wamelegeza msimamo wao?

Napata mashaka mno na CHADEMA, wamelegeza msimamo wao?

Mbona Huwa nakuonaga uko smart Leo unaandika kama layman

Ni haramu Heche kutamka neno maridhiano
Anaridhiana na nani? CCM?
Yaani anadai Lissu akiachiwa ndo wafanye maridhiano?
Kwamba chadema Leo wamenasa kwenye mtego wanampigania Lissu sio Watanganyika waliouliwa?

Heche anaomba Lissu aachiwe na nani?

Lissu anaonewa, waliomshitak wathibitishe mashtaka yake wamhukumu kunyongwa Kwa uhaini, Dunia ijue

Tulikuwa tushawaweka CCM angle mbaya, Leo Heche anatamka maridhiano
Mkuu nisamehe leo kwa kutoniona smart kama siku nyingine, nimekusaidia tu. Cdm siku chache zilizopita hata mwezi bado, Heche alisema Lisu ailsipoachiwa wataitisha maandamano nchi nzima. Huenda umesahau hilo.

Sio Heche wala mwanacdm yoyote anataka Lisu asamehewe maana hana kosa. Ila sio sahihi Lisu kuendelea kukaa gerezani wakati waliomshikilia ameshawashinda kwenye kesi, wanachofanya ni kumkoa ikiwemo na kumzuia kupata matibabu. Ingekuwa Heche anataka Lisu aachiwe kwa msamaha hapo sawa, ila anataka aachiwe kwani hakuna kesi inaendelea.

Maridhiano kwako ni nini, ama unadhani Lisu akiachiwa ndio cdm watakubali maridhiano ya hadaa? Kama unaona Heche ametumia njia usiyoipenda, ww pia unaweza kutumia njia nyingine lengo ni Lisu asiendelee kukaa ndani wakati ameshashinda kesi, na kinachoendelea ni kumuumiza. Cha ajabu ww huna jitihada yoyote ya Lisu kukaa ndani, bali unataka ccm waogope. Kama hawajaogopa kuua, wataogopa Lisu kukaa ndani?
 
Lissu anatokaje gerezani ikiwa kesi yake haitafika mwisho na kutolewa hukumu.

Heche anataka nani amtoe mahabusu gerezani?
Rais anamsahe mfungwa na sio mahabusu
Mahakama viongozi wasiojielewa wanashangilia ndo hizo zinamuonea Lissu.
Hivi Heche anajielewa kweli?

Vijana wa Tanganyika wameuwa, yeye anaongelewa habari ya maridhiano na CCM?
Watanganyika tuna hasira mno vijana wetu zaidi ya 10,000 wameuwa kutetea haki halafu Heche anabwabwaja maridhiano?

Ili maridhiano yafanyike laZima waliouwa Watanganyika wawajibishwe, Samuya ajiuzulu, katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, na uchaguzi urudiwe.
Sawa mna hasira mno kutokana na ndugu jamaa na marafiki zaidi ya 10,000 kama mnavyodai, nyinyi kama nyinyi huko mtaani mmechukua hatua gani dhidi ya hilo.
Lissu aendelee kuteseka mahabusu kwa kigezo kuwa serikali ieleze wako wapi ndugu zenu! Lissu ni sadaka yenu? Nae ana familia bwana Acheni hizo mambo
 
Je, ukimkosoa kiongozi wa CHADEMA unakuwa CCM moja kwa moja? CHADEMA wamekuwa wakikosea katika mambo kadhaa, na ni wajibu wetu kuwakosoa ili chama kinachotegemewa na watu wengi kisije kikakengeuka kabla ya kufikia ukombozi wa kweli.
Umetoa ushirikiano gani kwao zaidi ya kubaki kama mlalamikaji wa mitandaoni?
 
Mimi nasema nchii hakuna mwanasiasa amepitia magumu kuliko Lissu na atakua mtu wa mwisho kuwapigia magoti ,Lisu amechagua haki na naamini hataweza kuwalamba matako CCM
 
Badilishana na Lissu yeye atoke, wewe uingie...simple. Eti umeona wasiwasi kwa sababu Heche kaenda Wasafi akiwa kafurahi, hii ni akili au matope?
 
Mkuu nisamehe leo kwa kutoniona smart kama siku nyingine, nimekusaidia tu. Cdm siku chache zilizopita hata mwezi bado, Heche alisema Lisu ailsipoachiwa wataitisha maandamano nchi nzima. Huenda umesahau hilo.

Sio Heche wala mwanacdm yoyote anataka Lisu asamehewe maana hana kosa. Ila sio sahihi Lisu kuendelea kukaa gerezani wakati waliomshikilia ameshawashinda kwenye kesi, wanachofanya ni kumkoa ikiwemo na kumzuia kupata matibabu. Ingekuwa Heche anataka Lisu aachiwe kwa msamaha hapo sawa, ila anataka aachiwe kwani hakuna kesi inaendelea.

Maridhiano kwako ni nini, ama unadhani Lisu akiachiwa ndio cdm watakubali maridhiano ya hadaa? Kama unaona Heche ametumia njia usiyoipenda, ww pia unaweza kutumia njia nyingine lengo ni Lisu asiendelee kukaa ndani wakati ameshashinda kesi, na kinachoendelea ni kumuumiza. Cha ajabu ww huna jitihada yoyote ya Lisu kukaa ndani, bali unataka ccm waogope. Kama hawajaogopa kuua, wataogopa Lisu kukaa ndani?
Najua wazi magumu anayopitia Lissu
Ila asitumie mtaji wa damu za Watanganyika kutoka na kuwa huru Kisiasa
Atoke kama anastahili na ahukumiwe kama anastahili

Watu wengi wamekufa, asitumie damu za ndugu zetu ili atoke eti kufanya maridhiano
 
Sawa mna hasira mno kutokana na ndugu jamaa na marafiki zaidi ya 10,000 kama mnavyodai, nyinyi kama nyinyi huko mtaani mmechukua hatua gani dhidi ya hilo.
Lissu aendelee kuteseka mahabusu kwa kigezo kuwa serikali ieleze wako wapi ndugu zenu! Lissu ni sadaka yenu? Nae ana familia bwana Acheni hizo mambo
Waliomshitaki Lissu wamtoe au wamhukumu
Sisi tunapinga kutumia damu Watanganyika waliokufa ili wamtoe afanye maridhiano
 
Mimi nasema nchii hakuna mwanasiasa amepitia magumu kuliko Lissu na atakua mtu wa mwisho kuwapigia magoti ,Lisu amechagua haki na naamini hataweza kuwalamba matako CCM
Kweli Lissu anapitia magumu na I feel sorry for him
Naona Heche ndo kapwaya
Kutamka ati wamtoe Lissu ili wafanye maridhiano
Yaani maelfu ya Watanganyika waliouliwa oktoba 9 ndo uwe mtaji wa kumtoa Lissu kufanya maridhiano
Kwamba Kigezo ni Lissu atoke ili kufanya maridhiano
 
Badilishana na Lissu yeye atoke, wewe uingie...simple. Eti umeona wasiwasi kwa sababu Heche kaenda Wasafi akiwa kafurahi, hii ni akili au matope?
Tatizo mnajifanyaga nyie ndo wanachadema kuliko wengine.

Usijipe ubora huo mkuu, hata Mimi ni mwanachadema

Napinga upumbavu wa Heche kutamka kwanza upuuzi wa maridhiano

Kuwa Lissu atoke ili afanye maridhiano damu za Watanganyika ndo uwe mtaji wa Kisiasa wa kumweka huru Lissu
 
Najua wazi magumu anayopitia Lissu
Ila asitumie mtaji wa damu za Watanganyika kutoka na kuwa huru Kisiasa
Atoke kama anastahili na ahukumiwe kama anastahili

Watu wengi wamekufa, asitumie damu za ndugu zetu ili atoke eti kufanya maridhiano
Hahitaji hayo maridhiano, angeyahitaji angeshatoka. Ww tuambie mchango wako ni upi ili yeye aachiwe au kesi iendelee, au mchango wako ni kutunza hiyo historia ya watu kuuwawa?
 
Hahitaji hayo maridhiano, angeyahitaji angeshatoka. Ww tuambie mchango wako ni upi ili yeye aachiwe au kesi iendelee, au mchango wako ni kutunza hiyo historia ya watu kuuwawa?
Mimi ni mwanachadema
Natumia platform ya chadema, siwezi kufanya personal
Ndo maana Chama kikikengeuka nakosoa Kwa ukali
 
Kwa ufahamu wangu japo mdogo naona chadema wameregeza kamba kwenye hoja na misimamo Yao

Kwadababu

1. Kushangilia ushindi fake wa kuruhusuwa kufanya siasa.
Naona mtandao viongozi wa Chadema wakifurahi mno.

Hivi hawa akina Heche wanaona ati mahakama imewatendea haki?😂

2. Media tour ya Heche pale Wasafi

Nilimuona Heche kwenye facial
expression akiwa na furaha na ahadi.

Niliona kama ipo programmed
Aliongea mambo kama layman kabisa.

Uso huongeza kuliko maneno

3. Heche anahamisisha Lissu kuachiwa. Hivi Heche hajui utaratibu wa mahakama kuwa kesi ilifika mahakamani laZima isikilizwe na ifike mwisho
Hukumu haijatoka, makamu anaomba Lissu aachiwe

4. Heche alikuwa anakubali maridhiano kiaina.
Hili lilinishtua kidogo

Tushaweka msimamo, maridhiano hadi, waliouwa wajulikane na wawajibishwe, Samuya ajiuzulu na uchaguzi urudiwe
Heche amesahau yote haya saiv anajichekesha anaongelea usenge wa maridhiano redioni

5 Nilishtuka kuona magazeti na media zinatangaza habari za chadema Kwa bashasha
Hii ilinishtua kidogo

6 Ombi la Heche litakubaliwa na Lissu ataachiwa

7 Samuya hatajiuzulu na uchaguzi hautaridiwa Kwa kifupi hapa Kuna changa la macho

8 Tume itatoa majibu ya kinafiki kuikandia serikali kiaina na kuitaka serikali imuachie Lissu na Serikali itakeleza hilo agizo la tume
Wana jeuri ya kukaza?
 
Mbona Huwa nakuonaga uko smart Leo unaandika kama layman

Ni haramu Heche kutamka neno maridhiano
Anaridhiana na nani? CCM?
Yaani anadai Lissu akiachiwa ndo wafanye maridhiano?
Kwamba chadema Leo wamenasa kwenye mtego wanampigania Lissu sio Watanganyika waliouliwa?

Heche anaomba Lissu aachiwe na nani?

Lissu anaonewa, waliomshitak wathibitishe mashtaka yake wamhukumu kunyongwa Kwa uhaini, Dunia ijue

Tulikuwa tushawaweka CCM angle mbaya, Leo Heche anatamka maridhiano
Ni michango ya maoni kama haya ndiyo yanayovuruga kabisa hata akili za watu wanaoonyesha kuwa na utambuzi mzuri wa maswala.

Hebu tazama maneno kama haya uliyoandika kwenye mstari huu hapa chini, na utafakari kama ni kweli ulikuwa na maana halisi ya maneno hayo:
Lissu anaonewa, waliomshitak wathibitishe mashtaka yake wamhukumu kunyongwa Kwa uhaini, Dunia ijue

Samia ameua maelfu ya waTanzania, na dunia imejuwa... Ni kipi kinachokupa ujasiri wa kusema kutakuwa na hali tofauti Lissu akihukumiwa kunyongwa na akanyongwa hasa; pamoja na kwamba itajulikana kunyongwa kwake siyo kwa haki?

Niseme tu wazi hapa.
Tangu nilipoanza kusoma mada yako hii nimekuwa natatizwa sana na haya unayoeleza laeo.
Huko mwanzo nilijitahidi kupoza, lakini naona unaendelea kukazia yale yale.

Samia ni mtu mwovu, ni mhalifu. Huwezi kumtilia mashaka kwamba atasita kuendelea kufanya uovu wake huo wakati angali yupo madarakani kwa mabavu.

Hayo unayosema wewe ya Heche kutamka "maridhiano"; umesikia akisema anaridhiana na nani na kwa masharti gani?

Kwa nini maneno "Mazungumzo na maridhiano" yawe ni maneno ya sumu; kwa vile yametamkwa na hao waovu? Wao ndio pekee wanaoweza kuyatumia maneno hayo?
WaTanzania kwa ujumla wetu hatuwezi kuwa na mazungumzo na tukaridhiana nje ya mfumo wa hao waovu?
 
Back
Top Bottom