Nape Amlilia Roma Mkatoliki, ‘Ooooooh No!’

Nape Amlilia Roma Mkatoliki, ‘Ooooooh No!’

usalama wa wananchi upo wapi.na hii tabia ya kuchukuwaa watu bila taarifa za ndugu na jamaa .si ngeni kwa mtindo huu.je wajibu wetu kama raia kujua sheria.
huyu ni roma leo kila mtu anataka kujua.je makapuku kama sisi..?
 
Hii tabia ya uvamizi wa studio na utekaji imeshakomaa sasa lazima ikomeshwe.
 
Watanzania wengi hawana akili kama yako, wengi wanaangalia upande mmoja na ndio wanaitwaga nyumbu!!


mtu yeyote anaweza kufanya uhalifu na akataka ukitokea muwaze aliyefanya ni mwingine
Shabikia tu lakini siku yakikugusa direct au indirect utakuja kusimulia aina ya uongozi tulionao kwa sasa
 
Daaaah...!!! Mbona haya mambo kipind cha nyuma hayakuwepo kwann kipind hiki ndo yamekuwa yakitokea na hakuna anayechukua hatua stahiki si vyombo vya dola wala si viongozi wanaohusika na masuala haya...!!! Tunaelekea wapi watanzania...?????
 
2 days zishapita. So alisilimia za kuwapata wakiwa hai zinazidi kupungua tu. Ndio maana wakawabeba wote kupoteza ushahidi wa ni nani hasa amewachukua. Ila Mungu atawalipia tu
 
Wa upande huo msijione mko salama kiviiiiiile, wakimaliza huku watahamia huko, Nani aliamini kuwa Nape angeweza kudhalilishwa na kutishiwa kupigwa risasi na wana usalama?

mimi ni mpinzani na nitakuwa hivyo!! usiweke watu upande fulani kwa sababu ya kupishana mawazo, ni dalili ya kutojiamini ( inferiority)

my take ni alimaanisha nini?? wakati anaimba?? na statement hiyo haitoshi kwa maadui zake kuchukua chance na mwenye akili kamza zako akawaza seriali inahusika??

kamon!! you are better than that
 
Leta defender/Leta wajeda/
Leta wagambo Roma nimejitoa sadaka/
na mkitaka kuniua hakikisha sifii hapa/
Nichinjeni mkanitupe daraja la Mkapa /


Viva Roma vivaaaa
Vivaaaa roma vivaaaa aa eeeh

Bendera Bendera [emoji445][emoji445][emoji445]
Joh makini
Niki Wa II
Ney Wa mitego wakae vizuri
Hali si shwari
 


Ikiwa leo ni siku ya pili tangu ilipotolewa taarifa kuwa msanii Roma Mkatoliki alitekwa na watu wasiojulikana akiwa pamoja na Moni Centrozone, mtayarishaji wa muziki wa Tongwe Records, Bin Laden katika studio za Tongwe Records, Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemlilia msanii huyo.

Nape emetoa kilio chake kupitia ukurasa wake wa Twitter, akitumia maneno matatu pekee yanayosomeka kwa hisia za ndani kuwa ni mtu anayemlilia mpendwa wake.

“Roma! Oooooh No!” ametweet Nape.


Mbunge huyo wa Mtama ameongeza nguvu kwa kilio cha wadau wa muziki pamoja na wasanii waliotumia mitandao ya kijamii kushinikiza ifahamike alipo msanii huyo na wenzake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na uongozi wa Tongwe Records, watekaji walifika katika studio hizo na kuwahoji waliokuwepo, kisha kuondoka nao wote pamoja na baadhi ya vifaa vinavyotumika kurekodia muziki, kwenda kusikojulikana.

Mke wa Roma, Nancy ameeleza kuwa alifika katika vituo kadhaa vya polisi jijini Dar es Salaam kuulizia taarifa za mumewe, lakini alielezwa kuwa taarifa za Roma hazikuwepo.

Akizungumza kwa uchungu kwenye vyombo mbalimbali vya habari, Nancy aliwaomba Watanzania kwa ujumla pamoja na vyombo vya usalama kusaidia kufahamu alipo mumewe.

“Serikali, waandishi wa habari, Watanzania, yeyote aliyeona, aliyesikia, anayeweza kutusaidia Roma yuko wapi naombeni msaada wenu,” alisema.

Leo mchana, wasanii wamekutana katika studio za Tongwe Records kwa lengo la kuzungumzia suala hilo zito ambalo limevunja mioyo ya wadau wa muziki, familia na ndugu wa Roma na wenzake.
Kuua watu hakutaisaidia serikali bali kuhatarisha amani ya nchi.
 
Vip kuhusu yule mwenyekiti kule pwani aliepigwa risasi ,ali tweet pia?

Au yule hakua binadamu
 
Back
Top Bottom