Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sioni upenyo wa huyu jamaa na wenzake kupatikana wakiwa salamaSo sad mkuu,, inasemekana jamaa "kapotezwa"
Na Makonda lipotangaza wauza madawa wako wengi polisi, mkamwona mbaya!!
Shabikia tu lakini siku yakikugusa direct au indirect utakuja kusimulia aina ya uongozi tulionao kwa sasaWatanzania wengi hawana akili kama yako, wengi wanaangalia upande mmoja na ndio wanaitwaga nyumbu!!
mtu yeyote anaweza kufanya uhalifu na akataka ukitokea muwaze aliyefanya ni mwingine
Ndoto yako yaweza kuwa kweli lakini ngoja nikapige ramli kwa mganga nijue km ni kweli au noooSo sad mkuu,, inasemekana jamaa "kapotezwa"
so haina shida, amejitoa sadaka au??
Wa upande huo msijione mko salama kiviiiiiile, wakimaliza huku watahamia huko, Nani aliamini kuwa Nape angeweza kudhalilishwa na kutishiwa kupigwa risasi na wana usalama?
Joh makiniLeta defender/Leta wajeda/
Leta wagambo Roma nimejitoa sadaka/
na mkitaka kuniua hakikisha sifii hapa/
Nichinjeni mkanitupe daraja la Mkapa /
Viva Roma vivaaaa
Vivaaaa roma vivaaaa aa eeeh
Bendera Bendera [emoji445][emoji445][emoji445]
Kuua watu hakutaisaidia serikali bali kuhatarisha amani ya nchi.
Ikiwa leo ni siku ya pili tangu ilipotolewa taarifa kuwa msanii Roma Mkatoliki alitekwa na watu wasiojulikana akiwa pamoja na Moni Centrozone, mtayarishaji wa muziki wa Tongwe Records, Bin Laden katika studio za Tongwe Records, Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemlilia msanii huyo.
Nape emetoa kilio chake kupitia ukurasa wake wa Twitter, akitumia maneno matatu pekee yanayosomeka kwa hisia za ndani kuwa ni mtu anayemlilia mpendwa wake.
“Roma! Oooooh No!” ametweet Nape.
Mbunge huyo wa Mtama ameongeza nguvu kwa kilio cha wadau wa muziki pamoja na wasanii waliotumia mitandao ya kijamii kushinikiza ifahamike alipo msanii huyo na wenzake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na uongozi wa Tongwe Records, watekaji walifika katika studio hizo na kuwahoji waliokuwepo, kisha kuondoka nao wote pamoja na baadhi ya vifaa vinavyotumika kurekodia muziki, kwenda kusikojulikana.
Mke wa Roma, Nancy ameeleza kuwa alifika katika vituo kadhaa vya polisi jijini Dar es Salaam kuulizia taarifa za mumewe, lakini alielezwa kuwa taarifa za Roma hazikuwepo.
Akizungumza kwa uchungu kwenye vyombo mbalimbali vya habari, Nancy aliwaomba Watanzania kwa ujumla pamoja na vyombo vya usalama kusaidia kufahamu alipo mumewe.
“Serikali, waandishi wa habari, Watanzania, yeyote aliyeona, aliyesikia, anayeweza kutusaidia Roma yuko wapi naombeni msaada wenu,” alisema.
Leo mchana, wasanii wamekutana katika studio za Tongwe Records kwa lengo la kuzungumzia suala hilo zito ambalo limevunja mioyo ya wadau wa muziki, familia na ndugu wa Roma na wenzake.
Weusi hawana cha kukamatiwa.Joh makini
Niki Wa II
Ney Wa mitego wakae vizuri
Hali si shwari