Napataje barua ya uthibitisho wa safari? Ili kupata passport?

Weka 300k mezani mambo ya barua utasikia kwa jirani

Nimetumia 170 tu ila iyo ela akiweka ndani ya wiki tu kapata kama ana haraka ila kama huna haraka atumie pesa kama yangu ndani ya mwezi kaipata
Changamoto inakuja kwenye uthibitisho wa safari Mimi sina haraka sana na passport nataka kuondoka December this Year
 
Jaza fomu, andika nchi unayoenda ni Malawi. Unaenda kutembea tu kama Mtalii. Ingia online fanya booking ya hotel, ambatanisha booking ya hotel. Booking iwe kuanzia miezi mitatu toka sasa.

Sio kila msafiri anakuwa na mwenyeji anakoenda. Wewe mwenyeji wako ni hoteli.
 
Changamoto inakuja kwenye uthibitisho wa safari Mimi sina haraka sana na passport nataka kuondoka December this Year
Nenda pale uhamiaji kurasini kwenye zile stationary watakusaidia ila uwe na ela ya maji usilete ubahili au kama leseni unayo ndio inakua rahisi zaidi kupata tena haifiki hata laki2 gharama
 
Changamoto inakuja kwenye uthibitisho wa safari Mimi sina haraka sana na passport nataka kuondoka December this Year
Pasiport haikupi uthibitisho wa safari, Vifuatavyo ni vigezo vya wewe kupata Passport hakuna uthibitisho wa safari wa barua ya mwaliko.:-

MAHITAJI YA MWOMBAJI (RAIA WA KAWAIDA)​

Nyaraka Muhimu:​

  1. Cheti halisi cha kuzaliwa au kiapo cha kuzaliwa (affidavit).
  2. Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au Namba ya NIDA.
  3. Picha mbili za pasipoti (passport size) – background ya bluu.
  4. Barua ya utambulisho kutoka kwa mtaa/kata au mwajiri (kama unaajiriwa).
  5. Kitambulisho cha mzazi/mlezi (kwa waombaji wenye umri chini ya miaka 18).
  6. Ada ya maombi:
    • TSh 130,000 (kwa pasipoti ya kawaida ya kurasa 34)
    • TSh 150,000 (kwa pasipoti ya kurasa 50)
 
Changamoto inakuja kwenye uthibitisho wa safari Mimi sina haraka sana na passport nataka kuondoka December this Year
we endelea kua mgumu na 150k yako utaipata kwa shida sana,kama uko serious mwaga pesa otherwise utajikuta unatumia pesa na bado hupati kitu.
 
Hello Fellas
Nataka kuchukua passport kwa ajili ya matumizi ya baadae

Changamoto inakuja kwenye barua ya uthibitisho wa safari

Sina invitation letter nataka kuwa na passport in case anything happen natembea ughaibuni

Naombeni njia za kupata barua ya uthibitisho aiseee.
Sijui uko wapi mkuu, ila ungelikua Moshi ni rahisi sana kupata Passport, hautoitumia zaidi ya laki 2 kama Kila kitu Kiko sawa, I mean kama Majina ya vyeti vyako e.g cha kuzaliwa na Cha mzazi na Nida zako hayatofautiani huku huhitaji hizo invitation letter, Mimi niliandikiwa barua ya utambulisho kutoka Kwa mkuu wangu ninakofanyia kazi, aliandika ninaenda Kwa program exchange Kenya basi sikuombwa invitation nyingine
 
Hello Fellas
Nataka kuchukua passport kwa ajili ya matumizi ya baadae

Changamoto inakuja kwenye barua ya uthibitisho wa safari

Sina invitation letter nataka kuwa na passport in case anything happen natembea ughaibuni

Naombeni njia za kupata barua ya uthibitisho aiseee.
Mbona hicho kigezo walisema hakipo tena siku hizi maana wanataka kila Mtanzania mwenye uwezo wake umiliki passport? Hayo ya kutakiwa barua umeambiwa na nani?
 
Hello Fellas
Nataka kuchukua passport kwa ajili ya matumizi ya baadae

Changamoto inakuja kwenye barua ya uthibitisho wa safari

Sina invitation letter nataka kuwa na passport in case anything happen natembea ughaibuni

Naombeni njia za kupata barua ya uthibitisho aiseee.
Jitangaze kuwa wewe ni 🌈 huko tinder. Utapata mialiko ya kutosha toka Arabuni
 
Hello Fellas
Nataka kuchukua passport kwa ajili ya matumizi ya baadae

Changamoto inakuja kwenye barua ya uthibitisho wa safari

Sina invitation letter nataka kuwa na passport in case anything happen natembea ughaibuni

Naombeni njia za kupata barua ya uthibitisho aiseee.
Nenda uhamiaji waambie unataka kwenda kutalii -- bank uwe na vijihela kadhaa peleka bank statement, kama huna hela tafuta hata ndugu mwenye uwezo chukua ya kwake awe kama ndo aliyekupa ofa ya kwenda kutalii

Nchi ya sample chagua hata angola.

Komaa hakuna kutoa rushwa mkuu -- inawezekana bila rushwa
 
Barua ya mwaliko sio lazima.

Unatakiwa kuwa na barua ya mtendaji wa mtaa wako unaoishi au barua ya mwajiri wako kama unafanya kazi sekta binafsi au umma, na wala hiyo barua haihitaji kueleza kwamba unasafiri au vp inatakiwa kusema tu kuwa huyu mtu ni fulani na ashughulikiwe ombi lake bhas.

Watanzania tuache uwoga, vitu vingine kuvipata ni rahisi na wala havihitaji gharama yoyote bali ni kutambua na kuwa na taarifa sahihi.
 
Uhamiaji kule wanakupiga mkwala ukienda kizembe, unaulizwa unaenda wapi--- ukisema unataka uwe nayo tu wanakugomea
 
Kwa ushauri kuhusu maombi ya Scholarships, VISA, Passport, BRELA na Leseni za biashara waone Bright and Genius Editors.
 
Uhamiaji kule wanakupiga mkwala ukienda kizembe, unaulizwa unaenda wapi--- ukisema unataka uwe nayo tu wanakugomea
Ni kwenda kujiamini na kuwavimbia, bila kufanya hivyo hutoboi.

Mimi nilikwenda na hiyo barua ya mtendaji tu na nilikomaa kuwa nitasafiri wakati ukifika na walinipatia passport before 2 weeks.

Unajiuliza hii nchi watu ni wazima kweli? Iweje kuomba passport mpaka barua ya mwaliko na wakati tuna nchi tunasafiri bila Visa?
 
Watumishi wetu wana akili ndogo sana mkuu.

Yule mama mkuu wa uhamiaji alihojiwaga ITV katika kipindi cha dakika 45, suala hilo akalijibu kisiasa tu.

Naam kama ulivyosema jamaa achukue mbenu za wadau haoa akakomae tu- hakuna kutoa rushwa akaze tu
 
Back
Top Bottom