Napataje barua ya uthibitisho wa safari? Ili kupata passport?

Tengeneza barua ya uongo kwamba kuna mtu yupo south africa anakualika.
Mfano wake uwe

" Kumamoto Masumbuko
1002 Fiona Street
P.o Box 12
Ridged Way
Johansburg
2091
ZAF

Kwa
Kamishna Generali wa Uhamiaji
P.O.Box 000
Dodoma
TANZANIA

YAH: KUMWALIKA IDDI AMINI MAMA KUJA KUNITEMBELEA AFRIKA KUSINI

Mimi kumamoto Masumbuko ambaye ni Raia wa Afrika ya kusini nategemea kumwalika Iddi Amini Mama aje kunitembelea Afrika ya Kusini.
Iddi Amini Mama ni raia wa Tanzania na rafiki yangu wa siku nyingi niliyefahamiana naye nilipokuja kutembea Tanzania Mwaka 2024.

Nategemea kumwalika Iddi Amini Mama aje kunitembelea huku Afrika Ya kusini kipindi cha krismax mwaka 2025 .

Gharama zote za safari ya Iddi Amin Dada nitagharamia mimi na atafikia nyumbani kwangu

Kumamoto Masumbuko
South Afrika"

Jiandae kwa maswali mengi sana kama mlifahamiaje na kumamoto, anaishi wapi, una namba yake ya simu ,tunaweza kumpigia.
Ila kama hutaki mambo mengi tafuta vishoka wapo wengi pale kurasini uķiwatoa Laki wanakutengenezea kila kitu wewe unabaki kulipia na kwenda kupigwa picha na kuchukuliwa alama ya vidole unabaki kusubiri passport
 
Haya mambo si hata ya kuuliza, hii kitu wanamalizaga hapo hapo . Inabidi ueleweke tu
 
Weka 300k mezani mambo ya barua utasikia kwa jirani.
Na atapata ndani siku kadhaa kabla week haijaisha. Cha msingi kama unacheti cha kitaaluma ambatanisha,hata sababu isipokuwa inamashiko hicho cheti kitakubeba
 
Wakati unaomba usiseme matembezi Bali unaenda kikazi kwenye kazi barua ya mualiko hapana ila ukisema matembezi lazima upate barua ya aliyekualika
 
Mzazi amezaliwa mwaka 1945 cheti cha kuzaliwa anatoa wapi
 
Waambie umeipata mwenza mkenya so utafanya safari mara kwa mara. Hutodaiwa tiketi Wala barua.
 
Usiseme umealikwa we sema unaenda kutembea dubai ( Vacation)
 
Wakati unaomba usiseme matembezi Bali unaenda kikazi kwenye kazi barua ya mualiko hapana ila ukisema matembezi lazima upate barua ya aliyekualika
Ukiwambia unaenda kikazi watataka details za kampuni inayotaka kukupa kazi.

Ukisema unaenda kutalii watakwambia uwaonyeshe tiketi,(go and return) hotel utakayofikia.

Njia nyepesi ni ya mualiko wa mtu wa nje..

Njia Nyepesi zaidi ni ile ya MKONO MTUPU HAULAMBWI..
 
Mkuu kwa mfano ukiwaambia unaenda matembezi hapo south africa na hauendi na ndege bali gari binafsi watasemaje
 
Ikiwa upo kazini TZ ofisi yako Inaandika barua ya kukutambulisha kuwa wewe ni mfanyakazi ...hawatahitaji barua ya nje namaanisha uwe unafanya kazi Tz tu hiyo inatosha
 
Tanzania ni nchi ya kifala haijawai tokea yan passport tu inavipengele kama sijui fomu ya kugombea uraisi inavyotolewa moja 😂😂😂, very stupid
 
Shida sio fomu, ukishafika ofisi ya uhamiaji ndo ngonjera hizo unakutana nazo --- lazima uwe na plan ya kuruka vihunzi,

Kwenye yale madirisha usipokuwa majini kila ukienda wanakurudishia fomu yako
 
Ikiwa upo kazini TZ ofisi yako Inaandika barua ya kukutambulisha kuwa wewe ni mfanyakazi ...hawatahitaji barua ya nje namaanisha uwe unafanya kazi Tz tu hiyo inatosha
Hapo ni sahihi.. Nilidhani unawambia umepata kaz nje ndio unaomb passport kwenda.
 
Sikutoa hata 100.
Niliwaambia naenda kufuatilia familia ya kaka yangu Uganda.
Wakanisumbua nikafuate living certificate zangu za secondary school.
Hapo ninacho cheti cha kuzaliwa na vinginevyo.
Nikawaleta wakanipa mkoba wangu.
Hii gia mimi ilikwama walitaka niwape details na vielelezo vya watu huko napoenda, next week nikaenda upya kama mtalii🤣🤣🤣
 
Shida sio fomu, ukishafika ofisi ya uhamiaji ndo ngonjera hizo unakutana nazo --- lazima uwe na plan ya kuruka vihunzi,

Kwenye yale madirisha usipokuwa majini kila ukienda wanakurudishia fomu yako
Hakuna kitu kama hicho achaneni na story za juu juu, mwenye uhitaji aingie online ajaze na kuambatisha kila kinachohitajika vizuri aende kwa afisa wilayani aone kama atakutana na hizo stories, watu mmezoea ku make conclusions kwahadithi za kusimliwa! I'm speaking from experience na kuna member nshawasaidia humu wakafuata taratibu zote zinazotakiwa na passport wakapata baada ya 2wks bila usumbufu wala rushwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…