Napata mashaka mno na CHADEMA, wamelegeza msimamo wao?

Napata mashaka mno na CHADEMA, wamelegeza msimamo wao?

Je, ukimkosoa kiongozi wa CHADEMA unakuwa CCM moja kwa moja? CHADEMA wamekuwa wakikosea katika mambo kadhaa, na ni wajibu wetu kuwakosoa ili chama kinachotegemewa na watu wengi kisije kikakengeuka kabla ya kufikia ukombozi wa kweli.
Sasa kosa liko.wapi hapo kwa Lissu kusema aachiwe huru na kesi zote za Chadema zifutwe ndiyo wanaweza kukaa mezani? Wewe umeleta mada hii kwa nia ovu kawaambie waliokutuma kuwa hatudanganyiki kiboya hivyo.
 
Nijuavyo mimi ni kwamba maridhiano na mazungumzo ni vitu viwili tofauti !

Mnaweza mkaingia kwenye mazungumzo lakini maridhiano yasipatikane katika hayo mazungumzo !

Lakini pia ndani ya mazungumzo yanaweza yakapatikana baadhi ya maridhiano !
Na mazungumzo yakaendelea kufanyika ili kutafuta maridhiano kamili yaweze kupatikana !
Ccm na Chadema wamekaa mara ngapi kwenye maridhiano, nini kimepatikana. Kabla ya uchaguzi Ccm walikuwa wanasema waziwazi watafanya maridhiano baada ya uchaguzi, kwa hiyo walijua wataiba kura, wataua halafu watafanya maridhiano.
Labda nikukumbushe kabla ya uchaguzi kulikuwa na mazungumzo kati ya ccm na chadema lakini yalivunjika baada ya Ccm kumpa kesi ya uhaini Lissu.
Hao watu hawataki maridhiano ila wanavuta muda waendelee kutawala.
 
Kwa ufahamu wangu japo mdogo naona chadema wameregeza kamba kwenye hoja na misimamo Yao

Kwadababu

1. Kushangilia ushindi fake wa kuruhusuwa kufanya siasa.
Naona mtandao viongozi wa Chadema wakifurahi mno.

Hivi hawa akina Heche wanaona ati mahakama imewatendea haki?😂

2. Media tour ya Heche pale Wasafi

Nilimuona Heche kwenye facial
expression akiwa na furaha na ahadi.

Niliona kama ipo programmed
Aliongea mambo kama layman kabisa.

Uso huongeza kuliko maneno

3. Heche anahamisisha Lissu kuachiwa. Hivi Heche hajui utaratibu wa mahakama kuwa kesi ilifika mahakamani laZima isikilizwe na ifike mwisho
Hukumu haijatoka, makamu anaomba Lissu aachiwe

4. Heche alikuwa anakubali maridhiano kiaina.
Hili lilinishtua kidogo

Tushaweka msimamo, maridhiano hadi, waliouwa wajulikane na wawajibishwe, Samuya ajiuzulu na uchaguzi urudiwe
Heche amesahau yote haya saiv anajichekesha anaongelea usenge wa maridhiano redioni

5 Nilishtuka kuona magazeti na media zinatangaza habari za chadema Kwa bashasha
Hii ilinishtua kidogo

6 Ombi la Heche litakubaliwa na Lissu ataachiwa

7 Samuya hatajiuzulu na uchaguzi hautaridiwa Kwa kifupi hapa Kuna changa la macho

8 Tume itatoa majibu ya kinafiki kuikandia serikali kiaina na kuitaka serikali imuachie Lissu na Serikali itakeleza hilo agizo la tume
Mi naona wanatumia fursa ya "maridhiano"ili jamaa aachiliw huru alafu serikali iliingia kingi jamaa aliachiliwa ageuzie gia hewani aliqmzishe tena.
Yaani kwa kifupi jamaa sio wa kumwwkea dhamana anakugeuka mapema tuu
 
Unawashauri nini kifanyike??? Maana uhalisia lazima maisha yaendelee! Na chadema hata wakiweka mgomo haisaidii bado! Nchi lazima iendelee na mama Samia ataendelea kuwa Rais! Mimi nafikiri njia rahisi ya kutoka kwenye mkwamo huu ni maridhiano nothing else
Hivi ni leo wameanza kuzungumza, unakumbuka baada ya Mbowe kuachiwa break ya kwanza ilikuwa ikulu na baada ya hapo wakafunguliwa kufanya mkutano wakati ile ilikuwa haki yao, wakapewa ruzuku iliyokuwa imezuiwa wakati ni haki yao lakini muda mfupi Tundu Lissu aliwatuhumu ccm kuvunja makubaliano kwa hiyo unahisi maridhiano ya sasa hivi yatabadilisha chochote.
 
Unashauri nini kifanyike?
Chadema wafanye nini?
 
Hivi ni leo wameanza kuzungumza, unakumbuka baada ya Mbowe kuachiwa break ya kwanza ilikuwa ikulu na baada ya hapo wakafunguliwa kufanya mkutano wakati ile ilikuwa haki yao, wakapewa ruzuku iliyokuwa imezuiwa wakati ni haki yao lakini muda mfupi Tundu Lissu aliwatuhumu ccm kuvunja makubaliano kwa hiyo unahisi maridhiano ya sasa hivi yatabadilisha chochote.
Ni kweli CCM hawaaminiki lakini kwa hali iliyopo sasa hivi wewe unaweza kushauri nini kifanyike? Hawa washenzi walitumia mabavu ya majeshi yao kujisimika madarakani na Chadema wao hawana majeshi sasa unafikiri nini kifanyike?
 
Ccm wataondoka muda ukifika, sasa hivi wanatambua fika hawapo kwa matakwa ya wananchi ndio maana wanaajili makada wao kwenye vyombo vya usalama.
Tatizo kubwa wananchi walikuwa hawajapata elimu ya kutosha lakini kwa sasa wananchi wengi wanajua ubaya wa ccm dawa ni kutoshirikiana nao kitendo cha kukutana nao ina maana unahalalisha haramu kuwa halali.
 
Ni kweli CCM hawaaminiki lakini kwa hali iliyopo sasa hivi wewe unaweza kushauri nini kifanyike? Hawa washenzi walitumia mabavu ya majeshi yao kujisimika madarakani na Chadema wao hawana majeshi sasa unafikiri nini kifanyike?
Hawa CCM tumeshawapa pressure na kisukari yaani hawatawali Kwa raha

Yaani kusema wamtoe Lissu ili kufanya maridhiano ni kuwarahisishia uhalali wa kukaa madarakani
Na Lissu watamwachia tu ili wafanye maridhiano

CCM anahitaji maridhiano kuliko chochote saiv

Chadema na Heche wameshindwa kukaza
CCM wana pressure mno kukaa na Lissu huko gerezani, Kuna pressure ya kimataifa
 
Ndio maana haifai hata kidogo kwa UMMA kuweka dhamana ya Ustawi wake kwa Chama Cha Siasa.
 
Ubongo wa bata 🦆
Yaani mfanyie dhulumat Lissu halafu mtake chadema waombe huruma

Kama ni mhaini mpeleke mahakamani apate haki yake huko

Hii ni nchi ya utawala wa sheria
Haki gani unayoizungumzia wewe utakuwa ni moja ya watu wanaotaka lisu aendelee kukaa mahabusu maisha yake yote hapa duniani kwa maslahi yako binafsi
 
Ccm na Chadema wamekaa mara ngapi kwenye maridhiano, nini kimepatikana. Kabla ya uchaguzi Ccm walikuwa wanasema waziwazi watafanya maridhiano baada ya uchaguzi, kwa hiyo walijua wataiba kura, wataua halafu watafanya maridhiano.
Labda nikukumbushe kabla ya uchaguzi kulikuwa na mazungumzo kati ya ccm na chadema lakini yalivunjika baada ya Ccm kumpa kesi ya uhaini Lissu.
Hao watu hawataki maridhiano ila wanavuta muda waendelee kutawala.
Kila marefu hayakosi kuwa na ncha !
Huenda this time watakuwa serious na mazungumzo! Who knows ?!
Ndio maana mazungumzo huwa ndio njia bora pekee katika kupata suluhisho katika migogoro mingi hapa Duniani !
 
Kweli
Hakuna anayependa Lissu akae gerezani

Lissu atoke kisheria na sio Heche kuomba huruma
Kutoka kisheria kuna njia mbili:
1. DPP kufuta kesi kwa kutumia kifungu cha 91
2. Kesi kuendelea mahakamani na yeye kushinda.
 
Unasoma upotoshaji wa wanaccm huku mitandaoni, hadi unatumia upotoshaji huo kama sehemu ya mashaka yako. Lisu hajaombewa kutoka gerezani, bali anatakiwa aachiwe maana waliomfungulia kesi wameshindwa kuendelea na kesi. Ingekuwa kesi inaendelea kisha Heche akataka kesi isimame Lisu aachiwe, hapo shaka yako ingekuwa na msingi.

Lisu ameweka masharti saba, nadhani huyajui. Hakuna popote Lisu anataka akae gerezani ili ww uamini yeye ni mpiganaji, siku zote kajitetea kwenye kesi yake hadi amewashinda, ila kwa sasa anakomolewa. Je unataka aendelee kukaa kimya ama wanacdm wakae kimya hadi serekali iamue kuendelea na kesi? Ni hivi juzi Heche kasema Lisu asipotendewa haki, cdm watafanya maandamano kutaka aachiwe. Je hilo hukusikia?
Chadema ni wajanja sana hawawez kwenda kinyume na wananchi masuala ya kutekwa na mauaji ya oct 2025 bado ni vidonda vikubwa kwa wananchi nje ys mipaka ya CDM.
 
Back
Top Bottom