Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Napata shaka ndani ya CCM kinaratibu mipango kiufundi sana kumkwamisha Mama 2025 ikiwa anatahitaji tena kugombea. Hili jambo tunaweza kuona kama masihara lakini tutaelewana tu mbele ya safari. Wanataka kumchonganisha Mama na wananchi na jumuiya za kimataifa ili kufikia 2025 waseme ameshindwa kutuvusha, ili waseme tunahitaji mwanaume asimame.
Haiwezekani unatuma vyombo vya usalama wanaenda usiku kukamata kiongozi wa chama kikubwa cha upinzani, chama ambacho ndio mbadala wa chama tawala kwa sababu tu anataka kufanya kongamano la kujadili katiba mpya kitu ambacho hakuna kosa lolote kisheria alilofanya. Kitu hiki kimeripotiwa media zote za kimataifa na sasa inafahamika kua Tanzania hakuna utulivu wa kisiasa (Political instability). Mwekezaji gani ataamini kua Tanzania mazingira yamebadilika kama vyombo vya usalama vinakamata mtu bila kosa lolote? Mambo ya kubambikiziana kesi kweli yamekwisha? Ni mfadhili gani alete misaada yake eneo ambalo sasa litssomeka kuna migogoro ya kikatiba?
Hili kundi linaelewa madhara makubwa ya kumkamata Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani, hiki chama kina mahusiano na Democratic parties mbali mbali duniani tena vyenye dola katika mataifa makubwa makubwa. Kufanya hivi kumeichafua sana taswira ya nchi na ndio hapa Mama atakwamishwa makusudi.
Bado kuna suala la tozo za miamala, ukiliangalia kwa makini utaona ni kama lineratibiwa kiufundi sana kumchonganisha Mama na wananchi ingawa ameshtuka mapema. Hii haijawahi kutokea wananchi wanapandishiwa Tozo maradufu zaidi kwenye huduma wanayotegemea kwa kiasi kikubwa, halafu bado waziri anatoka hadharani na kuwatukana wananchi wanaolalamika tena anaongea kwa kibri bila kupima madhara yake. Huyu kiongozi unaweza kuhisi ni kama alitumwa kumharibia Mama makusudi.
Naweza kuandika haya na yakachukuliwa poa lakini tutajuana mbele ya safari. Kinachofuata ni kuibuka kwa migogoro ndani ya CCM yenyewe muda si mrefu. Hali hii itamkatisha tamaa sana Mama.