Napataje barua ya uthibitisho wa safari? Ili kupata passport?

Haya mambo si hata ya kuuliza, hii kitu wanamalizaga hapo hapo . Inabidi ueleweke tu
Siku hizi rushwa haiombwi maana kila kitu unafanya mwenyewe online unaenda tu kupitishiwa wilayani na baadaye ngazi ya mkoa, na uzuri ni kwamba ukianza kuapply imekupa muda wa siku 30 hata kama kuna details hauna unazifuatilia unazipata unaambatanisha muda unatosha kabisa bila kutoa pesa yoyote. Pale wilaya ndo wanakupa control no unalipia efu20, mkoani wakipitisha inatoka control no unamalizia laki na 30 unakaa wiki 2 unaitiwa kuchukua
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Hakuna kitu kama hicho achaneni na story za juu juu, mwenye uhitaji aingie online ajaze na kuambatisha kila kinachohitajika vizuri aende kwa afisa wilayani aone kama atakutana na hizo stories, watu mmezoea ku make conclusions kwahadithi za kusimliwa! I'm speaking from experience na kuna member nshawasaidia humu wakafuata taratibu zote zinazotakiwa na passport wakapata baada ya 2wks bila usumbufu wala rushwa
wewe unabishia experience mbaya za kwetu ndio tatizo --- sisi tunasisitiza mtu kujipanga kutokana na vikwazo wengi tulivyovipata

swali hili alishawahi banwa boss wa uhamiaji yule mama pale ITV katika kipindi cha DAKIKA 45, alafu we unachukulia poa mkuu --- na akapiga siasa tu
 
Siku hizi rushwa haiombwi maana kila kitu unafanya mwenyewe online unaenda tu kupitishiwa wilayani na baadaye ngazi ya mkoa, na uzuri ni kwamba ukianza kuapply imekupa muda wa siku 30 hata kama kuna details hauna unazifuatilia unazipata unaambatanisha muda unatosha kabisa bila kutoa pesa yoyote. Pale wilaya ndo wanakupa control no unalipia efu20, mkoani wakipitisha inatoka control no unamalizia laki na 30 unakaa wiki 2 unaitiwa kuchukua
nyinyi wa mkoani sjajua utaratibu wenu upo vipi --- uliza wa UHAMIAJI HQ
 
Na tunaotaka passport kama hitaji la kuomba master's scholarships tunatumia mbinu gani wakuu?

Maana kuna scholarships nyingne katika documents za maombi passport ni lazima
 
Tanzania ni nchi ya kifala haijawai tokea yan passport tu inavipengele kama sijui fomu ya kugombea uraisi inavyotolewa moja 😂😂😂, very stupid
Sio nchi ni namna tunavyo pata viongozi. Viongozi wa kura za wizi kazi yao ni kuwaza wizi tu.
 
Hakuna kitu kama hicho achaneni na story za juu juu, mwenye uhitaji aingie online ajaze na kuambatisha kila kinachohitajika vizuri aende kwa afisa wilayani aone kama atakutana na hizo stories, watu mmezoea ku make conclusions kwahadithi za kusimliwa! I'm speaking from experience na kuna member nshawasaidia humu wakafuata taratibu zote zinazotakiwa na passport wakapata baada ya 2wks bila usumbufu wala rushwa

Siku hizi rushwa haiombwi maana kila kitu unafanya mwenyewe online unaenda tu kupitishiwa wilayani na baadaye ngazi ya mkoa, na uzuri ni kwamba ukianza kuapply imekupa muda wa siku 30 hata kama kuna details hauna unazifuatilia unazipata unaambatanisha muda unatosha kabisa bila kutoa pesa yoyote. Pale wilaya ndo wanakupa control no unalipia efu20, mkoani wakipitisha inatoka control no unamalizia laki na 30 unakaa wiki 2 unaitiwa kuchukua
Acha kuleta ujuaji kwamba hakuna hizo blah blah watu wanazozishuhudia, Immigration Wameoza kuanzia kwa DGI wao, ukitaka kihalali lazima uwe na Supporting Doc zilizo nyooka na hiyo hazitoshi, tena kama utakua una asili ya mikoa ya pembezoni ya nchi ndio utakutana na mambo mengi , na hata ukisema unataka kwenda Zambia, au Kenya hapa kwa Mganga watakulazimisha uchukue Temporary Passport ya mpakani.

Njia nyepesi na nzuri kama hataki kutoa chochote kwa wale maafisa mavi asiombee hapo Dar,. Kama anamuda akaombee mikoa ambayo Haina heka na ambayo sio karibu na mipaka ya nchi za jirani kuepusha maswali ya ubini na asili.
 
Hakuna kitu kama hicho achaneni na story za juu juu, mwenye uhitaji aingie online ajaze na kuambatisha kila kinachohitajika vizuri aende kwa afisa wilayani aone kama atakutana na hizo stories, watu mmezoea ku make conclusions kwahadithi za kusimliwa! I'm speaking from experience na kuna member nshawasaidia humu wakafuata taratibu zote zinazotakiwa na passport wakapata baada ya 2wks bila usumbufu wala rushwa
Mkuu naomba website yao ya kujaza hizo form
 
Mkuu naomba website yao ya kujaza hizo
Ingia Google andika immigration itakuja website yao kwenye vile vya kuchagua utachugua e service, utaingia kwenye passport application, ingia ombi jipya anza kujaza
 
Acha kuleta ujuaji kwamba hakuna hizo blah blah watu wanazozishuhudia, Immigration Wameoza kuanzia kwa DGI wao, ukitaka kihalali lazima uwe na Supporting Doc zilizo nyooka na hiyo hazitoshi kama utakua unasili ya mikoa ya pembezoni ya nchi , na hata ukisema unataka hata kwenda Zambia, au Kenya kwa Mganga watakulazimisha uchukue Temporary Passport ya mpakani.

Njia nyepesi na nzuri kama hataki kutoa chochote kwa wale maafisa mavi asiombee hapo Dar,. Kama anamuda akaombee mikoa ambayo Haina heka na ambayo sio karibu na mipaka ya nchi za jirani kuepusha maswali ya ubini na asili.
Wewe binafsi umekutana nazo au na wewe unasimuliwa maana kitu unachokisema hapa kuna member kama wawili na wameshapata hizo passport waliaminishwa hivo hivo kabla ya uthubutu ila kile nlichowaelekeza walifanya na walizipata kirahisi kabisa ndani ya wiki mbili na nje ya member pia ninao ushahidi. Utajikuta kumuogopesha mwenzio weee kwa jambo la rumors
 
Shida sio fomu, ukishafika ofisi ya uhamiaji ndo ngonjera hizo unakutana nazo --- lazima uwe na plan ya kuruka vihunzi,

Kwenye yale madirisha usipokuwa majini kila ukienda wanakurudishia fomu yako
Kwenye yale madirisha majamaa wana very trick questions aiseee ukijichanganya tu utafanya maongezi yawe mareeeeefu mno

Jamaa aliniangalia tu akaniuliza swali moja tu mbona kama sio mzaliwa wa huko maana mie nimeoa huko kwenu nikamuuliza sehemu gani maana mi natokea sehemu fulani akadai ye hata hapajui na maongezi yakaishia hapo nikaambiwa tu nikalipie dirisha la mwisho kwa ajili ya kupiga picha
 
  • Thanks

naam, nenda rudi pale ni kawaida sana
 
Wewe binafsi umekutana nazo au na wewe unasimuliwa maana kitu unachokisema hapa kuna member kama wawili na wameshapata hizo passport waliaminishwa hivo hivo kabla ya uthubutu ila kile nlichowaelekeza walifanya na walizipata kirahisi kabisa ndani ya wiki mbili na nje ya member pia ninao ushahidi. Utajikuta kumuogopesha mwenzio weee kwa jambo la rumors
hakuna mtu anasema haiwezekani mkuu -
 
Ukiwambia unaenda kikazi watataka details za kampuni inayotaka kukupa kazi.

Ukisema unaenda kutalii watakwambia uwaonyeshe tiketi,(go and return) hotel utakayofikia.

Njia nyepesi ni ya mualiko wa mtu wa nje..

Njia Nyepesi zaidi ni ile ya MKONO MTUPU HAULAMBWI..
Sasa mkuu utakata ticket ya ndege bila kuwepo na Passport na uta booking vipi hoteli wakati hauna Passport mkononi je ukigosa vigezo vya kupata Passport ukiambiwa Siyo Mtanzania maana uhamiaji kukupa kesi sekunde tu.
 
Sijakutana na icho kitu mimi tena barua plus kujaza fomu nilijaziwa na kuandikiwa na huyo huyo afisa wa uhamiaji nikampooza na 30 kama asante
Hello,unaweza kunisaidia mawasiliano yake ,kama yupo Dar, passport yangu imezuiliwa,sina barua kutoka kazini,I'm jobless kwa sasa!!?.
 
Back
Top Bottom