Napata mashaka mno na CHADEMA, wamelegeza msimamo wao?

Mkuu nisamehe leo kwa kutoniona smart kama siku nyingine, nimekusaidia tu. Cdm siku chache zilizopita hata mwezi bado, Heche alisema Lisu ailsipoachiwa wataitisha maandamano nchi nzima. Huenda umesahau hilo.

Sio Heche wala mwanacdm yoyote anataka Lisu asamehewe maana hana kosa. Ila sio sahihi Lisu kuendelea kukaa gerezani wakati waliomshikilia ameshawashinda kwenye kesi, wanachofanya ni kumkoa ikiwemo na kumzuia kupata matibabu. Ingekuwa Heche anataka Lisu aachiwe kwa msamaha hapo sawa, ila anataka aachiwe kwani hakuna kesi inaendelea.

Maridhiano kwako ni nini, ama unadhani Lisu akiachiwa ndio cdm watakubali maridhiano ya hadaa? Kama unaona Heche ametumia njia usiyoipenda, ww pia unaweza kutumia njia nyingine lengo ni Lisu asiendelee kukaa ndani wakati ameshashinda kesi, na kinachoendelea ni kumuumiza. Cha ajabu ww huna jitihada yoyote ya Lisu kukaa ndani, bali unataka ccm waogope. Kama hawajaogopa kuua, wataogopa Lisu kukaa ndani?
 
Sawa mna hasira mno kutokana na ndugu jamaa na marafiki zaidi ya 10,000 kama mnavyodai, nyinyi kama nyinyi huko mtaani mmechukua hatua gani dhidi ya hilo.
Lissu aendelee kuteseka mahabusu kwa kigezo kuwa serikali ieleze wako wapi ndugu zenu! Lissu ni sadaka yenu? Nae ana familia bwana Acheni hizo mambo
 
Je, ukimkosoa kiongozi wa CHADEMA unakuwa CCM moja kwa moja? CHADEMA wamekuwa wakikosea katika mambo kadhaa, na ni wajibu wetu kuwakosoa ili chama kinachotegemewa na watu wengi kisije kikakengeuka kabla ya kufikia ukombozi wa kweli.
Umetoa ushirikiano gani kwao zaidi ya kubaki kama mlalamikaji wa mitandaoni?
 
Mimi nasema nchii hakuna mwanasiasa amepitia magumu kuliko Lissu na atakua mtu wa mwisho kuwapigia magoti ,Lisu amechagua haki na naamini hataweza kuwalamba matako CCM
 
Badilishana na Lissu yeye atoke, wewe uingie...simple. Eti umeona wasiwasi kwa sababu Heche kaenda Wasafi akiwa kafurahi, hii ni akili au matope?
 
Najua wazi magumu anayopitia Lissu
Ila asitumie mtaji wa damu za Watanganyika kutoka na kuwa huru Kisiasa
Atoke kama anastahili na ahukumiwe kama anastahili

Watu wengi wamekufa, asitumie damu za ndugu zetu ili atoke eti kufanya maridhiano
 
Waliomshitaki Lissu wamtoe au wamhukumu
Sisi tunapinga kutumia damu Watanganyika waliokufa ili wamtoe afanye maridhiano
 
Mimi nasema nchii hakuna mwanasiasa amepitia magumu kuliko Lissu na atakua mtu wa mwisho kuwapigia magoti ,Lisu amechagua haki na naamini hataweza kuwalamba matako CCM
Kweli Lissu anapitia magumu na I feel sorry for him
Naona Heche ndo kapwaya
Kutamka ati wamtoe Lissu ili wafanye maridhiano
Yaani maelfu ya Watanganyika waliouliwa oktoba 9 ndo uwe mtaji wa kumtoa Lissu kufanya maridhiano
Kwamba Kigezo ni Lissu atoke ili kufanya maridhiano
 
Badilishana na Lissu yeye atoke, wewe uingie...simple. Eti umeona wasiwasi kwa sababu Heche kaenda Wasafi akiwa kafurahi, hii ni akili au matope?
Tatizo mnajifanyaga nyie ndo wanachadema kuliko wengine.

Usijipe ubora huo mkuu, hata Mimi ni mwanachadema

Napinga upumbavu wa Heche kutamka kwanza upuuzi wa maridhiano

Kuwa Lissu atoke ili afanye maridhiano damu za Watanganyika ndo uwe mtaji wa Kisiasa wa kumweka huru Lissu
 
Najua wazi magumu anayopitia Lissu
Ila asitumie mtaji wa damu za Watanganyika kutoka na kuwa huru Kisiasa
Atoke kama anastahili na ahukumiwe kama anastahili

Watu wengi wamekufa, asitumie damu za ndugu zetu ili atoke eti kufanya maridhiano
Hahitaji hayo maridhiano, angeyahitaji angeshatoka. Ww tuambie mchango wako ni upi ili yeye aachiwe au kesi iendelee, au mchango wako ni kutunza hiyo historia ya watu kuuwawa?
 
Hahitaji hayo maridhiano, angeyahitaji angeshatoka. Ww tuambie mchango wako ni upi ili yeye aachiwe au kesi iendelee, au mchango wako ni kutunza hiyo historia ya watu kuuwawa?
Mimi ni mwanachadema
Natumia platform ya chadema, siwezi kufanya personal
Ndo maana Chama kikikengeuka nakosoa Kwa ukali
 
Wana jeuri ya kukaza?
 
Ni michango ya maoni kama haya ndiyo yanayovuruga kabisa hata akili za watu wanaoonyesha kuwa na utambuzi mzuri wa maswala.

Hebu tazama maneno kama haya uliyoandika kwenye mstari huu hapa chini, na utafakari kama ni kweli ulikuwa na maana halisi ya maneno hayo:
Lissu anaonewa, waliomshitak wathibitishe mashtaka yake wamhukumu kunyongwa Kwa uhaini, Dunia ijue

Samia ameua maelfu ya waTanzania, na dunia imejuwa... Ni kipi kinachokupa ujasiri wa kusema kutakuwa na hali tofauti Lissu akihukumiwa kunyongwa na akanyongwa hasa; pamoja na kwamba itajulikana kunyongwa kwake siyo kwa haki?

Niseme tu wazi hapa.
Tangu nilipoanza kusoma mada yako hii nimekuwa natatizwa sana na haya unayoeleza laeo.
Huko mwanzo nilijitahidi kupoza, lakini naona unaendelea kukazia yale yale.

Samia ni mtu mwovu, ni mhalifu. Huwezi kumtilia mashaka kwamba atasita kuendelea kufanya uovu wake huo wakati angali yupo madarakani kwa mabavu.

Hayo unayosema wewe ya Heche kutamka "maridhiano"; umesikia akisema anaridhiana na nani na kwa masharti gani?

Kwa nini maneno "Mazungumzo na maridhiano" yawe ni maneno ya sumu; kwa vile yametamkwa na hao waovu? Wao ndio pekee wanaoweza kuyatumia maneno hayo?
WaTanzania kwa ujumla wetu hatuwezi kuwa na mazungumzo na tukaridhiana nje ya mfumo wa hao waovu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…