Napata raha sana kuona mashabiki wa Simba na Man U wakiwa hawana raha

Napata raha sana kuona mashabiki wa Simba na Man U wakiwa hawana raha

Yaani katika maisha yangu naweza kupata hela nyingi tu na nikaona kawaida yaani. Ila Mashabiki wa Simba na Man wakiishi kwa stress napata faraja sana na naona nina kila kitu katika maisha.

Hasa hasa hawa watu wa Msimbazi wanapoanza kunyosheana vidole, kukamatana uchawi, kufukuzana na kusutana furaha yangu huzidi.

Nimekuwa addicted kufatilia mapovu ya aina zote youtube, JF ndo usiseme siwezi kupitisha dk 2 sijaingia jukwaa la Michezo kuangalia current povu la wanasimba.

Waza unavyowaza ila kila mtu ana namna yake ya kuburudika.

Jana nimeangalia povu la wanaSimba wakiimba hawamtaki Mangungu siafikiani nao ila nilifurahi tu kuona wanavyoumia na kuteseka huku nyuso zao zikiwa zimekunjamana. Kuna shabiki nilikuona analia kisa Simba kutoa sare na Namungo hakika nilifarijika sana mpaka nikamsamehe kodi ya miezi 2 mpangaji wangu.

Mashabiki wa Simba walichangishwa hela ya kujenga uwanja mpka sasa hela zao hazieleweki zimefanya kazi gani.Kitendo cha hela zao kuliwa kinanifurahisha sana maana wanaumia.Natamani aliyekula hizo hela nimpe zawadi.

Ufanisi wangu katika kufanya kazi za Jamhuri umeongeza mara dufu kwa siku hizi chache. Hakika Simba wameineemesha Serikali🤣🤣

Sinywi pombe wala aina yeyote ya anasa furaha yangu ndo hiyo. Kipindi Simba inafanya vizuri niliteseka sana.

Haka kamsemo ka TABULELE nakapenda sana japo sijui maana yake maana kanawakera, kuwahuzunisha sana Mashabiki wa Simba huku kakiniacha na tabasamu pana usoni.

TABULELEE

Waheed.
Hapo kwa man utd unazingua
 
Mkuu usichukulie mambo serious hivyo na gazeti lako lisilo na aya.

Watu tuna wapenzi, wazazi na marafiki wanazipenda hizo timu haina maana tunapenda kweli kuona wanavyoteseka.
Ni utani tu, nothing serious.
Pole
Kono la nyani (FIVE O'CLOCK) limewaumiza wengi.
Hajui kama huu mwengine ni utani tu wa mpira.
 
kuna ndugu yangu mmoja hapa ni shabiki wa simba na mwanitesa, ndani ya siku mbili tatu hizi amekonda ghafla. kimebaki kichwa tu. kichwa kikubwa mwili mdogo kama siafu. basi nikimuona naaimba 'sio leo, toka zamani, mnyama hana amani"....
 
kuna ndugu yangu mmoja hapa ni shabiki wa simba na mwanitesa, ndani ya siku mbili tatu hizi amekonda ghafla. kimebaki kichwa tu. kichwa kikubwa mwili mdogo kama siafu. basi nikimuona naaimba 'sio leo, toka zamani, mnyama hana amani"....
kichwa kikubwa mwili mdogo kama siafu[emoji23][emoji23][emoji113]
 
kuna ndugu yangu mmoja hapa ni shabiki wa simba na mwanitesa, ndani ya siku mbili tatu hizi amekonda ghafla. kimebaki kichwa tu. kichwa kikubwa mwili mdogo kama siafu. basi nikimuona naaimba 'sio leo, toka zamani, mnyama hana amani
Safi sana😊😊😊🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom