Napata shaka, kuna kikundi ndani ya CCM kinaratibu kumkwamisha Rais Samia 2025

Napata shaka, kuna kikundi ndani ya CCM kinaratibu kumkwamisha Rais Samia 2025

Team Jiwe ndani ya CCM ishaanza kumharibia mama nje na ndani ya Tanzania...tangu juzi jana na leo Maza ana trend kimataifa vibaya mno.
 
Lipo wazi,mama bora liende nadhani hana mpango wa kuendelea kuendesha gari.Nakubali kauli ya Mwalimu,"mtu mwenye akili timamu Katu hawezi tamani kwenda ikulu" true tabu yote ya nn,maisha si zaidi ya kula na kunywa vingine ni kuukimbiza upepo tu.
Stress za nini,mizigo ya nn,life is too short.
 
Aisee binafsi kuna maono nimeyapata Mama kasusa haoni maana ya kuwa rais vile anaendeshwa kama gari bovu na wale wanaodhani taifa hili ni mali yao huku mambo yaki haribika lawama zinamrudia yeye.
Mama hawezi mapema keshachemka, tulimwambia huwezi endesha gari bovu kisa we ni dereva mpya akusikia.
Ajachelewa aingize gari services piga chini vitu vyote chakavu weka vyako vipya piga engine overhaul.
Hawezi fanikiwa hali kuna toxin kibao za mwendakombo.
Wengi walioteuliwa sio kwa weledi bali ni baada ya kuimba Sana kwaya na kuisujudia Sanamu,sasa watu wenye mentality hizi za kufokewa,kusimamiwa wasio na semina elekezi huwezi panda nao kitonga.
Labda tu nae kaamua kuanza kuachia mapema.Hivi unadandanywa vipi eti kodi za uzalendo dabo taxation haipo sehemu yeyeto duniani tozo za aina.
Watu wanaokufa kwa kukosa sh 500 ya panadol au kosa hata sh 400 ya daladala sababu ya mifumo mibovu ya uzalishaji unaweza vipi watoza kodi za ajabu hivyo.
 
Prof Kaboko,

Naona kitu ambacho ama hukioni au unajifanya hukioni.

Freeman Mbowe
alimsonya Rais Samia hadharani na kuazimia kuangusha serikali kwa njia ya makongamano, mikutano ya hadhara na maandamano.

Kwa ufupi, Mbowe alitangaza nia ya kufanya uhaini, pure and simple.

Hauzifahamu kanuni za kuwashughulikia watu wenye dhamira ya kufanya uhaini?

Wewe ungekuwa mkuu wa serikali usingezitumia?

We have to call a spade not a spoon.
Mbowe anataka kuivuruga nchi maana kachukua chake kwa mabeberu,Mara ashauri chanjo iwe kwa lazima anajua rais akifuata ushauri wake atakuwa amemchonganisha na wananchi.

Analazimisha kufanya vurugu ili aangaliwe tu kuonyesha rais ni dhaifu,na akiguswa waliomtuma wanaikoromea nchi.
Maadam mama ni rais wa Watanzania aangaliwe maslahi ya watu wake.Hawa mabeberu leo watakuambia mwachie Mbowe,kesho uukubali ushoga,hawezi kuwaridhisha.
 
Umenadika vizuri, isipikuwa mwishoni. Achana na spinning kwa kutumia habari sensational kama vile ushoga.

Tuongelee hard issues. Hotuba ya Mbowe ya Mwanza ni tangazo la kuipindua serikali.

Ndio maana magazeti yoye kesho yake yaliipiga kisogo, isipokuwa gazeti la Raia Mwema linalotumiwa kama mdomo wa Team Mbowe.

Katiba mpya ni muhimu. Lakini, kwa mujibu wa mipango ya serikali sio ajenda yenye kipaumbele cha kwanza, hata Mbowe anajua hivyo. Lakini sasa anataka kuulaghai umma uamini vinginevyo.

Dinsinformation ni kosa kisheria. Hata hao unaowaita mabeberu wanafahamu ukweli huu.

Kwa hiyo, hoja za kuwajibu zipo.

Jana nimeona bang reporting kwenye magazeti mbalimbali ya kimataifa. Meseji ni ile ile kwa kuwa waandishi ni wale wale.

Hakuna sehemu waliandika kauli za Mbowe kuazimia kuipindua serikali. That is bias. Na hao unaowaita mabeberu wanaelewa vema hoja hii ikijengwa vema.

Hata hivyo, simfahamu vizuri Waziri Mula Mula, ili kuwa na uhakika kama anaweza kudadavua mambo haya kimantiki.

Team Mbowe wanao wataalam wa propaganda waliobobea. Baadhi ni Maaskofu, wengine ni wanafalsafa.

Kwa hiyo, kunahitajika anti-Team Mbowe yenye weledi mkubwa pia kujibu mapigo na kutetea ukweli.

Kwa sasa naishia hapa, lakini sikubaliani na disinformation inayofanywa na Team Mbowe.
 
Prof Kaboko,

Naona kitu ambacho ama hukioni au unajifanya hukioni.

Freeman Mbowe alimsonya Rais Samia hadharani na kuazimia kuangusha serikali kwa njia ya makongamano, mikutano ya hadhara na maandamano.

Kwa ufupi, Mbowe alitangaza nia ya kufanya uhaini, pure and simple.

Hauzifahamu kanuni za kuwashughulikia watu wenye dhamira ya kufanya uhaini?

Wewe ungekuwa mkuu wa serikali usingezitumia?

We have to call a spade not a spoon.
Hongera zako kwa kuwa sehemu ya kufurahia na kushabikia uovu ila siku usirudi hapa na kutuambia shakira yako ina kusuta.Hata pole hatutakupa.
 
Freeman Mbowe alimsonya Rais Samia hadharani na kuazimia kuangusha serikali kwa njia ya makongamano, mikutano ya hadhara na maandamano..
Kufanya makongamano, mikutano na maandamano ni haki ya kikatiba ya kila raia wa JMT na anayepanga kufanya hivyo hawezi kuwa branded eti ni Mhaini

Rais aliyeapa kuilinda Katiba ya Nchi hawezi kuogopa mikutano. Hoja jizibiwe kwa hoja na sio mitutu ya bunduki
 
Hongera zako kwa kuwa sehemu ya kufurahia na kushabikia uovu ila siku usirudi hapa na kutuambia shakira yako ina kusuta.Hata pole hatutakupa.
Hakuna uovu mkubwa kama kusigina hadhi ya ubinadamu kwa njia ya disinformation. Hii ndio sababu inanifanya nipinge hayo yanayoendelea huko kwenye Team Mbowe. Huwezi kumwambia mwenzio atoe kibanzi jichoni wakati kwako kuna boriti.
 
Kufanya makongamano, mikutano na maandamano ni haki ya kikatiba ya kila raia wa JMT anayepanga kufanya hivyo hawezi kuwa branded eti ni Mhaini

Rais aliyeapa kuilinda Katiba ya Nchi hawezi kuogopa mikutano. Hija jizibiwe kwa hoja na sio mitutu ya bunduki
Malizia hivi: "Kufanya makongamano, mikutano na maandamano ni haki ya kikatiba" ambayo ni double edged sword. Inaweza kutumika kama silaha ya kuangusha serikali au vinginevyo. Mbowe amesema anataka kuitumia kama mbinu ya kulifikisha Taifa kwenye "TIPPING POINT". Mpaka hapo bado hujaelewa dhamira yake kuwa ni kuangusha serikali kimabavu?
 
Hakuna uovu mkubwa kama kusigina hadhi ya ubinadamu kwa njia ya disinformation. Hii ndio sababu inanifanya nipinge hayo yanayoendelea huko kwenye Team Mbowe. Huwezi kumwambia mwenzio atoe kibanzi jichoni wakati kwako kuna boriti.
Uzuri jamvi hili hutunza kila kitu,nakutakia kila la kheri.
 
Bambika na la uhujumu uchumi pamoja na utakatishaji fweza kwa uchache.
Hayo safari hii hakuna kwa upande wa Mwanza. Yako mawili:

  • Mosi, kosa la kutumia offinabus language dhidi ya Rais (kumsonya hadharani) kinyume cha penal code
  • Pili, kutangaza dhamira ya kuiangusha serikali halali kinyume cha Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa ya 1996 kama ikisomwa pamoja na Katiba halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom