Napata Wasiwasi Sana Na Uelekeo Wa "DiamondPlatnumz"

Hio shughuli ya producer manecky, diamond nje ya manecky hamna lolote la maana alilofanya zaidi ya kutoa nyimbo mbovu kimapigo na kimashairi.
Refer to: Ukimwona, Mawazo, Mbagala, Nitarejea, Nenda Kamwambie n.k
True kabisa, baada ya kuachana na Manecky, ile ladha tamu ya mziki wake imeshuka kwa kiwango cha juu,
Naomba aufanyie kazi ushauri wa wadau maana mimi kama mimi ameshanikosa kwa sasa nabaki kusikiliza zake za zamani tu.
 
Mwenzenu alishasema hizo nyimbo za kulia lia za ndani sio za kimataifa. Nyie pendeni za kulia lia huko nje wanapenda za viduku
 
Mwenzenu alishasema hizo nyimbo za kulia lia za ndani sio za kimataifa. Nyie pendeni za kulia lia huko nje wanapenda za viduku
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji85]
 
Diamond prod. Manecky ndio anaemuwezea tu. Beats nzuri zisizo na kelele plus mashairi ya modi ya kulalamika mle ndio vinakonga nyoyo. Toka aache kufanya kazi na manecky nyimbo nzuri zilizofata ni kesho,nata kulewa and maybe nana!
Yah umeongea kweli yani diamond anavyolalamika akikutana na beat za manecky ndiyo tunapata ukimuona...
 
Na mimi nakubariana na mengi uliyosema lakini unasahau kuwa mziki ni biashara na kijana kaweza kufanya hilo.
Mziki sio kazi ya kutoa msaada ama shukurani eti akapige show kwa ela ndogo kisa kuwafurahisha watu.
I am sure akipewa ela anayoitaka kokote show atafanya hata hao unaosema wasanii wa marekani kaulize wakifanya show ya fiesta wanabeba pesa kiasi gani...
Nakumbuka alikuwa barozi wa vodacom wakati fiesta inadhaminiwa na tigo na hilo alishalisemea kuwa mkataba wake hauruhusu...
 
Hamna jipya kwake, kaangukia pua kakosa fikra mpya. Menegment yake fikra za kimaono nil.
 
Nieleweshe mkuu hiyo sponsa unayo isema ww niip, mfano show za mikoan hua hakuna hiyo kitu,mbona kuna kampun kibao mikoan hua wanajipanga kwaajili ya kufany hizo mambo kwa wasanii wengine na si mondi au yeye ana nn kama sio kulinga
Hizo kampuni za mikoani ni kama zipi kwa mfano?!

Kama ni hizi kampuni za kawaida zitaishia kudhamini shows za akina Young Dee peke yake lakini sio mtu kama Diamond. Diamond amekupunguzia sana labda 20M. Huwezi kurudisha 20M kwa kutegemea viingilio vya mlangoni!

Chukulia ile show ya Mombasa mwaka jana! Diamond alilipwa Sh. 5 million za Kenya! Shilingi milioni 5 za Kenya ni takribani sh. 100 Million za Tanzania! Kampuni gani kwa hizi za mikoani italipa hiyo pesa?! Na ni kutokana na huo ukweli ndio maana hata Kenya Diamond huwa anaitwa kwenye festivals au big shows kwa sababu zinakuwa na sponsors. Mathalani, show ya hivi karibuni aliyopiga Nairobi!

Kwa Tanzania chukulia mfano wa show ambayo alipiga Iringa! Ile ilikuwa full sponsored na Vodacom!!! Aidha mwaka jana hiyo hiyo alipiga show Kyela kwenye ufunguzi wa Ngonga Beach Resort! Hii hapa namba ya simu ya Ngonga: 0712 169 669. Wapigie jifanye unataka ku-book room wakutajie bei zao halafu uone kama kwao kumpa show Diamond ingekuwa tatizo!!! Mwakajuzi alipiga show Leaders... hii ilikuwa full sponsored na Tigo!!!

In short, sio mikoani tu... hata Dar es salaam shows za Diamond zimeshakuwa adimu labda aamue kufanya pro bono jambo ambalo ni gumu!!

Na hii sio kwa Tanzania tu... sehemu nyingi shows zinazohitaji wasanii wakubwa lazima zipate sponsorships kutoka kampuni kubwa kubwa!!!
 

Shabiki namba moja wa Diamond ni mama ake ,acha kujivisha hicho cheo
 

Hizo sababu zake ndo zinazomuweka mbali na mashabiki! , kwani hao wakina Babutale na Salama k hawawezi kuandaa show wenyewe wakazunguka mikoani kupiga mfano Kirumba, sokoine , majimaji, mtwara, arusha ,kigoma n.k kweli uongozi wake wanashindwa tu gharama za kuwasafirisha kundi la wasafi na gharama za malazi ambazo zitarudi kila show?

Lengo la hizo show iwe kuwaburudisha wapenzi wake na asiweke masilahi mbele sana japo pia atapata pesa nyingi kwa kiingilio cha 10,000 kwenye viwanja vya mpira.

Narudia tena team ya Diamond wanauwezo wa kuandaa show sema ni kujidekeza na kutudharau tu mshabiki wao
 
Huezi kuwa shabiki WA mondo mtoa nyuzi acha ujinga

Nyimbo ametowa mondo in Bonge la dude kama hujui
Huezi fananisha Na ile rimix ilioshia Morogoro tu

Watu wanaenda Na wakati
Msaniii kama diamond anajua nifanye nini
 
Zinamweka mbali na mashabiki according to wewe au?! Unamaanisha nini hasa unaposema hizo ndizo sababu zinazomweka mbali na mashabiki?!

Btw, kwanini Diamond awe ndie wa kuandaa pro bono shows na sio mwingine yeyote yule?! Kiba alishawahi kuandaa show kama hiyo? Vanessa alishawahi kuandaa show kama hiyo? Jux alishawahi kuandaa show kama hiyo?! n.k, n.k, n.k!!!
 
Una muono mzuri sana joh, Labda one day anaweza kubadilika kama tukiendelea kumwambia hivi,

hatumuombei aanguke ila kama wasikilizaji tunataka kile kilicho bora,

umetolea mfano wimbo wa NALIA umenikumbusha mbali sana.
I miss old Diamond kwa kweli.
Mnajua watanzania/walimwengu hamana shukran na wala hamkosagi vyakuongea

kwa mfano akitoa nyimbo kama hzo unazotaka ww sijui NENDA KAMWAMBIE, NALIA NA MENGI
mtakuja hapa kudai kwamba DIAMOND habadiliki kila siku anatoa ngoma dizain moja Na mtaanza kumnanga hatotoboa kimataifa TUACHE POROJOOO
 
Kama ulimsikia juzi akiwa anahojiwa xxl amelizungumzia hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…